Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kumsimamisha Edward Lowassa kama mgombea wa Urais CHADEMA 2015? Lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa?

Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kumsimamisha Edward Lowassa kama mgombea wa Urais CHADEMA 2015? Lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa?

Thread 'Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo' Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Kasome hiyo report, then do the maths, utaona mkataba na hiyo kampuni uchwara ilikuwa na vimitego lukuki ukijumlisha utapata hiyo pesa hapo mpaka unajiuliza aliyeusaini aliwaza nini ndio maana Mwanasheria Mkuu wa Kipindi hicho Johnson Mwanyika nae alitakiwa ajiuzulu.

Hili la bandari ni muendelezo wa hawa kina Lowassa , Karamagi na Msabaha waliposhindwa kuwekwa nyuma ya nondo ndio maana hata walioshiriki mkataba mbovu wa bandari wala hawaogopi na hawatoogopa chochote sababu hakuna cha kuwafanya.
Kikichosababisha Lowasa kuindolewa na hicho ripoti ni kuwa yeye ni Waziri mkuu ambae ni msimamizi wa shughuli za kila siku za serikali.
Waliohitajika kushtakiwa ni Waziri wa Nishati na madini, Katibu mkuu wizara ya nishati na madini, Mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na mwanasheria mkuu wa wizara ya Nishati na Madini...tofauti na hapo serikali yote kuanzia Rais wa nchi alitakiwa kuwajibishwa kwakushindwa kusimamia maslahi ya nchi.
Tofauti na hapo ni porojo tu za akina Sita na Mwakiembe.
 
Chama kikubwa kama CHADEMA hakiwezi kuchukua mtu aliyekataliwa na CCM waliomlea na kuwa mgombea wao wa kiti cha urais. Kibaya zaidi Viongozi zaidi ya watano wa kamati kuu ya CDM akiwemo M/kiti na katibu mkuu wakati huo walikuwa wamemtuhumu LOWASA kwa wizi na ufisadi waz wazi
Kipi kiliwafanya CDM wampitishe LOWASA KUWA mgombea wa kiti cha urais 2015?
Wananchi walio wengi (zaidi ya 90%) ni wajinga wanaofuata mkumbo bila Kututumia akili za kujali wanapata faida gani.
Wakati ule uelekeo wa mkumbo huo ulikuwa kwa Lowasa na kwa sababu hiyo upinzani ulipata kura na viti vingi zaidi
Kwa sababu hizo hizo za kufuata mkumbo, tuliona hata viongozi wakiwemo wabunge wakiunga juhudi.
Siasa zetu ni za kufuata mkumbo zaidi kwa sababu ya umasikini wa fikra.
Vyama vya siasa vinalijua hili na hulitumia vizuri na kwa ufanisi.
 
Slaa ndiye aliyekijenga Chadema kwa kiasi kikubwa, wangechukua idadi ya kula alizopata Dr. Slaa mwaka 2010 na idadi ya wapiga kura ni wazi angepata kura maradufu katika uchaguzi wa 2015.

badala yake wakaamua kumchafua Dr. Slaa kuwa amenunuliwa wakati ukweli viongozi wa Chadema ndio walinunuliwa na pesa za Lowassa.
Kuna vitu vya ndani deep interior wengi hamvijui kuhusu Chadema na viongozi wake!. Soma hili bandiko uangalie ni la lini CHADEMA Kuna Kirusi! Je, Unajua kirusi hiki ni Nani?! Na The Motive Behind? unakijua kirusi hiki?.

Sii wengi wanawajua viongozi wa Chadema kwa karibu na misimamo yao kuhusu issues mbalimbali, mimi ni mmoja wa watu ambao nawajua viongozi wa Chadema kwa karibu na misimamo yao kwa kuzungumza nao face to face, hivyo niliongea na Dr. Slaa kuhusu yeye kugombea 2015, hivyo naujua msimamo wake na niliuweka humu Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?

Kwa msio jua Dr. Slaa hakujipanga kugombea 2015!.

P.
 
Kama Chadema walikuwa wanaheshimu mawazo ya wanachama wao basi wangefata taratibu za vikao na kumteua mgombea urais badala ya watu wachache kukaa na kuja na jina lao hii ilionyesha wazi Chadema sio chama cha kidemokrasia kama kinavyojiita ila ni kikundi cha watu wachache wenye malengo maalumu.
Mkuu rodrick alexander, kwanza asante sana kwa kuwa very objective, na kama wewe ni member, mshabiki, mfuasi au mpenzi wa Chadema, watu objective kama nyinyi ndio mnaweza kuisaidia Chadema ikae kwenye mstari!. Wengi wa members, wafuasi na washabiki ni ma nyumba!.

Naomba kukuuliza, jee unaijua katiba ya Chadema?, uliwahi kuisoma?, unazijua taratibu za kufukuza wanachama na mamlaka ya nidhamu kwa mujibu wa katiba ya Chadema?. Katika timua timua zote, ni lini Chadema waliwahi kuheshimu mawazo ya wanachama wao na kufuata taratibu za vikao vya mamlaka ya nidhamu kwenye timua timua zote?.
Mimi nilifuatilia timua timua hizi

Hakuna hata mara moja Chadema wamefuata katiba yao!.

Nashukuru baadhi ya watu ndio mnaanza kutambua kuwa Chadema sio chama cha kidemokrasia kama kinavyojiita ila ni kikundi cha watu wachache wenye malengo maalumu!.
Angalia tarehe ya bandiko hili Kufuatia Madudu na Maroroso ya CHADEMA, Je, bado kuna imani na matumaini na CHADEMA kwa 2015?

P.
 
Slaa ndiye aliyekijenga Chadema kwa kiasi kikubwa, wangechukua idadi ya kula alizopata Dr. Slaa mwaka 2010 na idadi ya wapiga kura ni wazi angepata kura maradufu katika uchaguzi wa 2015. Lowassa kama alikuwa na nguvu kwanini hakuchagua vyama vingine kama Cuf au NCCR Mageuzi, ni wazi alitafuta chama chenye mtaji wa wapiga kura kazi iliyofanywa na Dr. Slaa.
Kama Chadema walikuwa wanaheshimu mawazo ya wanachama wao basi wangefata taratibu za vikao na kumteua mgombea urais badala ya watu wachache kukaa na kuja na jina lao hii ilionyesha wazi Chadema sio chama cha kidemokrasia kama kinavyojiita ila ni kikundi cha watu wachache wenye malengo maalumu.
Chadema hawakutaka kukubaliana na ukweli badala yake wakaamua kumchafua Dr. Slaa kuwa amenunuliwa wakati ukweli viongozi wa Chadema ndio walinunuliwa na pesa za Lowassa.
Kuna point hapa
 
Vyama visivyoaandaa wagombea wao ni sumu ya ustawi wa demokrasia nchini, hivi ingekuwaje mfano leo CCM umuombe Lissu kuwa mhombea wake?
 
Mimi si Chadema lakini nafikiri kosa lako kubwa hapa, Nehemia Kilave, ni utoto. Tatizo la nyie watoto wa jana ni kwamba hamuijui historia.

Kihistoria hakuna tofauti yoyote kati ya Slaa na Lowassa. Kwa namna ile ile Slaa alivyotoka CCM na kukimbilia Chadema na kukaribishwa ndivyo Lowassa alivyotoka CCM na kukimbilia Chadema.

Sababu kubwa ya wana siasa malaya kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa ni kwamba ni walafi wa madaraka...huku wataka na kule wataka!

Slaa aliisaliti chama chake cha kifisadi, CCM, baada ya jina lake kukatwa kugombea ubunge mwaka 1995. Chadema ilimpa hifadhi na hivyo akagombea ubunge kwa tiketi ya Chadema.

Lowassa aliisaliti chama chake cha kifisadi cha CCM na kutafuta hifadhi Chadema baada ya jina lake kukatwa alipotaka kugombea Urais mwaka 2000!

Hata marehemu mzee wa Kiraracha naye mwaka 1995 pamoja na kupiga vita mageuzi alidandia NCCR baada ya jina lake kukatwa kugombea Urais kupitia chama cha kifisadi cha CCM.

Kwa kifupi ni kwamba awali wote walikuwa mamluki wa Chama cha Kifisadi, CCM. Slaa alimtaka Lowassa kama mtaji wa kuukwaa Urais. Kwa bahati mbaya UKAWA wakamteua Lowassa kugombea, hivyo akazira!
Umemjibu vizuri sana

Tatizo lake kubwa huyu ndugu Nehemia Kilave ni kuwa, ameandika kipropaganda bila kutumia akili akidhani anaandikia wasiotumia akili na kufikiri vyema kama yeye..
 
Kwani TISS nani asiyewajua siku hizi makada wa CCM wanafanya hiyo kazi, sio lazima uletewe kitambulisho na vitu vingine.

Suala la kiasi alicholipiwa sio issue unless uniambie alienda hotelini kukaa bure, kwamba unaamini kwa akili zako kuna hoteli za bure hapa Tanzania!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kwani Slaa halikuwa hana ela ya kukaa hotelini? Maana kabla ya uchaguzi kufika Slaa alikuwa na mshahara wa zaidi ya milioni 7, pia alikuwa na marafiki kibao wa nje na ndani, kumbuka alipokuwa katibu wa chadema haliwahi kufanya ziara America mwezi mzima,pasipo kutumia ela ya chama,hivyo kusema Slaa hotel halilipiwa na Ccm kwa kuongwa ni ujinga mtupu Slaa maisha yake yote ya ubunge alikuwa hakiishi hotelini alikuwa hana nyumba,nyumba aliijenga juzijuzi tu ameisha acha ubunge hapo Mbweni Magengeni.
 
Je, ni kuongeza kura ,wabunge ili kupata Ruzuku kubwa? Au kulikuwa hakuna mgombea anaefaa Chamani .

Kama ni ruzuku, je kama hili lilikuwa linatosha kuhalalisha tuhuma zote za ufisadi zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA dhidi ya EL na kumfanya awe msafi?

Je, aliletwa kwa maslahi ya Wananchi au watu wachache kwa maslahi yao?

Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kusimamishwa EL? Je kama ni maslahi ya wachache kulikuwa na haja ya Viongozi wa CHADEMA walioshiriki kuachia ngazi?

Na ni lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa mpaka anaonekana msaliti?

Tuweke hisia za Uchama pembeni.

View attachment 2830164
Siasa za hapa Tanzania zimeingiliwa na kizazi kinachoamini ktk uchawa na ushabiki husiokuwa na tija kwa nchi. Uchawa umekuwa mtaji ktk teuzi na baadhi wanalipwa ujira kidogo kuangaikia viongozi fulanifulani mitandaoni.

Kwenye siasa za ushindani, Lowassa alikuwa mtaji mkubwa kwa Chadema na ukawa mwaka 2015 kuliko Lipumba au Dr. Slaa. Tujifunze kwa wenzetu Kenya, hakuna uadui wa kudumu ktk siasa kama alivyofanya Slaa kuhamia kwa JPM na baada ya hapo akamwagwa.
 
Siasa za hapa Tanzania zimeingiliwa na kizazi kinachoamini ktk uchawa na ushabiki husiokuwa na tija kwa nchi. Uchawa umekuwa mtaji ktk teuzi na baadhi wanalipwa ujira kidogo kuangaikia viongozi fulanifulani mitandaoni.

Kwenye siasa za ushindani, Lowassa alikuwa mtaji mkubwa kwa Chadema na ukawa mwaka 2015 kuliko Lipumba au Dr. Slaa. Tujifunze kwa wenzetu Kenya, hakuna uadui wa kudumu ktk siasa kama alivyofanya Slaa kuhamia kwa JPM na baada ya hapo akamwagwa.
Hakuna picha yeyote inayomwonyesha Slaa amevaa nguo ya ccm au kujiunga CCM kama hipo unaweza kuiweka hapa kama ushaidi,Slaa alionewa uruma na Magufuli baada ya vijana wa chadema kuanza kumzodoa na kumdhalilisha kwenye mitandao kuwa Mzee anabeba mabox kwenye Supermarket huko Canada, Magufuli alijua uhaminifu na uchapakazi wa Slaa,ndipo alipompa ubarozi kutoka kwenye kubeba mabox,hata wewe usingelikataa hiyo kazi, Maana akina Mbowe waliisha vuruga mipango yake yote.
 
Je, ni kuongeza kura ,wabunge ili kupata Ruzuku kubwa? Au kulikuwa hakuna mgombea anaefaa Chamani .

Kama ni ruzuku, je kama hili lilikuwa linatosha kuhalalisha tuhuma zote za ufisadi zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA dhidi ya EL na kumfanya awe msafi?

Je, aliletwa kwa maslahi ya Wananchi au watu wachache kwa maslahi yao?

Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kusimamishwa EL? Je kama ni maslahi ya wachache kulikuwa na haja ya Viongozi wa CHADEMA walioshiriki kuachia ngazi?

Na ni lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa mpaka anaonekana msaliti?

Tuweke hisia za Uchama pembeni.

View attachment 2830164
Chadema walinunuliwa mkuu...hawakua na sababu yoyote zaidi nguvu ya hela kuhusika. Ile laana ya kupokea hela kuuza nafasi kwa mzee mamvi ndiyo mpaka kesho inawatafuna...credibility yao ilipotelea pale!
 
Umemjibu vizuri sana

Tatizo lake kubwa huyu ndugu Nehemia Kilave ni kuwa, ameandika kipropaganda bila kutumia akili akidhani anaandikia wasiotumia akili na kufikiri vyema kama yeye..
Mimi nadhani wewe ndio hutumii akili ,mimi binafsi nliyekuzidi akili naona mtoa mada yuko sahihi .
 
Ila nilipenda zile harakati za Lowasa za kuutafuta uraisi akiwa ndani ya CCM. Yaan vikao vya maangamizi Mara Sea Cliff, Mara nyumbani kwa Apson Mwan'gonda. Yaani full kumjambisha Born Town.
 
Chadema walinunuliwa mkuu...hawakua na sababu yoyote zaidi nguvu ya hela kuhusika. Ile laana ya kupokea hela kuuza nafasi kwa mzee mamvi ndiyo mpaka kesho inawatafuna...credibility yao ilipotelea pale!
So sad
 
Wagombea walikuwepo ila uchaguzi unahitaji rasilimali na mtandao na Dr slaa asingeweza raise funds kiasi hiko as compared to lowassa.

Nadhani hapa ilifanyika tu risk assessment ikaonekana ni bora kutumia silaha zote kuing'oa CCM hata ikiwezekana shetani kutoka kuzimu. Yes ingekua na madhara baada ya kushindwa uchaguzi ila kama tungeshinda watu wangesahau yote.

Na defense ya Mbowe ni kwamba alikua fisadi sababu Ccm nzima ni mafisadi ila kwakuwa kahamia chama "kisafi" obviously hatoweza kuwa fisadi akiwa Rais maana atakua monitored.

Kwa maslahi ya wananchi maana chadema ingeleta mabadiliko kuliko CCM ambayo miaka 60 sasa haijaacha ufisadi.

Kama ingekua maslahi binafsi wangempitisha Dr slaa maana wangepata majimbo kadhaa na kuongeza ruzuku basi ila pale walipoamua kuweka rehani credibility ya chama ili waingie ikulu ilionyesha seriousness ya kulinda maslahi ya nchi kuliko ya chadema wenyewe.

Dr Slaa alikuwepo kwenye kamati ya kumleta Lowassa chadema cha ajabu alipopewa fomu ya kugombea akasusa!! Hivi really ulitegemea umchukue mtu kama majaliwa aje chadema eti asigombee Urais ila awe mpambe wa Lissu?? It's not realistic.....

Kingine alikosea kuita press na kuanza kuitukana chama. Waliokasirishwa na Lowassa kuja ni wengi akiwemo Lissu, Mnyika, kina safari n.k lakini walijitenga tu na chama ila hawakuwahi kitukana hadharani that was a traitor habit.

JPM was very strong maana alikubalika mpaka na sisi chadema. So Dr Slaa na JPM wana siasa zinafanana so kusingekua na haja ya kumchagua Dr slaa wakati "mpinga ufisadi" JPM naye alikua kwenye ballot.

So ilihitajika nguvu ya juu zaidi kuzima ule upepo wa JPM na kweli tokea Lowassa atangazwe kuhamia chadema siasa zote zikabadilika, JPM akapotezwa kwenye ramani ikawa Lowassa kuanzia media mpaka watoto wa chekechea.

Politics is an art but the few have really mastered, in fact the Lowassa factor was a lifeline to opposition to Mount a serious challenge to the ruling party. Unfortunately we might never witness such a candidate ever again.
Umejibu vizuri sana Mkuu.
 
Back
Top Bottom