Ni harufu ya ufisadi tu! Mikataba mikubwa ya trilioni ya pesa haiwekwi wazi na wala Bunge hatusikii likihusishwa. Tunaibiwa tushtuke kabla ya 2025

Ni harufu ya ufisadi tu! Mikataba mikubwa ya trilioni ya pesa haiwekwi wazi na wala Bunge hatusikii likihusishwa. Tunaibiwa tushtuke kabla ya 2025

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Huwezi ukaingia mkataba mkubwa kama huu wa kuchakata gesi Lindi kimya kimya kama unaenda kuuza machungwa. Trilioni 70 ni uhai wa taifa letu.

Tunatakiwa kuambiwa ukweli juu ya huu mkataba. Ufafanuzi wa kinagaubaga na kujadiliwa na Bunge.

Hiyo mikataba iliyosainiwa Oman ni mashaka matupu. Maana kuna janja ya kutaka kurejesha usulutani wa Oman kuja kutuibia sisi watanzania weusi.

Kwa nini isainiwe bila ufafanuzi wa kina namna tutavyonuofaika?

Harufu mbaya inayotia mashaka inafoka.
 
Nishasemaga, hawa kenge wanajua sisi ni simba wa makaratasi, sisi wazee wa malalamiko mitandaoni, ndio maana bado wanafanya vimbwanga, Tanzania ya leo wanaitafuna, hawajali kuhusu kesho, wao wameshawaandalia vizazi vyao mema ya nchi.

Kelele hizi za chura(sisi) hazimzui tembo(viongozi) kunywa maji(keki ya taifa) [emoji23]
 
Mikataba iwekwe wazi , wawakilishi wa wananchi wajue kwakuwa kazi yao ni kusimamia nakuishauri serikali kama kweli mikataba hiyo imezingatia maslahi mapana ya Taifa ,,,
 
Inashangaza sana kusaini mkataba mkubwa kama huo haraka kisiri siri. Inawezekana hatupati hata senti tano.

Kama una manufaa,faida kwa Watanzania kwanini hatuuweki wazi. Kama una manufaa kwa Watanzania utapendwa na kuungwa mkono.

Unajua JPM alituambia tutapata nini kwenye mikataba yote ya madini. Aliweka wazi vyote, wenye akili timamu tuliona manufaa kwetu na vizazi vyetu.

Simple wangefuata same principles, mikataba ile ile kwa rasilimali zetu zote. Waarabu, wazungu wanafanya hivyo.

Nahisi kila kipengele kwao walisema ndio, wakiangalia matumbo yao na asilimia kumi zao.

Kwanini kuwe na kigumumizi kuweka mikataba muhimu kwa Taifa wazi?

Loliondo inaunzwa kwa majangili kuwinda na kuchukua wanyama jinsi wanavyojisikia. Hakuna nchi inayojitambua ingefanya huu ujinga.

Kama wanyama wamezidi, wanasumbua wakulima anzisha mbuga mpya, wapeleke huko. Tuna mapori ya kutosha.

Kwanza walisema watauza vitalu na wanyama, wamebadilisha na kusema watauza wanyama hai. Maneno tofauti lengo lao ni lile lile. Kuuza wildlife.
 
Wamasai laki moja wamejengewa nyumba 100 Handeni.

Nyumba maja waishi 1000? pia compesation haiko vizuri, kutoa watu kwenye eneo walioishi miaka 1000 na zaidi nakuwalipa pesa mbuzi haijakaa sawa.

The whole issue haijakaa sawa na serikali imeonyesha kutojali kabisa haki za Wamasai, maswali, concerns zao Watanzania wote kwa ujumla.

Democracy, human right ni nini? Serikali iko kwa ajili gani? ya nani? Wawekezaji?
 
Samia siyo kiongozi mwenye kujali maslahi ya Tanzania.

Hata akiigiza ionekane kuwa ni kiongozi anayyewajali waTanzania, itaonekana tu kwamba anaigiza!

Wanachoweza kufanya waTanzania kwa watu hawa wasiokuwa na uchungu na nchi hii na watu wake, ni kuwatapisha mali zote watakazokuwa wamejikusanyia huko mbele ya safari.

Inabidi wajue hivyo, kwamba watazitapika tu, muda ukifika. Hata wazifiche nje ya nchi, zitatafutwa zirudishwe kwa wananchi.
 
Huwezi ukaingia mkataba mkubwa kama huu wa kuchakata gesi Lindi kimya kimya kama unaenda kuunza machungwa. Tril 70 ni uhai wa taifa letu.

Tunatakiwa kuambiwa ukweli juu ya huu mkataba. Ufafanuzi wa kinagaubaga na kujadiliwa na bunge.

Hiyo mikataba iliyosainiwa Oman ni mashaka matupu. Maana kuna janja ya kutaka kurejesha usulutani wa Oman kuja kutuibia sisi watanzania weusi. Kwa nini isainiwe bila ufafanuzi wa kina namna tutavyonuofaika.

Harufu mbaya inayotia mashaka inafoka.
Oman wataakuja kutuibia ni
ni Tanzania?
Oman wa enzi ya kina Barghash na hii ya Sasa ni tofauti ya mbingu na ardhi
 
Mikataba iwekwe wazi , wawakilishi wa wananchi wajue kwakuwa kazi yao ni kusimamia nakuishauri serikali kama kweli mikataba hiyo imezingatia maslahi mapana ya Taifa ,,,
Kwahiyo hiyo mikataba ikipelekwa kwa wawakilishi wa wananchi wataipinga??
 
Sultan aliiba Nini, au historia imekuchenga
 
Na Bunge la kujadili huo mkataba ni hili hili la kikundi cha KIJANI.......?
 
Huwezi ukaingia mkataba mkubwa kama huu wa kuchakata gesi Lindi kimya kimya kama unaenda kuunza machungwa. Tril 70 ni uhai wa taifa letu.

Tunatakiwa kuambiwa ukweli juu ya huu mkataba. Ufafanuzi wa kinagaubaga na kujadiliwa na bunge.

Hiyo mikataba iliyosainiwa Oman ni mashaka matupu. Maana kuna janja ya kutaka kurejesha usulutani wa Oman kuja kutuibia sisi watanzania weusi. Kwa nini isainiwe bila ufafanuzi wa kina namna tutavyonuofaika.

Harufu mbaya inayotia mashaka inafoka.
Mikataba ya ndege,sgr,Bwawa la Nyerere nk viliwekwa wazi? Jumla ni Til.ngapi?
 
Back
Top Bottom