Ni halali kutuma pesa za matumizi kwa mama wakati mke wangu yupo kwake?

Wewe hebu achana na uharo wako njoo na hoja
Kama uko menopause hasira zako hazina faida yeyote kwangu na sihitaji msaada wako
Unaweza nipa msaada gani wewe
Jiheshimu kunguni
Sijibizani na wehu.... kwaheri
 
Muache arudi kwao,ndiko kwenye Uhuru zaidi.
 
umeongea point! Ila uliposema "mkamwana" nikacheki na id yako hahah

super!
 
Kuna namna mke wako anasauti kwako means ni kama amekupanda kichwani hivi.
 
Muwe mnaacha ujuaji na maneno makali ya kijinga, mpaka anampeleka ukweni walikubaliana haikuwa lazima, kufika huko ndo anabadilisha gia angani kwa sababu za kijinga.
Angekua na shida toka mwanzo angeenda kwao
Ona litoto lingine hili ,kuwa na akili mkeo hawezi kuwa anapendwa kikweli na mama yako ,wanawake huwa ni maadui by nature inatakiwa amtembelee akiwa mzima tena asizidishe siku 3 kwa mama yako watatengezeana bifu ,naongea kwa uzoefu kama unaakili itakuokoa mahali,kukubaliana kwenda kujifungulia kwa mama asiye mama yake? Unajua purukushani za kuzaa ww?? Ashasema huwa anatoa matumizi alishindwa nn kumpeleka kwao mkewe akawa huru na furaha na mtu waliye free naye ,huyu bado qnachukua ushauri wa mama kwenye ndoa ,ukishaoa wazazi wako pia ni maadui wa ndoa yako ,sababu wanapambana ww usihame kwenye utawala wao ,mke ataacha kwa ,kijana ataacha kwao wataaambatana ,we mfano unadhani mdogo wako wa kiume anafurahi umeokota limwanamke tu ghafla linanafasi kuliko yeye aliekujua toka utoto,unadhani gubu la mawifi ni kuwa mawifi ni wabaya ? Ile ni asili kuna ugomvi wa dada zako na mkeo wa kisaikolojia wanagombeq upendo wako.

Mwanaume halisi unatakiwa umlinde mkeo na ndugu ,wazazi nq marafiki,kwani kaka mara ngapi marafiki ukioa wanachukia ukianza waacha baa unamuwahi wife??
Ndoa inataka mtu ngangali sio unakaa sikiliza sikiliza watu
 
Wala sijajihangaisha kusoma after the first sentence..... so kaa na ujinga wako
 
Naweza kuwa Hovyo ila nyie watoto wa mama hamuwezi kuelewa. Mke wako ndio wa kuambatana nae mama yako atapewa hela na mume wake ya kuhemea.

Tena kimsingi kama mkwe yuko pale ilitakiwa mama ndio amhudumie maana ni mgeni., Umasikini wa familia zetu ndio unatufanya tugomnaie hizo elfu mbili mbili za mboga.
 
Mkuu,kwanza elewa. Kaenda kutembea au kapelekwa na shida zake?
Je,kama kwao na mwanaume hawajiwezi,huyo mama anaetakiwa kumtunza mkwewe,amtunze na nini?

Elewa basi. Mwanaume kakili hali si shwali na ameomba hifadhi kwa mda. Ni vyema unaelewa familia hizo ni za kiswahili,hazijiwezi. Umejaribu kupima uzito lakini wa mke kupewa hela na kuamua alipopelekwa waishije?

Kama wewe ni mwanaume wa kuambatana na mkeo na kumuacha mama yako,una matatizo. Kabla hujazaliwa,enzi wanawake wana heshima na adabu. Leo hii mnaoa au mnaokota?
Huyo mzazi hajalaimisha kupewa pesa,lakini mwanaume imembidi kwa sababu anatambua alipompeleka si kwake,hivyo anatakiwa asiharibu. Haya,haribu mahusiano na ndugu na wazazi,af ambatana na chokolaa walo,kesho akikigeuka utajua hujui. Kwa hiyo,anatakiwa asiegemee upande wowote.
 
Mwenye jiko ndiyo atumiwe pesa ya matumizi ya msingi kama vile chakula.

Mkeo akienda kwa mama, mtumie mama pesa ya ku-muaccomodate huyo mwanamke.

Mama akija kuwatembelea, mkeo ndiye mwenye jiko, so yeye ndiye anayepewa fedha ya matumizi.

Mbona ni common sense?

Mke atumiwe fedha ya chakula ilhali yupo ugenini? Yeye anajua nini huko? Kwanza ye mjamzito, pili ni mgeni, tatu, hana haki ya kuwapangia aliowakita huko ugenini namna ya kuishi na nini cha kula.

Kwanini asitulie mama mkwe wake amuhudumie.!
Ukorofi tu!
 
Kama una pesa za kutuma huku na kule umeshindwa nini kukaa na mkeo???

Hiyo ni trela.....mke, mama mkwe, wifi huu utatu utakupasua kichwa mwanaume!!!!
 
Kama una pesa za kutuma huku na kule umeshindwa nini kukaa na mkeo???

Hiyo ni trela.....mke, mama mkwe, wifi huu utatu utakupasua kichwa mwanaume!!!!
DAda hapa hakuna mume nilichogundua bado anaendeshwa na mamake mzazi huyu.ukishindwa mfichamkeo dhidi ya huo utatu huna ndoa
 
Mwanaume ambaye ana akili, hapo mama ni wako mke ni wako sasa wewe ni kubalance mambo la sivyo kitakukomba upande mmoja
 
Najiuliza tu,
Huyo mke angekuwa kwa mama yake na ukawa unatuma pesa zote kwa mama yake, angekuwa na maoni gani?
 
Najiuliza tu,
Huyo mke angekuwa kwa mama yake na ukawa unatuma pesa zote kwa mama yake, angekuwa na maoni gani?
Wewe sasa ndo unajua kuishi na wanawake ,nimemcshangaa sana na nimemwambia huu ndo ukweli ,kaishia kutukana
 
Sioni haja za kubishana mkuu. Kimsingi na ushauri wangu mke wake atumiwe hiyo hela mama akitaka kwenda sokoni apewe hela na mka mwana, Huyo mkamwana ni ubavu wa mwanae, sawa na mwanae.
Usimdharau mke wako eti akitaka hela ya kununua hata pedi amuombe mama mkwe, akitaka kwenda sokoni kuhemea amuombe mama hela. Yaani vijana wa siku hizi hovyo kabisa

Kama unampenda sana mama yako au baba yako pls usioe. Sisi vijana wa zamani tunayajua haya mambo vizuri ile vijana wa leo munapangiwa na mama zenu wanawaamulia hadi yasiyowahusu kwenye ndoa zenu.

Hamna maamuzi mbele ya wake zenu mama akishaamua.

kwa sisi wakristo Biblia inasema utawaacha wazazi wake uambatane na mkeo, sio wazazi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…