Ni headphone/earphone za brand gani zina ubora wa juu?

Ni headphone/earphone za brand gani zina ubora wa juu?

Rock zircon ile earphones kiboko,saiz hazipo tena,nina kz ed9 lakin naona haifati mziki wa rock zircon,naona wadau wanashauri tupande dau tuacheni na upuuuzi wa low budget hizi [emoji2][emoji23]
Mchawi pesa tu ndugu,ukifikiria headphone ya 900k unawaza TV ya ukutani nchi kadhaa hapo imetulia sebuleni au ada ya mtoto au chochote mbadala wake,ila ndio hivyo kila kitu ni maamuzi tu
 
Mziki wake ni noma sana, very good, battery inakaa vya kutosha, build quality kali sana, with active noise Cancellation... Kwa ufupi they are very good.

Mimi Natumia Sony 1000xm4, kwenye best earbuds duniani, hii Sony 1000xm4 ipo kwenye top 3.

Hizi ni Earbuds zenye Noice Cancellation(ANC), ndio maana bei yake imesimama... but they are very good, huwezi kulinganisha na hizi fekero za 35,000 sijui 90,000.

kwamba za 30k na 90k ni fekero[emoji1787][emoji1787]

hivi mnajua sisi wa zile za elfu 5 tunajiskiaje tukisoma vitu kama hivi!!!!

au mpaka aitwe mod ndio mjue kwamba kuna shambulio mmefanya[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Pia, kuna hizi earphones za Philips, Philips she3800, (nyingi zilizopo mtaani ni fake) original sehem yenye rangi nyeupe imefifia, zinauzwa elfu 10,000)
Ukipata original zake zinalia vizuri Sana, zina deep base, high, mid ,low zinasikika bila shida, na sauti yake haiumizi maskio

Hapo kabla niliwahi kutumia earphones za JBL tune 110t, nikaachana nazo, zinalia kawaida na sauti ya upande mmoja imefifia,

Nikajaribu earphones za Qkz zxn 10pro, nazo sikuzifurahia, ukisikiliza Kwa muda mrefu maskio Yana Uma, zina flat sound , haupati Ile 3d immersive sound.

Pia kuna earphones za Xiaomi piston basic nilitumia Kwa muda, nikaachana nazo, kutokana na kuumiza maskio ukitumia Kwa muda mrefu,

Kipindi cha nyuma niliwahi kuagiza earphones za rock zircon, hizi zilikua zinalia vizuri Sana, Kila tune unaiskia vizuri, haziumizi maskio, Kwa sasa sizioni AliExpress, naona kuna Toleo jingine wanaita rock obsidian, sijajua kama zinalia vizuri kama rock zircon ya zamani.

Hizo earphone za Philips zinalia vizuri zaidi ukitumia rubber/ cover zake.

View attachment 2345763

hizi ndio league zangu sasa,huko kwenye earphone za 700k mnitue kwanza[emoji23]
IMG_0133.jpg
 
Oraimo za 5000 nikisikiliza mziki najihisi nipo mambele. Balaa lingine zilikuwa NEC siku hizi sizioni.
 
Oraimo za 5000 nikisikiliza mziki najihisi nipo mambele. Balaa lingine zilikuwa NEC siku hizi sizioni.
Aisee, kumbe nazo sio za mchezo
 
kwamba za 30k na 90k ni fekero[emoji1787][emoji1787]

hivi mnajua sisi wa zile za elfu 5 tunajiskiaje tukisoma vitu kama hivi!!!!

au mpaka aitwe mod ndio mjue kwamba kuna shambulio mmefanya[emoji24][emoji24][emoji24]
Mara ya mwisho nilinunua earphone kwa 45k na hazikudumu hapo ndo nkajua SAA ZA MSHALE NA EARPHONE hata ununue ya gaharama vipi unajisumbuaa hasa bongooo..wiziiii tuuuuu
 
Mara ya mwisho nilinunua earphone kwa 45k na hazikudumu hapo ndo nkajua SAA ZA MSHALE NA EARPHONE hata ununue ya gaharama vipi unajisumbuaa hasa bongooo..wiziiii tuuuuu
[emoji23][emoji23]
 
Milioni mbona cha mtoto!
O Bravo Ra series headphones (wired) zinagharimu hadi dola 12000
Kuna happy plugs earphone dola 14500

Maisha huko dunia ya kwanza , yanatia hasira na uchungu kwa sisi masikini, dola 12000 ni kariu miloni 30 za madafu , mtu anaweka masikioni!!
Zina nini humo ndani?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Daah kuna comments zimenichekesha sana maisha haya

Anyway sishangai wanaonunua earphones za milioni maana kila mtu ana kile kitu chake fulani ambacho roho inapenda

Kile ambacho yuko tayari kukitolea pesa yoyote ilio ndani ya uwezo wake haijalishi ni kubwa kiasi gani

Lakini pesa hiyo hiyo akiambiwa atoe kununua kitu asichokipenda lazima tu ataiona kubwa na hatokinunua
 
Ni kweli kabisa
 
Back
Top Bottom