Ni hatari sana kwa nchi kutegemea ushauri wa Legal Officer (Hamza Johari), na kuiingiza nchi kwenye mkataba

Duh!
Sikujua kuwa ulikuwa thismuch shallow!
God have mercy upon us.

This is it! Kumbe huna kitu kabisa.
Shallow ni wewe unayetumia nguvu kubwa kupinga huu uwekezaji ukiwa huna wazo lolote mbadala lenye kuweza kujenga nchi.

Shallow ni wewe ambaye siasa za nchi hii zinaamua kukustahi zikimheshimu Baba yako mzazi na mchango wake wa uwaziri katika awamu ya Mwinyi na Mkapa.

Shallow ni wewe ambaye hujui upana wa uharibifu unaouleta kwenye nchi yako kwa kuamua tu kupinga kila kinacholengwa kufanyika.

Mungu katika ukuu wake na akusamehe yote unayoyafanya dhidi ya Taifa lako mwenyewe.
 
Ungeyasema haya kuhusu Samia, ambaye alikuwa ni Makamu wa Rais, ningekushangaa; lakini naona umeepana kuangukia kwingine.

Sasa ninakuunganisha na huyo Hamza, pengine itakuwa ni wewe mwenyewe, au uko karibu sana na huyo mtu.
Samia hakujipeleka ikulu yeye mwenyewe amepelekwa na katiba ya JMT aliyoapa kuilinda na kuisimamia kwa kipindi chake chote cha urais.

Na hayupo pale kwa dhana nyepesi za kuwa kiongozi dhaifu, hana huo udhaifu na yupo very strategic katika kila anachokifanya. Udhaifu ninaoungelea ni huu wa jamii pana ya watu kukubali kupotoshwa na kupoteza muda kwenye mijadala isiyo na kichwa wala miguu wakati majirani zetu wanaweza kabisa kuamua kutumia options nyingine za kuingiza pesa kupitia bandari.
 
TAAA inachohitajika Mkurugenzi sio lazima awe mwanasheria mnatuchanganya. Hamza wa TAAA alihusika vipi mkataba wa ikulu na DP World
Hamza ni bosi wa TCAA sio TAAA, ni mwanasheria aliyechukuliwa na hayati Rais Magufuli ili awe msaidizi wake wa karibu kwenye masuala ya sekta ya anga. Akawa ni mmoja wa washauri wa masuala mengi tu wakati wa awamu ile.

Amerithiwa na Samia na anaendelea kuwa mtu wa karibu wa maamuzi ya kiserikali yanayofanyika ikulu.
 
Weka hapa huo ushahidi wako, umewekewa link hapo juu huyo unayemtetea yumo?
Ninamfahamu Hamza tangu mwaka tisini na sita tukiwa masomoni Ukraine miaka ile. Sihitaji kupitia hizo link.

Ni corporate lawyer aliyeshiriki kwenye kufanya negotiations nyingi za kiserikali ikiwemo lile suala la mpaka wa Malawi kwenye Ziwa Nyasa wakati wa Rais Jakaya Kikwete.
 
Hamza ni bosi wa TCAA sio TAAA, ni mwanasheria aliyechukuliwa na hayati Rais Magufuli ili awe msaidizi wake wa karibu kwenye masuala ya sekta ya anga. Akawa ni mmoja wa washauri wa masuala mengi tu wakati wa awamu ile.

Amerithiwa na Samia na anaendelea kuwa mtu wa karibu wa maamuzi ya kiserikali yanayofanyika ikulu.
Kwa nini yeye atumike kufanya kazi ambazo zinamhusu moja kwa moja Mwanasheria mkuu wa serikali?!
 
Shallow ni wewe unayetumia nguvu kubwa kupinga huu uwekezaji ukiwa huna wazo lolote mbadala lenye kuweza kujenga nchi.

Shallow ni wewe ambaye siasa za nchi hii zinaamua kukustahi zikimheshimu Baba yako mzazi na mchango wake wa uwaziri katika awamu ya Mwinyi na Mkapa.

Shallow ni wewe ambaye hujui upana wa uharibifu unaouleta kwenye nchi yako kwa kuamua tu kupinga kila kinacholengwa kufanyika.

Mungu katika ukuu wake na akusamehe yote unayoyafanya dhidi ya Taifa lako mwenyewe.
Umejuaje kuwa "sina wazo mbadala", kama siyo yale yale ya kuonyesha kuwa ngazi yako ipo chini sana?

Hayo mengine yote ni takataka zile zile ambazo sasa unahusiana nazo humu JF.

Huna kitu mkuu. Sikuiti tena na majina yako hayo ya bandia.
 
Samia hakujipeleka ikulu yeye mwenyewe amepelekwa na katiba ya JMT aliyoapa kuilinda na kuisimamia kwa kipindi chake chote cha urais.
Kuna mahali popote ndani ya katiba panapoonyesha kuwa rais anayo madaraka ya kugawa vipande vya nchi kwa nchi nyingine?
 
Utangulizi:
Katika taaluma ya sheria kote dunia, na kwa kipekee hapa nchini Tanzania, ili mtu akidhi vigezo vya kuwa mshauri, au kuwakilisha watu mahakamani, au kushauri mambo msingi ya kisheria , au kuhakiki nyaraka mbalimbali ni lazima awe na taalum hiyo katika ngazi au nafasi ya uwakili.

Hivyo kwa sababu ni taaluma, ina taratibu zake kuweka kutambulikwa na jumuia wa wataaluma hao katika nchi, kwa mathalani wale waliomaliza shahada za sheria kabla ya 2007 walifanya mitihani iliyotambulika kama bar exams , na wale waliomaliza baada ya 2007 shahada zao, ilianzishwa shule ya sheria kwa vitendo (law school of Tanzania.)

Katika mifumo hiyo yote wanaofaulu wanaomba kupokelewa, na Jaji Mkuu akiwakubalia wanaapishwa na kufanywa kuwa jumuia ya mawakili, wakiwa na majukumu mbalimbali, kama mawakili, mafisa viapo, na waidhinisha nyaraka mbalimbali katika jamii; na mawakili wanaweza kuwa wakujitegemea au mawakili wa serikali.

Kama hujapitia hatua hizo hata ungekuwa una LLD (PhD), LLM. LLB, unaitwa legal officer, na chochote unachotaka kukifanya lazima uwe chini ya wakili (either private or public), kwa sababu hautambuliki kama member in professional fratenity na huna comitment za obligation ya taaluma hiyo. na hivyo ushauri wako sio ushari

Utata:
Ukifuatilia sintofahamu ya Bandari, chimbuko lake kubwa ni mkataba na wala si uwezo wa DP world kama inavyoelezwa na waunga hoja wa waarabu hao, na kimsingi mkataba ni kazi ya sheria moja kwa moja, na yeyote anayetaka kuzungumzia mkataba lazima arejee sheria, au awe na background ya sheria, aidha za mikataba mbalimbali, ikiwepo za ndani na za nje, au uwezo wa kisheria kiujumla.

Kumekuwa na mwanasheria ambaye amejinasibu kuwa alishiriki katika mchakato na kushauri, swali langu Je, "mwanasheria" huyo ni wakili? (private or public) (is he a member of professional fratenity in Tanzania? Jibu ni hapana Hamza Johari si wakili(public or private) inawezekana ni mwanasheria kwa maana labda ana LLD, LLM, LLB, lakini si wakili, na si lawyer by professional, labda ni mwanasheria kwa kumaliza degree za sheria. lakini haonekani katika kanzi data za mahakama (data base) za judiciary.

Kulijua hilo ingia kwenye (tovuti ya mahakama) www.ewakili.judiciary.go.tz. kuna sehemu ya kumjua wakili wako, (know your advocate) ingiza majina utagundua si wakili.

Wale mnaolaumu wanasheria, tujiulize kwanza, Je aliyetoa ushauri wa kisheria ni mwanasheria kwa mujibu wa taaluma yetu ya kisheria?

Na kama si hivyo, aliwezaje kufanya kazi asiyokuwa na taaluma nayo?
Si judiciary hufanya favor kwa executives, sasa usishangae kuona legal officer akifanyakazi ya Hakimu...
 
Umejuaje kuwa "sina wazo mbadala", kama siyo yale yale ya kuonyesha kuwa ngazi yako ipo chini sana?

Hayo mengine yote ni takataka zile zile ambazo sasa unahusiana nazo humu JF.

Huna kitu mkuu. Sikuiti tena na majina yako hayo ya bandia.
Wewe ni wakala tu wa World Bank, na ni taasisi kubwa inayopinga DPW na wawekezaji wote wa kiarabu na kutoka mashariki kina China.

Ni vita nzito na umechagua kuwa upande wa Magharibi dhidi ya upande unaokuwa kiuchumi wa mashariki.

Ongea mengi lakini watu wanakujua pengine kuliko unavyodhani.
 
Kuna mahali popote ndani ya katiba panapoonyesha kuwa rais anayo madaraka ya kugawa vipande vya nchi kwa nchi nyingine?
Hakuna hata mita moja ya mraba ya Tanzania ambayo SSH ameigawa kwa mtu yoyote, hizi ni siasa nyepesi za fitina ambazo zimezoeleka miaka hii yenye ushawishi mwingi kutoka taasisi kama World Bank.

Vita ya bandari sio ya kitoto, World Bank sasa hivi wamewakutanisha marais watatu wa huku kusini na wanafadhili ujenzi wa reli mpya ya Angola ili bandari ya Lobito itumike na kazi zote wanakwenda kupewa wamarekani.

Ni njama tu ya kujaribu kutuchanganya sisi tulioamua kwenda na DPW, wanachukia hao wamarekani wanapouona ushawishi wa Nchi za mashariki ukianza kuwafunika katika masuala mengi ya kidunia.

Hawakupenda kombe la dunia lichezwe kule Qatar kwa mfano lakini wenyeji wakawa na msimamo thabiti mpaka kila kitu kikafanyika na kumalizika tena likiwa ni kombe la dunia lililoacha historia kwa ubora wake.

Marekani anaona ushawishi wake duniani unaanza kupotea hivyo anatumia mawakala wake wa kila aina ili kuendelea itikadi zao zilizojaa udhalimu na ushenzi.
 
Sheria ipo kisheria,hebu wabobezi wachakate vzr ili nguvu ya Sheria isimamie vipengere vyake!
 
Wewe ni wakala tu wa World Bank, na ni taasisi kubwa inayopinga DPW na wawekezaji wote wa kiarabu na kutoka mashariki kina China.

Ni vita nzito na umechagua kuwa upande wa Magharibi dhidi ya upande unaokuwa kiuchumi wa mashariki.

Ongea mengi lakini watu wanakujua pengine kuliko unavyodhani.
Aiiiseeeeee!

"Mimi niwe wakala wa WB"?

Tafadhali sana. Unapokuwa huna ufahamu wowote kumhusu mtu, usijaribu kumhusisha na jambo unaloona wewe kuwa linamhusu.
Na kujua mtu unaye mzungumzia, angalau kwa humu JF, njia rahisi ni kutazama maandishi yake anayoweka humu ukumbini.
Mimi nimekuwemo humu miaka mingi, maandishi yangu yapo wazi kabisa siku zote. Umeona wapi, hata mara moja tu tokea uingie humu nikitetea au kushabikia mambo ya WB, kwamba ndio msingi wako wa kunihusisha na Benki hiyo?

Ndiyo maana ninakwambia kuwa uwezo wako wa kifikra ni mwepesi mwepesi sana, pamoja na kwamba hapo mwanzo nilipoanza kukusoma nilidhani kuwa una msimamo maalum, kumbe hakuna kitu.

Kama ni "Uwakala", kama unavyodai wewe, hivi huoni wewe ulivyojipambanua waziwazi kabisa kuwa ni "wakala" katika jambo hili la DPW?

Ngoja nihitimishe hili na wewe ili usiwe na mashaka tena na "uwakala" wangu unapoangukia. "UWAKALA" nilionao, na ninajua ndio nitakaokufa nao ni juu ya Tanzania na maslahi ya waTanzania wote.
Hili hata ufanye nini, hutabadili msimamo wangu juu yake.

Ninakuomba sana unielewe hivyo na usihoji tena ni wapi ninaposimamia.

Samia leo hii akipiganaia maslahi ya nchi yetu kwa dhati, sitakuwa na sababu yoyote ya kumlalamikia, nitamuunga mkono.
Kwa haya anayoyafanya sasa hivi, Samia ni adui mkubwa wa nchi hii na wananchi wake.
 
Hakuna hata mita moja ya mraba ya Tanzania ambayo SSH ameigawa kwa mtu yoyote, hizi ni siasa nyepesi za fitina ambazo zimezoeleka miaka hii yenye ushawishi mwingi kutoka taasisi kama World Bank.

Vita ya bandari sio ya kitoto, World Bank sasa hivi wamewakutanisha marais watatu wa huku kusini na wanafadhili ujenzi wa reli mpya ya Angola ili bandari ya Lobito itumike na kazi zote wanakwenda kupewa wamarekani.

Ni njama tu ya kujaribu kutuchanganya sisi tulioamua kwenda na DPW, wanachukia hao wamarekani wanapouona ushawishi wa Nchi za mashariki ukianza kuwafunika katika masuala mengi ya kidunia.

Hawakupenda kombe la dunia lichezwe kule Qatar kwa mfano lakini wenyeji wakawa na msimamo thabiti mpaka kila kitu kikafanyika na kumalizika tena likiwa ni kombe la dunia lililoacha historia kwa ubora wake.

Marekani anaona ushawishi wake duniani unaanza kupotea hivyo anatumia mawakala wake wa kila aina ili kuendelea itikadi zao zilizojaa udhalimu na ushenzi.
Sasa inabidi nikuonee huruma tu kwa ujinga mkubwa ulio nao.

Kama siyo ujinga unaokusumbua, bali ni kutafuta kutumia hadaa maksudi kupoteza lengo; fahamu kuwa ninao upeo mpana sana wa kujua upuuzi ni upi unapouleta kwangu.

Nina'confirm' ile "shallowness" niliyokupa hivi karibuni. Sikukosea hata kidogo.
 
Aiiiseeeeee!

"Mimi niwe wakala wa WB"?

Tafadhali sana. Unapokuwa huna ufahamu wowote kumhusu mtu, usijaribu kumhusisha na jambo unaloona wewe kuwa linamhusu.
Na kujua mtu unaye mzungumzia, angalau kwa humu JF, njia rahisi ni kutazama maandishi yake anayoweka humu ukumbini.
Mimi nimekuwemo humu miaka mingi, maandishi yangu yapo wazi kabisa siku zote. Umeona wapi, hata mara moja tu tokea uingie humu nikitetea au kushabikia mambo ya WB, kwamba ndio msingi wako wa kunihusisha na Benki hiyo?

Ndiyo maana ninakwambia kuwa uwezo wako wa kifikra ni mwepesi mwepesi sana, pamoja na kwamba hapo mwanzo nilipoanza kukusoma nilidhani kuwa una msimamo maalum, kumbe hakuna kitu.

Kama ni "Uwakala", kama unavyodai wewe, hivi huoni wewe ulivyojipambanua waziwazi kabisa kuwa ni "wakala" katika jambo hili la DPW?

Ngoja nihitimishe hili na wewe ili usiwe na mashaka tena na "uwakala" wangu unapoangukia. "UWAKALA" nilionao, na ninajua ndio nitakaokufa nao ni juu ya Tanzania na maslahi ya waTanzania wote.
Hili hata ufanye nini, hutabadili msimamo wangu juu yake.

Ninakuomba sana unielewe hivyo na usihoji tena ni wapi ninaposimamia.

Samia leo hii akipiganaia maslahi ya nchi yetu kwa dhati, sitakuwa na sababu yoyote ya kumlalamikia, nitamuunga mkono.
Kwa haya anayoyafanya sasa hivi, Samia ni adui mkubwa wa nchi hii na wananchi wake.
Samia anayofanya ni muendelezo wa yale yale aliyofanya hayati JPM na watangulizi wengine wanne.

Tatizo ni siasa zinazojificha nyuma ya maamuzi yake haya ya sasa, pia ni nguvu kubwa ya mataifa makubwa inayotumika kupinga suala hili la bandari.

Mashambulizi kutoka kila upande yanawezeshwa na pesa za hao wanaoona Tanzania inakwenda kupaa kiuchumi, hivyo hayashangazi hata kidogo.

Upotoshaji wa suala zima hili la DPW ni mkakati wenye kueleweka vilivyo. Wanasheria wameshatumia nguvu kubwa sana katika kuelezea mkataba huu kifungu kwa kifungu lakini upingaji wanaokutana nao unakuwa ni mkubwa kwani nguvu iliyo nyuma yake ni kubwa.

Ni vita ya kiuchumi kama alivyowahi kusema hayati JPM lakini Tanzania itaibuka mshindi.
 
Sasa inabidi nikuonee huruma tu kwa ujinga mkubwa ulio nao.

Kama siyo ujinga unaokusumbua, bali ni kutafuta kutumia hadaa maksudi kupoteza lengo; fahamu kuwa ninao upeo mpana sana wa kujua upuuzi ni upi unapouleta kwangu.

Nina'confirm' ile "shallowness" niliyokupa hivi karibuni. Sikukosea hata kidogo.
Unachekesha sana unapotumia kejeli za kingereza na lugha za ukali. Ni wale wale wapotoshaji wanaotumiwa na mataifa tunayoshindana nayo kwenye kutaka kufaidika na biashara pana ya bandari.

Kwa taarifa tu DPW kajipanga kufanya biashara nzima ya logistics kuanzia huko Congo mpaka huko mashariki ya mbali. Na hii vita serikali itashinda asubuhi tu.
 
Back
Top Bottom