Ni hatari sana kwa nchi kutegemea ushauri wa Legal Officer (Hamza Johari), na kuiingiza nchi kwenye mkataba

Mkuu, sijui sasa nikuite nani wewe, Samia ni rais pekee ambaye anafanya jambo ambalo halijawahi kufanywa na mtu mwingine yeyote kwa nchi yetu. Kama wewe, kwa sababu zako mwenyewe hulioni hili, usipende kufanya na wengine wasilione uhalisia wake ulivyo.

Nyaraka si hiyo hapo mnayopenda kuiita "makubaliano"?

Sasa kama wewe unasoma na kuona hakuna ubaya wowote na nyaraka hiyo, wacha nasi wengine tutumie akili zetu alizotujaalia Mwenyezi Mungu kuisoma nyaraka na kuielewa ilivyo andikwa.
Sisi tunasoma na kuelewa maandishi hayo kama yalivyowasilishwa na kuona ubaya uliomo ndani yake.

Kuwa Rais wa nchi hakumfanyi huyu rais kutufanya tusiwe na akili za kuelewa anayonuia kuyafanya juu ya nchi yetu. Huyu rais hakupewa madaraka ya kutunyamazisha, au kuziba akili zetu; kama asivyokuwa na mamlaka ya kuzuia asiondolewe madarakani kama anavuruga nchiyetu. Uwezo huo hana.
 
Nirudie tena kwa mara nyingine.
Usifikiri sisi wengine wote hatujui "vita ya kiuchumi" ni jambo gani.
Hapa hakuna vita ya kiuchumi, ni uporaji wa madaraka ya waTanzania juu ya mali zao,... ni ukoloni mpya wa aina yake.

"DPW ajipange" vyovyote anavyotaka, lakini sisi hatutaki ajipange kututumia sisi kama nyenzo ya kupigana vita yake hiyo unayoizungumzia wewe.
Sisi kama sisi, vita yetu ni kulinda usalama wa nchi yetu, na kuhakikisha maslahi yetu hayachezewi na yeyote.

Hizi porojo zako hazina mvuto kabisa.
 
Huu ni ulimwengu wa kibiashara, na huwezi kuendelea kwa kuwa na mawazo ya kipuuzi kama haya ya kwako.

Rwanda na Congo wameshasaini makubaliano ya kufanya biashara na hao DP, ina maana wao hawaogopi uporaji wa mali za kwao?, kumbuka hao ni wenye mali wenyewe sisi tunatumika kama nchi ya kusafirishia tu huo mzigo.

Wenye kutakuwa kuja na maoni ya kuchekesha kama haya ya kwako ni wao sio sisi kama nchi.

DPW analeta ufanisi bandarini hapo, anakuja kufunga mitambo ya kisasa inayokwenda kurahisisha kazi nzima ya bandari. Unaweza ukasema huwataki hao jamaa ukiwa mtu wa mitandaoni tu.

Lakini huwezi kueleweka kwa mfanyabiashara anayeitumia bandari hii mara kwa mara kwa hoja zisizo na mashiko kama hizi za kwako.

Hakuna anayetaka kukutumia wewe kama nyenzo ya kupigana vita yake, hizi ni akili hasi za kitanzania, akili za wanaharakati ambazo haziitazami dunia halisi na mahitaji yake.
 
Anayesema nyaraka hazina matatizo ni wanasheria wazalendo Hamza Johari na Dr Possi walioshiriki kuziandaa wakiwa pamoja na wanasheria wa DPW na wapo tayari kutetea hoja zao wakihitajika mahali popote.

Samia anao mtazamo wake unaokwenda na wakati tuliopo, Nyerere alikuwa na wa kwake uliokuwa na haki kwa miaka ile, Mwinyi akawa na wa kwake wenye mashiko wakati wa urais wake.

Pia ukumbuke kuwa SSH ni mrithi wa JPM, hakuna kipya anachokifanya ni muendelezo wa sera zile zile alizoachiwa na hayati.

Marais huja na mitazamo yao wanapoingia ikulu, Samia aliamua KAZI IENDELEE na akawabakisha baadhi ya wasaidizi aliowakuta toka awamu ya tano.

Chuki zenu za kijinga hazina msaada wowote.
 
"...Ulimwengu wa kibiashara" nani kahoji hilo kama siyo kutoelewa kinachojadiliwa hapa?

Biashara unafanya huku ukiwa mjinga bila kujua inakuingiza shimoni kama anavyofanya Samia?

Toka mwanzo ni kama huelewi kinachojadiliwa katika swala hili. Kila mara mnageuza mambo, mnapoezwa mnazua mengine ambayo hayahusiani kabisa na kinachojadiliwa.

Inabidi niachane na wewe; kwa sababu naonha huna jipya la kuongeza thamani kwenye mjadala huu.
Imebaki kupotezeana muda tu, nami sina muda huo wa kupoteza.
 
Muda sio mrefu DPW wanaingia kazini pale bandarini, wakiwaachia majungu ya mitandaoni.
 
Muda sio mrefu DPW wanaingia kazini pale bandarini, wakiwaachia majungu ya mitandaoni.
Huo hautakuwa mwisho wa swala husika, na hata wewe unalijua vizuri hili.

Kwa hiyo waje wasije, hiyo siyo hatma ya jambo husika. Samia ataondoka na kuna wazalendo wanazaliwa kila siku ndani ya nchi hii.

Na ninakuomba usisahau, hakuna msiba usiokuwa na mwenzake. Jambo hili linaweza kuwa ndio utakao liokoa taifa hili kutoka kwenye makucha ya CCM hii mbovu iliyotufikisha hapa. Hilo ni la maana zaidi, kuliko ujio wa DPW.
Mkuu 'steve', sijui nikuage mara ngapi?
 
Maneno ya mkosaji yapo miaka na miaka. Roho ya upinzani huwa haifi hilo kila mtu analifahamu.

Samia anataka kuongeza pato la taifa ili tuweze kutatua matatizo mengi ya ndani kwa uwezo wetu wenyewe.

Hakuna anayependa kujidhalilisha kwa hao wazungu kila siku kupanda ndege kwenda kuomba misaada huko EU na World Bank, hayupo anayependa kujishusha kiasi hicho.

Huyo Mbowe miaka ya 2000 alikuwa mwanaharakati wa magazetini, akiandika mawazo kama hayo ya kwako, mpaka leo ni kiongozi wa CDM anayeelekea uzeeni. Siasa za uanaharakati zipo pale pale na hazitaacha kuwepo hata baada ya mimi na wewe tukiwa tayari tumeshafukiwa.

Shida za wananchi na zenyewe zipo pale pale, zinahitaji utatuzi kuliko hizi kelele nyingi za uanaharakati ambazo muda mwingi msingi wake ni hao hao wafadhili wanaotoa pesa zao.
 
Hamza ni corporate lawyer. Alianza kama mwanasheria wa kawaida pale Tritel Arusha, akaja mamlaka ya anga TCAA katika kitengo cha haki za walaji [consumers] akatuma maombi ya kazi ya mkurugenzi mkuu wa anga enzi za JK na akafaulu vizuri.

Akafanyiwa mtimanyongo na aliyekuwa mkurugenzi wa anga wa wakati ule aliyekuwa na ukaribu na Mwakyembe aliyekuwa waziri wa uchukuzi, kwani Rais JK alikubali awe mkurugenzi na akaidhinisha lakini jina lake likawekwa kabatini pale wizarani, mambo yale yale ya roho za kwanini na wivu wetu wa kitanzania.

Alipoingia JPM akamuona katika moja ya vikao vya kiserikali akaamua kumpa nafasi ya ukurugenzi wa TCAA, amekuwa sehemu ya negotiations teams za serikali.

Kuanzia suala zima la mgogoro wa Malawi na Tanzania wa Ziwa Nyasa na serikali yetu ikaibuka mshindi baada ya wanasheria wa Malawi kuingia mitini jumla.

Ameendelea kuwa mwanasheria wa serikali na mmoja wa washauri wa Rais JPM na sasa Samia.
 
Samia anataka kuongeza pato la taifa ili tuweze kutatua matatizo mengi ya ndani kwa uwezo wetu wenyewe.
Naona unaendelea kunikaribisha.

"Kuongeza pato" kwa gharama gani. Ya kuwapeleka waTanzania utumwani?

Naona sasa unajifanya kuwika sana, kwa sababu hujui kuwa usiku huu utakuwa kitoweo.
Kama katika mawazo yako unaona tayari kuna "wakosaji" fikiri tena vizuri kujua mkosaji ni nani.
Hakuna anayependa kujidhalilisha kwa hao wazungu kila siku kupanda ndege kwenda kuomba misaada huko EU na World Bank, hayupo anayependa kujishusha kiasi hicho.
Mbona tayari Samia anajidhalilisha kwa kwenda kuwekwa kimada Dubai wiki kadhaa huku akilisaliti taifa analoliongoza yeye. Kwa vile kaenda kwa waarabu?
 
Aiseeee!

Sasa nimekusoma vizuri zaidi na kukufahamu.

Hebu soma tena ule mstari wa mwisho wa andiko lako hilo hapo juu.

Mara nyingi huwa sikosei katika kutambua tabia halisi za watu kutokana na maandishi wanayoweka humu ndani.
sasa tazama kama hili hapa.
Si nilishasema tayari uhusiano kati yako na huyo Hamza?

Hapa sioni lolote la maana sana alilonalo Hamza aliyeelezewa hapa.
 
Akili za chuki kwa jinsia ya kike wakati wewe mwenyewe ni mwanamke, unashangaza sana aisee.

Kuongeza pato kwa ufanisi wa hapo bandarini. Kushusha meli nzima ndani ya siku moja au mbili hamuoni kwamba ni suala jema sana kwa sababu hamna biashara yoyote ile mnayoifanya yenye kuwapa uelewa wa masuala ya meli.

Mnashangaza sana namna mnavyopinga uwekezaji yaani mnapambania kushindwa kwa rasilimali yenu wenyewe kwa faida ya wakenya na wasumbiji!.
 
Maadam umeonyesha kwenda upande huo, sasa nimeamua twende sawasawa; nimeondoa ile kukuaga kwa vile nilishajua huna kitu kichwani.
Sasa nipo tayari kukabiriana na chizi, vyovyote utakavyotaka twende kwa pamoja.

Wewe ni mmoja wa wapuuzi wote niliokwishakutana nao humu jukwaani, kwa hiyo sitakuacha utambe na ukichaa wako huo.
 
Pamoja na uchizi unaodai mimi ninao sitaacha kutetea awamu ya Samia, pia sitaacha kutetea uwekezaji wa DPW nikiwa najua lengo haswa la serikali ni lipi.

Nikiwa mtu nayefahamu masuala ya bandari naelewa faida wanazokwenda kupata wadau halisi wa bandari kwa kupata aina ya mwekezaji mwenye teknolojia za kisasa.

Nawasikitia wadau hawa wa masuala ya bandari kwani wana bahati mbaya ya nchi hii kuendekeza siasa za kipumbavu ambazo zina malengo binafsi yasiyohusiana kabisa na shughuli zao za kila siku.
 
Hakuna anayekuzuia kutetea, hata kama unachotetea ni upumbavu ulio wazi kabisa.

"Lengo la serikali" umekwisharudiarudia hapa na kuelezwa kwamba hilo siyo tatizo kama kweli nia ndiyo hiyo, bado hutaki kuelewa. Kwa hiyo ni wazi kabisa kwamba wewe hutetei hilo "lengo" ambalo wengi hawalipingi.

Upumbavu ni huo wa kudhani watu hawaelewi upotoshaji, na hata uongo unapoelezwa kwenu hamuukiri, badala yake mnaendelea tu kukaza shingo na kueleza uongo mwingine.

Mtu mwenye akili timamu hadi wakati huu angekuwa alishaelewa kwamba uongo ulishatambulika na hao wanaotakiwa kuukubali uongo huo kuwa ndiyo kweli

Jisikitikie mwenyewe, kwani ufisadi wenu umekataliwa. Kama hapo bandarini kuna mapapa ya mafisadi (na kwa uhakika yapo), nyinyi mlitaka kutumia bandari nzima na kuitoa mikononi mwa waTanzania ili kiwe ni kitega uchumi wenu wa siku nyingi.
Mpango huo umevurugwa, ndiyo sababu upo hapa ukiandika uchafu tu humu kama aliyerukwa na akili.

haya mafisadi ya siku nyingi hapo bandarini, dawa yao ni ndogo tu, kwa kiongozi mwenye upeo amaboo Samia hana kabisa.

Haya yatashughulikiwa na Bandari itafanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa.

DPW siyo pekee mwenye ujuzi huo. Hilo liondoe akilini mwako, hata kama ni mjomba wako.
 
Tatizo lako ni uwakala wa hizo taasisi za kimagharibi, hivyo upande wako unaeleweka,

Hautegemewi kukubaliana na mpango wa kiserikali. Unapotosha kadri unavyoweza.

Nakuhakikishia tu kwamba huu uwekezaji una manufaa kiuchumi kuliko hizi propaganda unazoleta humu jukwaani.

Na jambo zuri hucheleweshwa tu lakini ni lazima litatimizwa.
 
Wakili ni mwanasheria mwenye mamlaka ya kutetea kesi mahakamani na kuandaa nyaraka za kimahama na pia anaweza kutoa ushauri wa kisheria.

Mwanasheria ana uwezo wa kutoa ushauri wa kisheria na kuandaa nyaraka chini ya usimamizi wa wakili.

Kuna tofauti nyepesi sana kati ya wakili na mwanasheria.
 
Nakubaliana na wewe ila hiyo tofauti siyo nyepesi,unawezaje kujiita 'mwanasheria mbombezi' kwenye legal fraternity wakati hata hauko competent ku-appear mahakamani ,kufanya attestation n.k
 
Wakilia ni mwanasheria mwenye mamlaka ya kutetea kesi mahalamani na kuanda nyaraka za kimahama na pia anaweza kitoa ushauri wa kisheria.

Mwanasheria ana uwezo wa kutoa ushauri wa kisheria na kuandaa nyaraka chini ya usimamizi wa wakili.

Kuna tofauti nyepesi sana kati ya wakili na mwanasheria.
Nakubaliana na wewe ila hiyo tofauti siyo nyepesi,unawezaje kujiita 'mwanasheria mbombezi' kwenye legal fraternity wakati hata hauko competent ku-appear mahakamani ,kufanya attestation n.k
Kubobea kwenye sheria ni kuwa na uelewa mpana wa sheria na hili hufanyika kwa kufanya utafiti pamoja na kusoma sana.

Mahakamani ni hatua ya mwisho sana. Na hata katika sheria tunasema ushindi na presentation nzuri hutegemea na namna utafiti ukivyofanyika.

Hao mawakili uwaonao wazuri wengi hufanyiwa research na legal officers.

Ni Tanzania tu ambapo competency inapimwa kwa vyeti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…