Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kumsimamisha Edward Lowassa kama mgombea wa Urais CHADEMA 2015? Lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa?

Je, ni kuongeza kura ,wabunge ili kupata Ruzuku kubwa? Au kulikuwa hakuna mgombea anaefaa Chamani .
Wagombea walikuwepo ila uchaguzi unahitaji rasilimali na mtandao na Dr slaa asingeweza raise funds kiasi hiko as compared to lowassa.
Kama ni ruzuku, je kama hili lilikuwa linatosha kuhalalisha tuhuma zote za ufisadi zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA dhidi ya EL na kumfanya awe msafi
Nadhani hapa ilifanyika tu risk assessment ikaonekana ni bora kutumia silaha zote kuing'oa CCM hata ikiwezekana shetani kutoka kuzimu. Yes ingekua na madhara baada ya kushindwa uchaguzi ila kama tungeshinda watu wangesahau yote.

Na defense ya Mbowe ni kwamba alikua fisadi sababu Ccm nzima ni mafisadi ila kwakuwa kahamia chama "kisafi" obviously hatoweza kuwa fisadi akiwa Rais maana atakua monitored.
Je, aliletwa kwa maslahi ya Wananchi au watu wachache kwa maslahi yao
Kwa maslahi ya wananchi maana chadema ingeleta mabadiliko kuliko CCM ambayo miaka 60 sasa haijaacha ufisadi.

Kama ingekua maslahi binafsi wangempitisha Dr slaa maana wangepata majimbo kadhaa na kuongeza ruzuku basi ila pale walipoamua kuweka rehani credibility ya chama ili waingie ikulu ilionyesha seriousness ya kulinda maslahi ya nchi kuliko ya chadema wenyewe.
Na ni lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa mpaka anaonekana msaliti?
Dr Slaa alikuwepo kwenye kamati ya kumleta Lowassa chadema cha ajabu alipopewa fomu ya kugombea akasusa!! Hivi really ulitegemea umchukue mtu kama majaliwa aje chadema eti asigombee Urais ila awe mpambe wa Lissu?? It's not realistic.....

Kingine alikosea kuita press na kuanza kuitukana chama. Waliokasirishwa na Lowassa kuja ni wengi akiwemo Lissu, Mnyika, kina safari n.k lakini walijitenga tu na chama ila hawakuwahi kitukana hadharani that was a traitor habit.
Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kusimamishwa EL?
JPM was very strong maana alikubalika mpaka na sisi chadema. So Dr Slaa na JPM wana siasa zinafanana so kusingekua na haja ya kumchagua Dr slaa wakati "mpinga ufisadi" JPM naye alikua kwenye ballot.

So ilihitajika nguvu ya juu zaidi kuzima ule upepo wa JPM na kweli tokea Lowassa atangazwe kuhamia chadema siasa zote zikabadilika, JPM akapotezwa kwenye ramani ikawa Lowassa kuanzia media mpaka watoto wa chekechea.

Politics is an art but the few have really mastered, in fact the Lowassa factor was a lifeline to opposition to Mount a serious challenge to the ruling party. Unfortunately we might never witness such a candidate ever again.
 
Kwa Lowassa sikuwahi kumuunga mkono , Mbowe alichemka hapo huyu Lowassa kwangu ni fisadi mpaka kesho.

Nchi ilikuwa inalipa $137,000 kila siku kwa kampuni hewa huku document za kampuni hewa akizihodhi zionekane ni halisi.
 
Hao waliowahi kukwambia hayo walikuonesha ushahidi wa hiyo $137,000 per day?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hakika
 
Je, ni kuongeza kura ,wabunge ili kupata Ruzuku kubwa? Au kulikuwa hakuna mgombea anaefaa Chamani .

Kama ni ruzuku, je kama hili lilikuwa linatosha kuhalalisha tuhuma zote za ufisadi zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA dhidi ya EL na kumfanya awe msafi?

Je, aliletwa kwa maslahi ya Wananchi au watu wachache kwa maslahi yao?

Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kusimamishwa EL? Je kama ni maslahi ya wachache kulikuwa na haja ya Viongozi wa CHADEMA walioshiriki kuachia ngazi?

Na ni lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa mpaka anaonekana msaliti?

Tuweke hisia za Uchama pembeni.

View attachment 2830164
Umechokonoa mkuu. Uamuzi huu unaigharimu Chadema.
 
Report ya Mwakyembe ya mwaka 2008 kuhusu richmond yenye page 165 ile uliwahi kuisoma?

Kama bado jaribu kuitafuta.

Ajabu ni nchi haina utaratibu wa kupata hizi archives ndio maana hadi leo report ya kuungua soko la Kariakoo kwenye tume aliyounda Majaliwa haijawahi kuleta majibu na report haijulikani ilipo.
Hao waliowahi kukwambia hayo walikuonesha ushahidi wa hiyo $137,000 per day?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
- Part ya 1 ya mada yako, kosa la Dr. Slaa.

Kosa la Dr. Slaa alikuwa msaliti, alinunuliwa na CCM akaenda kufichwa hotelini, kisha akapewa ulinzi na TISS.

Alikuwa msaliti pia kwasababu, wakati wa kumpokea Lowassa alikuwepo, akajua yote yatakayotokea, lakini ghafla akabadilika na kuifuata njia ya CCM.

Nafahamu alinunuliwa na CCM ili apunguze nguvu ya Chadema kwa wakati ule, bahati nzuri licha ya kuhama kwake, bado Chadema ilishinda uchaguzi mkuu 2015 lakini wakaibiwa kura na wakina Nape na Makamba.

- Part 2 kumsimamisha Lowassa.

Alikuwa mgombea mwenye ushawishi kwa wakati ule, hili linathibitishwa na idadi ya kura za urais ilizopata Chadema zaidi ya milioni sita, licha ya kuibiwa kura nyingine na wakina Makamba.

Suala la ruzuku nalo ni sahihi, kwasababu chama kinapopata kura nyingi kwenye uchaguzi, matokeo yake huwa ni kupata ruzuku nyingi pia inayokiwezesha kuendesha chama.

Lowassa aliletwa kwa maslahi ya wananchi, na wananchi hao walikuja kuthibitisha kumuunga mkono kupitia idadi ya kura alizopata kama mgombea urais, alipata kura nyingi ambazo hazijawahi kupatikana kwa mgombea yeyote wa upinzani mpaka sasa.

Suala la kuhalalisha tuhuma za ufisadi zilizowahi kutolewa dhidi ya Lowassa, hapa ndipo kuna "collective responsibility", kwasababu rule inasema; he who alledges must prove.
Kwa kauli yako hapo juu. Wewe unaweza kuprove kuwa Dr. Slaa alinunuliwa na CCM?
Bahati mbaya wale waliomtuhumu hawakuwahi kuja na ushahidi, na bahati mbaya zaidi yule aliyemtuhumu kwa kulitaja jina lake kwenye list of shame pale Temeke, Mwembeyanga, akawa wa kwanza kukimbilia kwa wale waliomlea Lowassa.

Above all, usidanganyike na kile kinachoitwa "nguvu ya Dr. Slaa", huo ulikuwa ni msemo tu, kumbuka Dr. Slaa huyo mwenye nguvu aliwahi kushindwa uchaguzi dhidi ya Kikwete aliyeonekana dhaifu 2010, sasa utamuitaje mwenye nguvu mtu wa aina hiyo?!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hao waliowahi kukwambia hayo walikuonesha ushahidi wa hiyo $137,000 per day?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Thread 'Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo' Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Kasome hiyo report, then do the maths, utaona mkataba na hiyo kampuni uchwara ilikuwa na vimitego lukuki ukijumlisha utapata hiyo pesa hapo mpaka unajiuliza aliyeusaini aliwaza nini ndio maana Mwanasheria Mkuu wa Kipindi hicho Johnson Mwanyika nae alitakiwa ajiuzulu.

Hili la bandari ni muendelezo wa hawa kina Lowassa , Karamagi na Msabaha waliposhindwa kuwekwa nyuma ya nondo ndio maana hata walioshiriki mkataba mbovu wa bandari wala hawaogopi na hawatoogopa chochote sababu hakuna cha kuwafanya.
 
EL ni mtaji, Dr ni hakuna kitu pale!.
Karibu Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM!
Dr. Slaa hakuwa na uwezo wa kupata hata nusu ya kura za Eddo!. Elections 2015 - Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa... mtaji huu ndio Chadema wameutumia. Na kilichowakosesha Chadema ikulu ile 2015 ni kufanya makosa ya kijinga tuu Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...

P
Kwa taarifa yako Lowassa kura alizikuta cdm, hakuna kura hata moja alikwenda nayo. Alaaniwe Mbowe na genge lake kwa kumpokea yule mzee tapeli la siasa. Lowasa angeenda TLP na kupata kura zile hapo ungekuwa sawa. Kama alileta kura zile akiwa na miezi miwili, je alileta viti vingapi vya ubunge akiwa na miaka miwili?
 
Report ya Mwakyembe ya mwaka 2008 kuhusu richmond yenye page 165 ile uliwahi kuisoma?

Kama bado jaribu kuitafuta.

Ajabu ni nchi haina utaratibu wa kupata hizi archives ndio maana hadi leo report ya kuungua soko la Kariakoo kwenye tume aliyounda Majaliwa haijawahi kuleta majibu na report haijulikani ilipo.
Kwani wewe uliwahi kuisomea wapi hiyo ripoti ili nami nikaifuate huko?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kwa kauli yako hapo juu. Wewe unaweza kuprove kuwa Dr. Slaa alinunuliwa na CCM?
Ndio maana wakampa ulinzi wa TISS, kwasababu walijua ana manufaa kwao, na gharama za hotelini kwa siku zote alizokaa huko alilipiwa na CCM.

Hili likafanyika hata kwa Lipumba, yeye akaamua kwenda kula bata Rwanda kwa pesa aliyohongwa na CCM ya Jakaya.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Thread 'Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo' Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Kasome hiyo report, then do the maths, utaona mkataba na hiyo kampuni uchwara ilikuwa na vimitego lukuki ukijumlisha utapata hiyo pesa hapo mpaka unajiuliza aliyeusaini aliwaza nini ndio maana Mwanasheria Mkuu wa Kipindi hicho Johnson Mwanyika nae alitakiwa ajiuzulu.

Hili la bandari ni muendelezo wa hawa kina Lowassa , Karamagi na Msabaha waliposhindwa kuwekwa nyuma ya nondo ndio maana hata walioshiriki mkataba mbovu wa bandari wala hawaogopi na hawatoogopa chochote sababu hakuna cha kuwafanya.
Hii ripoti ya Mwakyembe nakumbuka kuna vitu alivificha, akadai akivisema vyote nchi ingeyumba, sasa mtu wa aina ile aliyeonekana kutokuwa muwazi kwenye ripoti yake kwanini nimuamini?

Hivyo, hata hayo aliyoandika hapo kwenye ripoti yake siwezi kuyaamini kwa asilimia zote, mpaka nione na utetezi wa Lowassa ndio nipime uzito wa pande zote mbili.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kwa taarifa yako Lowassa kura alizikuta cdm, hakuna kura hata moja alikwenda nayo. Alaaniwe Mbowe na genge lake kwa kumpokea yule mzee tapeli la siasa. Lowasa angeenda TLP na kupata kura zile hapo ungekuwa sawa. Kama alileta kura zile akiwa na miezi miwili, je alileta viti vingapi vya ubunge akiwa na miaka miwili?
Lowassa alizikuta kura gani Chadema? Kwanini Dr. Slaa asingezitumia hizo kura kumuondoa yule Kikwete dhaifu 2010?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hii ripoti ya Mwakyembe nakumbuka kuna vitu alivificha, akadai akivisema vyote nchi ingeyumba, sasa mtu wa aina ile aliyeonekana kutokuwa muwazi kwenye ripoti yake kwanini nimuamini?

Hivyo, hata hayo aliyoandika hapo kwenye ripoti yake siwezi kuyaamini kwa asilimia zote, mpaka nione na utetezi wa Lowassa ndio nipime uzito wa pande zote mbili.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
It is very simple kama ulimsoma katikati ya mistari.

Yaloyofichwa ni kuhusu pacha mmoja wa Boys 2 Men (mzee tabasamu) na mshirika wao mkuu RA.

Kwahiyo hayo waliyoficha yalitakiwa yamuondoe boss kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na mshirika wa automatically bunge lingekuwa dissolved na nchi kurudi kwenye uchaguzi.

Kwangu haiondoi uhalali wa EL kuwa fisadi na hao washirika wake ni kwamba yeye tu ndio alitolewa kama sadaka na mwenzie miaka 3 mbele alijiengua mwenyewe.
 
Ndio maana wakampa ulinzi wa TISS,
Pamoja na Kuhamia CHADEMA Lowasa Bado aliendelea kuwa na ulinzi wa TISS
kwasababu walijua ana manufaa kwao, na gharama za hotelini kwa siku zote alizokaa huko alilipiwa na CCM.
Thibitisha kuwa gharama za hoteli alilipiwa na ccm
Hili likafanyika hata kwa Lipumba, yeye akaamua kwenda kula bata Rwanda kwa pesa aliyohongwa na CCM ya Jakaya.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
It is very simple kama ulimsoma katikati ya mistari.

Yaloyofichwa ni kuhusu pacha mmoja wa Boys 2 Men (mzee tabasamu) na mshirika wao mkuu RA.

Kwahiyo hayo waliyoficha yalitakiwa yamuondoe boss kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na mshirika wa automatically bunge lingekuwa dissolved na nchi kurudi kwenye uchaguzi.

Kwangu haiondoi uhalali wa EL kuwa fisadi na hao washirika wake ni kwamba yeye tu ndio alitolewa kama sadaka na mwenzie miaka 3 mbele alijiengua mwenyewe.
Ok fine, hapa naona umewaunganisha hao wawili ili ku-justify kile kilichoandikwa kwenye ripoti kuwa ni ukweli, so unataka tuamini hiyo ripoti ndio kama "hukumu ya mahakama ya rufaa"... tuishie hapo.

Hebu tena nikumbushe jambo moja, ni wakati gani Dr. Mwakyembe aliwekewa sumu akanyonyoka nywele, ilikuwa ni kabla, au baada ya hiyo ripoti kusomwa?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Je, ni kuongeza kura ,wabunge ili kupata Ruzuku kubwa? Au kulikuwa hakuna mgombea anaefaa Chamani .

Kama ni ruzuku, je kama hili lilikuwa linatosha kuhalalisha tuhuma zote za ufisadi zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA dhidi ya EL na kumfanya awe msafi?

Je, aliletwa kwa maslahi ya Wananchi au watu wachache kwa maslahi yao?

Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kusimamishwa EL? Je kama ni maslahi ya wachache kulikuwa na haja ya Viongozi wa CHADEMA walioshiriki kuachia ngazi?

Na ni lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa mpaka anaonekana msaliti?

Tuweke hisia za Uchama pembeni.

View attachment 2830164
Usitake kufukunyua haisaidii kitu tunapiganane na Katiba mpya.
 
Back
Top Bottom