Ni headphone/earphone za brand gani zina ubora wa juu?

Aiseeh kuna headphone nilipataga kipindi hicho zinaitwa "creative" back in 2012 nilibahatisha mliman city kwa 100k.huwa nazitafutaga mpaka kesho sijawahi ziona...Zina mziki mmoja umechujika balaa.
Nilipata websita yao ila nitakujaga kuziagiza
 
Sarahivi bei yake si itakuwa balaa
 
Mlimani City kuna Duka la Sony nitapitia nione km watakua nazo
 
Agiza mkuu , za pale naamini hutaziweza bei
Ile ni sony outlet , kama za ulaya tu, wanakuwa na latest products .ambazo zinakuwa gharama sana , wf xb 700, ni profuct ya 2019 kama sikosei , hutaikuta mlimani city, utazikuta wf 1000xm4, mambo ya laki saba plus
Mlimani City kuna Duka la Sony nitapitia nione km watakua nazo
 
Jana nimepokea oneodio pro 50, professional studio headphones, ni wired, nimechukua around 90,000tsh/=

Ngoma zinapiga balaa , hazichoshi maskio, very comfortable maskioni,

Kuna music player ya huawei naitumia, ina option ya 3d sound, utadhani studio imehamia kwenye maskio.


(Angalizo: matumizi ya muda mrefu ya headphones/earphones yanaweza hatarisha afya ya maskio,
usizidishe sauti zaidi ya asilimia 60 ya sauti ya kifaa chako )
 
Hivi studio headphones unaweza tu kutumia kwa matumizi ya kusikiliza muziki?uliagiza mtandaoni?
 
Duuuh Sawa Mkuu
 
Hivi studio headphones unaweza tu kutumia kwa matumizi ya kusikiliza muziki?uliagiza mtandaoni?
Yah, studio headphones unaweza pia kuskilizia muziki, tena unapata hires sound . Nyingi zina 40 to 50mm driver , so tegemea mziki uliochujika kama wa studio

Niliagiza AliExpress, mwezi uliopita mwishoni,

Kuna audio technica pia wapo vizuri Sana, Sema bei za headphones zake zimechangamka .
 
OK,asante japo umeongea kitaalamu sana,40-50 mm driver ina kazi gani?
 
Mimi natumia moxom

Brand: Moxom.

Model Number: MX-WL22.

Type: Over Ear.

Wireless Version: V5.0.

FREQ: 2.402-2.480GHz.

Speaker: 40mm * 1.

Sensitivity:105±3dB S.P.L at 1KHz.

Lithium Battery: 300 mAh.

Charging time: 2 hours

Playing time=24hrs

Usipo play kitu 33hrs

Bei nilichukua 45k k/koo
 
 
Vipi mziki wake ukoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…