Ni harufu ya ufisadi tu! Mikataba mikubwa ya trilioni ya pesa haiwekwi wazi na wala Bunge hatusikii likihusishwa. Tunaibiwa tushtuke kabla ya 2025

Chakushangaza, ni ulivyojua hata hayo mapunjo, Umejua mpaka "Ammendments"??...na kama ilikua siri ina maana sasa sio siri tena....Huo ni uwazi.
Tumejua wameshapitisha hatukutoa maoni wengi, wabunge hawakupewa muda wa kujadili zaidi ya dakika chache sana kazi kwisha, sasa hata kama Nia ni nzuri je huo ndio uwazi tunaopigania??

Matokeo Yake vipengele vinanyofolewa Kila siku maana hawakuuandaa kwa umakini walikurupuka, mfano kipengele Cha arbitration sheria ilisema zifanyikie Tanzania ila imebidi kifutwe na sasa itakua huko huko kwa mabeberu!!!

Hayo yote yasingekosewa kama uwazi ungekuwepo
 
Ahsante kwa Taarifa.
 
Nani alihoji mikataba ile ya ununuzi wa ndege? Magufuli alikuwa mpuuzi kwelikweli
 
 
Hata makubaliano kati ya Barrick na serikali anayajua mwendazake kaburini na Propesa jalala Kabudi..
Hawajawahi kuyaweka wazi.
Lakini waungwana Wanasemaga we learn through mistakes !!

Au ni vyema tuendelee tu kama walivyokuwa wakifanya wengine ??!

Ni lini Usimba na Uyanga kwenye maslahi ya Nchi tutauweka pembeni ??!
Najaribu kutafakari tu ! Maana kila mtu anapotoa maoni kwa mfano kuhusu ubadhirifu wowote ule watakaopinga wataelekeza mashambulizi kwa awamu iliyopita !!

Sasa hii itaenda hivi mpaka lini !! Na tunafanya hivi kwa maslahi ya nani ??!

Najaribu kutafakari tu. !!
 
Mind boggling .....
Nimeweza kuwaona wale waliokuwa wakiteta, kuhusu Lissu, Akwilina(R.I.P) na ripoti ya CAG wakiwa kimya!
Yani kuna wakati walitaka tuingie barabarani...lakini .hili la DAR-ES-SALAAM Kha! ....tunaambiwa hatujui kiingereza, hatujasoma vizuri mistari ......uwongo, ukweli, ,Rushwa, wizi, geresha, kabumba.... ali mradi tu!

Ndii Watanzania tujue hatujui!


Sihami Nchi lakini, mumu humu
 
Ukihama Nchi Maana yake ni muoga unayakimbia matatizo πŸ˜…πŸ™πŸ™
 
Tukumbuke kuwa;
1. CCM wanapoingia mikataba yoyote kipaumbele cha kwanza ni MATUMBO yao (Ubinafsi)
2. Mkataba huu tayari ulishasainiwa tena hukohuko ughaibuni, hapa wanakuja kuupitisha tu kwa bunge dhaifu la chama chao (ccm) wenye malezi ya RUSHWA.
3. Wanachoangalia hawa CCM ni kupata fedha za kupigania uraisi wa mwaka 2025 na kuacha maslahi ya Taifa!
4. Ni ngumu mno kutofautisha kati ya RUSHWA na CCM kwani hawa ni NDUGU tena MAPACHA
 
Ufisadi upi Magufuli alifanya unajua huu unafiki na uzushi mnaoufanya mitandaoni mkiongozwa na mihemko ya chuki na visasi
Tukiandika ufisadi wa mwendazake hapa sidhani kama nafasi itatosha!
Aliiba!, alipora! alinyanganya! alikwapua! tena kaa kimya!
 
Haya yote yanatokea kwa sababu ya uoga wa wanachi tunaogopa kufa. inafikia mahali kila mtu anatetea uhai wake laiti tungekuwa na ushirikiano nje ya mitandao ya kijamii, haya yote yasingetokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…