Inashangaza sana kusaini mkataba mkubwa kama huo haraka kisiri siri. Inawezekana hatupati hata senti tano.
Kama una manufaa,faida kwa Watanzania kwanini hatuuweki wazi. Kama una manufaa kwa Watanzania utapendwa na kuungwa mkono.
Unajua JPM alituambia tutapata nini kwenye mikataba yote ya madini. Aliweka wazi vyote, wenye akili timamu tuliona manufaa kwetu na vizazi vyetu.
Simple wangefuata same principles, mikataba ile ile kwa rasilimali zetu zote. Waarabu, wazungu wanafanya hivyo.
Nahisi kila kipengele kwao walisema ndio, wakiangalia matumbo yao na asilimia kumi zao.
Kwanini kuwe na kigumumizi kuweka mikataba muhimu kwa Taifa wazi?
Loliondo inaunzwa kwa majangili kuwinda na kuchukua wanyama jinsi wanavyojisikia. Hakuna nchi inayojitambua ingefanya huu ujinga.
Kama wanyama wamezidi, wanasumbua wakulima anzisha mbuga mpya, wapeleke huko. Tuna mapori ya kutosha.
Kwanza walisema watauza vitalu na wanyama, wamebadilisha na kusema watauza wanyama hai. Maneno tofauti lengo lao ni lile lile. Kuuza wildlife.