Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kumsimamisha Edward Lowassa kama mgombea wa Urais CHADEMA 2015? Lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa?

Kikichosababisha Lowasa kuindolewa na hicho ripoti ni kuwa yeye ni Waziri mkuu ambae ni msimamizi wa shughuli za kila siku za serikali.
Waliohitajika kushtakiwa ni Waziri wa Nishati na madini, Katibu mkuu wizara ya nishati na madini, Mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na mwanasheria mkuu wa wizara ya Nishati na Madini...tofauti na hapo serikali yote kuanzia Rais wa nchi alitakiwa kuwajibishwa kwakushindwa kusimamia maslahi ya nchi.
Tofauti na hapo ni porojo tu za akina Sita na Mwakiembe.
 
Wananchi walio wengi (zaidi ya 90%) ni wajinga wanaofuata mkumbo bila Kututumia akili za kujali wanapata faida gani.
Wakati ule uelekeo wa mkumbo huo ulikuwa kwa Lowasa na kwa sababu hiyo upinzani ulipata kura na viti vingi zaidi
Kwa sababu hizo hizo za kufuata mkumbo, tuliona hata viongozi wakiwemo wabunge wakiunga juhudi.
Siasa zetu ni za kufuata mkumbo zaidi kwa sababu ya umasikini wa fikra.
Vyama vya siasa vinalijua hili na hulitumia vizuri na kwa ufanisi.
 
Kuna vitu vya ndani deep interior wengi hamvijui kuhusu Chadema na viongozi wake!. Soma hili bandiko uangalie ni la lini CHADEMA Kuna Kirusi! Je, Unajua kirusi hiki ni Nani?! Na The Motive Behind? unakijua kirusi hiki?.

Sii wengi wanawajua viongozi wa Chadema kwa karibu na misimamo yao kuhusu issues mbalimbali, mimi ni mmoja wa watu ambao nawajua viongozi wa Chadema kwa karibu na misimamo yao kwa kuzungumza nao face to face, hivyo niliongea na Dr. Slaa kuhusu yeye kugombea 2015, hivyo naujua msimamo wake na niliuweka humu Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?

Kwa msio jua Dr. Slaa hakujipanga kugombea 2015!.

P.
 
Mkuu rodrick alexander, kwanza asante sana kwa kuwa very objective, na kama wewe ni member, mshabiki, mfuasi au mpenzi wa Chadema, watu objective kama nyinyi ndio mnaweza kuisaidia Chadema ikae kwenye mstari!. Wengi wa members, wafuasi na washabiki ni ma nyumba!.

Naomba kukuuliza, jee unaijua katiba ya Chadema?, uliwahi kuisoma?, unazijua taratibu za kufukuza wanachama na mamlaka ya nidhamu kwa mujibu wa katiba ya Chadema?. Katika timua timua zote, ni lini Chadema waliwahi kuheshimu mawazo ya wanachama wao na kufuata taratibu za vikao vya mamlaka ya nidhamu kwenye timua timua zote?.
Mimi nilifuatilia timua timua hizi

Hakuna hata mara moja Chadema wamefuata katiba yao!.

Nashukuru baadhi ya watu ndio mnaanza kutambua kuwa Chadema sio chama cha kidemokrasia kama kinavyojiita ila ni kikundi cha watu wachache wenye malengo maalumu!.
Angalia tarehe ya bandiko hili Kufuatia Madudu na Maroroso ya CHADEMA, Je, bado kuna imani na matumaini na CHADEMA kwa 2015?

P.
 
Kuna point hapa
 
Vyama visivyoaandaa wagombea wao ni sumu ya ustawi wa demokrasia nchini, hivi ingekuwaje mfano leo CCM umuombe Lissu kuwa mhombea wake?
 
Umemjibu vizuri sana

Tatizo lake kubwa huyu ndugu Nehemia Kilave ni kuwa, ameandika kipropaganda bila kutumia akili akidhani anaandikia wasiotumia akili na kufikiri vyema kama yeye..
 
Kwani Slaa halikuwa hana ela ya kukaa hotelini? Maana kabla ya uchaguzi kufika Slaa alikuwa na mshahara wa zaidi ya milioni 7, pia alikuwa na marafiki kibao wa nje na ndani, kumbuka alipokuwa katibu wa chadema haliwahi kufanya ziara America mwezi mzima,pasipo kutumia ela ya chama,hivyo kusema Slaa hotel halilipiwa na Ccm kwa kuongwa ni ujinga mtupu Slaa maisha yake yote ya ubunge alikuwa hakiishi hotelini alikuwa hana nyumba,nyumba aliijenga juzijuzi tu ameisha acha ubunge hapo Mbweni Magengeni.
 
Siasa za hapa Tanzania zimeingiliwa na kizazi kinachoamini ktk uchawa na ushabiki husiokuwa na tija kwa nchi. Uchawa umekuwa mtaji ktk teuzi na baadhi wanalipwa ujira kidogo kuangaikia viongozi fulanifulani mitandaoni.

Kwenye siasa za ushindani, Lowassa alikuwa mtaji mkubwa kwa Chadema na ukawa mwaka 2015 kuliko Lipumba au Dr. Slaa. Tujifunze kwa wenzetu Kenya, hakuna uadui wa kudumu ktk siasa kama alivyofanya Slaa kuhamia kwa JPM na baada ya hapo akamwagwa.
 
Hakuna picha yeyote inayomwonyesha Slaa amevaa nguo ya ccm au kujiunga CCM kama hipo unaweza kuiweka hapa kama ushaidi,Slaa alionewa uruma na Magufuli baada ya vijana wa chadema kuanza kumzodoa na kumdhalilisha kwenye mitandao kuwa Mzee anabeba mabox kwenye Supermarket huko Canada, Magufuli alijua uhaminifu na uchapakazi wa Slaa,ndipo alipompa ubarozi kutoka kwenye kubeba mabox,hata wewe usingelikataa hiyo kazi, Maana akina Mbowe waliisha vuruga mipango yake yote.
 
Chadema walinunuliwa mkuu...hawakua na sababu yoyote zaidi nguvu ya hela kuhusika. Ile laana ya kupokea hela kuuza nafasi kwa mzee mamvi ndiyo mpaka kesho inawatafuna...credibility yao ilipotelea pale!
 
Umemjibu vizuri sana

Tatizo lake kubwa huyu ndugu Nehemia Kilave ni kuwa, ameandika kipropaganda bila kutumia akili akidhani anaandikia wasiotumia akili na kufikiri vyema kama yeye..
Mimi nadhani wewe ndio hutumii akili ,mimi binafsi nliyekuzidi akili naona mtoa mada yuko sahihi .
 
Ila nilipenda zile harakati za Lowasa za kuutafuta uraisi akiwa ndani ya CCM. Yaan vikao vya maangamizi Mara Sea Cliff, Mara nyumbani kwa Apson Mwan'gonda. Yaani full kumjambisha Born Town.
 
Chadema walinunuliwa mkuu...hawakua na sababu yoyote zaidi nguvu ya hela kuhusika. Ile laana ya kupokea hela kuuza nafasi kwa mzee mamvi ndiyo mpaka kesho inawatafuna...credibility yao ilipotelea pale!
So sad
 
Umejibu vizuri sana Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…