Ni hatua gani za kuchukua iwapo hakuna maelewano kwenye ndoa?

Bila kupepesa macho shida ni wewe mwanamke! we mwanamke ndo una uwezo wa kutengeneza hiyo ndoa!
-nimegundua ndoa nyingi kuyumba chanzo ni mwanamke!(yaani hata neno la Mungu lipo wazi)
Wanawake tumepewa huu uwezo wa kujenga na kubomoa!
-wewe hebu jishushe,usishindane na mwanaume!
Mtii,mheshimu,msikilize uone km hatabadirika!
Lkn pia unatakiwa uombe! Lkn kuomba bila kutimiza wajibu hakuna maana Mungu sio mjinga,timiza wajibu wako then omba!
Shida ya wanawake wengi mnataka tu kuitwa mke ila hamtaki kukaa Kwenye nafasi km inavyotakiwa!
-we mwanamke nafasi hizi 4,usipokaa nazo vzr ndoa yako itakuwa majanga,na itakufa..√mke√mama√mlinzi√msaidizi
-Wengi mmekaa nafasi ya mke na mama, hizo mbili ambazo ndo mhimu na zimebeba kila kitu mmeacha na ndo shida inapoanzia!

-wanawake wa sikuhizi kutwa kulalamika,majukumu ya mke hatufanyi ndo maana wanaume wanatafuta amani nje huko!(sio wote ila wengi )
-ss akikutana na ushirikina huko ndoa huna.
-ndoa ni jambo la kiroho kwanza kabla halijawa la kimwili!

-wanaume wengi wasaidizi wao ni michepuko,! ndio,sbb ndo anaambiwa mambo mengi mpk ya miradi na ndo mshauri unategemea nn? We unabaki tu km mke hapo!jmn tubadirikeee!

-yaani km kuna kitu nimejifunza ni kugombana na mume halafu kumnyima ni kumtuma tu nje!

Ila sikuzote nasema inategemea hiyo ndoa uliipataje,km ilikuja tu,easy come easy go!
 
Ni kweli kabisa. Na watu wanaachana wakiwa wanapendana. Ikitokea wakaanzisha mahusiano mengine wanarudi kuwa wapasha viporo wakuu
Hao wanakuwa hawakufikia hali mbaya sana!
 
Mungu akusaidie sana!
Niombee mkeo akae tu Kwenye nafasi yake vzr
 
Yes huyu kaka naekwambia ni mtumishi!
Kuna wanawake wana roho mbaya sana aisee.
DUUUH, Mungu amsaidie huyu sio kabisaaaa, kuna watu wanaishi kwa tabu sana,,,ila utumishi ndio unamuweka hapo

duuuh mie siwezi japo mie Ke
 
Hao wanakuwa hawakufikia hali mbaya sana!
Na hatua mbaya ni pale ambapo uhai wa mmojawapo uko hatarini yaani ndani ni vipigo kwa kwenda mbele. Hali ambayo muomba ushauri hajaisema. Mengine yanatatulika tu wakiamua.

Ikifikia hatua mahusiano yanahatarisha uhai ondoka mara moja
 
DUUUH, Mungu amsaidie huyu sio kabisaaaa, kuna watu wanaishi kwa tabu sana,,,ila utumishi ndio unamuweka hapo

duuuh mie siwezi japo mie Ke
Ndo uone wanawake baadhi walivyo na roho mbaya
 
Karibu kwa ushauri wakitaalamu zaidi hautojutia Asante
 
Ahsantee 😂😂
 
Mimi ilipofika hapo nilikula kimya, yaani kimya! Na ndio falsafa yangu.

Wakati mwingine inanigarimu lakini inanisaidia kujiponya majereha.
 
Unajua ndugu yangu maisha tunaishi mara moja tu, yaani mara moja

Sasa shida ya kukosa amani na furaha kwenye maisha haya mafupi hivyo nini, kwa mtu nilie kutana nae ukubwani? Kwa hivyo viapo visivyo na kichwa wala mguu vya kanisani?
 
Ni kusikilizana tu, lazima mmoja amsikilize mwenzie zaidi.
Mnatakiwa kujifunza unapomkubalia mwenzako kitu haimaanishi ameshinda, ndoa sio mashindano.
 
Umeongea point nzuri sana na nimekuelewa vizuri
 
Mimi ilipofika hapo nilikula kimya, yaani kimya! Na ndio falsafa yangu.

Wakati mwingine inanigarimu lakini inanisaidia kujiponya majereha.

Mkuu jazia nyama kidogo..... Ulipiga Kimya kwa muda gani na je ilikusaidia?
 
Sasa hapo Kuna ndoa? Njia sahihi ni kuachana maana kulea watoto kwenye ndoa kama hiyo ni mbaya zaidi ya kuwa na mzazi mmoja
 
90% ya shida za kwenye ndoa huanzia wakati wa uchumba na huwa mnapuuzia mkiamini baada ya ndoa atabadilika kumbe ndio atayaongeza makali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…