Kikichosababisha Lowasa kuindolewa na hicho ripoti ni kuwa yeye ni Waziri mkuu ambae ni msimamizi wa shughuli za kila siku za serikali.Thread 'Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo' Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo
Kasome hiyo report, then do the maths, utaona mkataba na hiyo kampuni uchwara ilikuwa na vimitego lukuki ukijumlisha utapata hiyo pesa hapo mpaka unajiuliza aliyeusaini aliwaza nini ndio maana Mwanasheria Mkuu wa Kipindi hicho Johnson Mwanyika nae alitakiwa ajiuzulu.
Hili la bandari ni muendelezo wa hawa kina Lowassa , Karamagi na Msabaha waliposhindwa kuwekwa nyuma ya nondo ndio maana hata walioshiriki mkataba mbovu wa bandari wala hawaogopi na hawatoogopa chochote sababu hakuna cha kuwafanya.
Waliohitajika kushtakiwa ni Waziri wa Nishati na madini, Katibu mkuu wizara ya nishati na madini, Mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na mwanasheria mkuu wa wizara ya Nishati na Madini...tofauti na hapo serikali yote kuanzia Rais wa nchi alitakiwa kuwajibishwa kwakushindwa kusimamia maslahi ya nchi.
Tofauti na hapo ni porojo tu za akina Sita na Mwakiembe.