Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kumsimamisha Edward Lowassa kama mgombea wa Urais CHADEMA 2015? Lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa?

Taja kiasi alicholipiwa Dr. Slaa Hotelini na list ya jina la mlipaji. Tutajie pia majina ya walizi wa TISS NA namba za vitambulisho vyao. Huo ndo aina ya ushaidi unaotakiwa

Ndugu yangu jielimishe kujua aina mbalimbali za ushaidi unavyotakiwa uwe itakusaidia kujenga hoja
Kwani TISS nani asiyewajua siku hizi makada wa CCM wanafanya hiyo kazi, sio lazima uletewe kitambulisho na vitu vingine.

Suala la kiasi alicholipiwa sio issue unless uniambie alienda hotelini kukaa bure, kwamba unaamini kwa akili zako kuna hoteli za bure hapa Tanzania!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Ushahidi gani sasa unaoutaka?

Ile sadaka aliyoitoa kule Lagos unadhani ilikuwa sadaka kama ya matonya?

EL alimhonga nabii ili tangazo la nabii litangazwe madhabahuni ili liwalainishe walokole lia lia na ndivyo ilivyofanyika.

Slaa akifanywa tu kuwa mbuzi wa kafara.
😂😂😂😂
 
EL ni mtaji, Dr ni hakuna kitu pale!.
Karibu Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM!
Dr. Slaa hakuwa na uwezo wa kupata hata nusu ya kura za Eddo!. Elections 2015 - Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa... mtaji huu ndio Chadema wameutumia. Na kilichowakosesha Chadema ikulu ile 2015 ni kufanya makosa ya kijinga tuu Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...

P
Maswali ya msingi hukujibu.
Je, ilikiwa kwa maslahi ya wananchi au ya wachache?
Je, hilo lilitosha kumsafisha na kumwondolea tuhuma walizozunguka wakimtuhumu kwa zaidi ya miaka mitano?
Je, kama mtu waliyemtuhumu kwa miaka 5 wakisema apigwe mawe, wakisema ni fisadi ila ndani ya siku moja wakamsafisha na kumpa kijiti cha kugombea urais, kwanini waaminike kwa tuhuma nyingine watakazozisema au chochote watakachosema maana inawezekana ikawa yale yale kama ya lowassa siku moja wanaweza kusema mwenye ushahidi aupeleke mahakamani.
 
Anakwepa maswali muhimu
 
Lowassa alizikuta kura gani Chadema? Kwanini Dr. Slaa asingezitumia hizo kura kumuondoa yule Kikwete dhaifu 2010?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
2010 ilikuwa ni turning point ya cdm kwenda kuchukua nchi 2015. Kuanzia 2010-2015 cdm ndio chama Cha siasa kilichofanya kazi ya siasa kuliko chama kingine chochote. Wakati huo cdm wakifanya kazi ya siasa, Lowassa alikuwa ccm akigawa fedha makanisani. Tukajiandikisha kwa hamasa kubwa kupiga kura tukiamini ccm watampitisha Lowassa, huku tukiita kitambulisho Cha kura kichinjio, kwa kumaanisha ni Cha kumchinjia mbali Lowassa.

Kwa mshangao wa wengi, uongozi wa cdm chini ya genge la Mbowe kwa maslahi Yao binafsi wakamuuzia Lowassa nafasi ya ugombea urais! Kosa lile la karne limeharibu haiba ya cdm hadi Leo kuwa ni chama Cha waropokaji, na wachafua heshima ya watu kwa tuhuma za uongo. Alaaniwe Mbowe na genge lake kwa kumpa mtu mchafu nafasi adhimu ya kugombea urais kwa maslahi Yao. Lowassa alifanikiwa kuwahadaa viongozi wa cdm kuwa angekwenda na wabunge zaidi ya 50 na madiwani lukuki, kitu ambacho kulikuwa uongozi mkubwa.

Hakuna uongozi makini unaweza kuukota mgonjwa, mchafu asiye na maadili muda mfupi wa kampeni na kumpa nafasi muhimu kama ya ugombea urais. Ukiona hivyo ujue hicho chama hakina uongozi wa maana, bali genge la wapigaji. Kwa hapa Slaa alikuwa sahihi kuzira, japo naye ni boya tu kwa kwenda kujiunga na dhalimu.
 
Daaa so sad
 
- Part ya 1 ya mada yako, kosa la Dr. Slaa.

Kosa la Dr. Slaa alikuwa msaliti, alinunuliwa na CCM akaenda kufichwa hotelini, kisha akapewa ulinzi na TISS.

Alikuwa msaliti pia kwasababu, wakati wa kumpokea Lowassa alikuwepo, akajua yote yatakayotokea, lakini ghafla akabadilika na kuifuata njia ya CCM.

Nafahamu alinunuliwa na CCM ili apunguze nguvu ya Chadema kwa wakati ule, bahati nzuri licha ya kuhama kwake, bado Chadema ilishinda uchaguzi mkuu 2015 lakini wakaibiwa kura na wakina Nape na Makamba.

- Part 2 kumsimamisha Lowassa.

Alikuwa mgombea mwenye ushawishi kwa wakati ule, hili linathibitishwa na idadi ya kura za urais ilizopata Chadema zaidi ya milioni sita, licha ya kuibiwa kura nyingine na wakina Makamba.

Suala la ruzuku nalo ni sahihi, kwasababu chama kinapopata kura nyingi kwenye uchaguzi, matokeo yake huwa ni kupata ruzuku nyingi pia inayokiwezesha kuendesha chama.

Lowassa aliletwa kwa maslahi ya wananchi, na wananchi hao walikuja kuthibitisha kumuunga mkono kupitia idadi ya kura alizopata kama mgombea urais, alipata kura nyingi ambazo hazijawahi kupatikana kwa mgombea yeyote wa upinzani mpaka sasa.

Suala la kuhalalisha tuhuma za ufisadi zilizowahi kutolewa dhidi ya Lowassa, hapa ndipo kuna "collective responsibility", kwasababu rule inasema; he who alledges must prove.

Bahati mbaya wale waliomtuhumu hawakuwahi kuja na ushahidi, na bahati mbaya zaidi yule aliyemtuhumu kwa kulitaja jina lake kwenye list of shame pale Temeke, Mwembeyanga, akawa wa kwanza kukimbilia kwa wale waliomlea Lowassa.

Above all, usidanganyike na kile kinachoitwa "nguvu ya Dr. Slaa", huo ulikuwa ni msemo tu, kumbuka Dr. Slaa huyo mwenye nguvu aliwahi kushindwa uchaguzi dhidi ya Kikwete aliyeonekana dhaifu 2010, sasa utamuitaje mwenye nguvu mtu wa aina hiyo?!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ni kweli ni tuhuma kama Makonda na Lengai Ole walivyosingiziwa bila ushahidi
 
Mengi ya maelezo yako kumhusu Lowassa upo sahihi, kuanzia kwenda makanisani kuomba kura, mpaka kutuahidi kutuletea wabunge 50 wa CCM, hapo tuko pamoja.

Suala la ugonjwa wa Lowassa hili hebu tuliache tu, lisiingie kwenye mjadala kwani ugonjwa ni mapenzi ya Mungu, hakuna aijuaye kesho yetu.

Suala la ufisadi wa Lowassa; hapa naamini tukianza kufukua makaburi hayupo mtu kwenye KK ya Chadema atakayebaki salama, wengi walimuita hivyo bila ushahidi.

Hoja yangu inaanzia hapa, uliposema kuanzia 2010 - 2015 ndio ilikuwa turning point ya Chadema kuchukua nchi, ukiamini kwamba hapo ndipo walifanya siasa za nguvu.

Sasa hizo siasa za nguvu kwanini zikashindwa kumuondoa yule Kikwete dhaifu kwenye uchaguzi wa 2010? kwasababu walianza harakati zao Jan. uchaguzi ukafanyika Oct. 2010, miezi kumi hiyo!.

Naona unataka kutuaminisha hapa kwamba nguvu ya Chadema kwenye siasa za Tanzania ilianza kuonekana 2010 kuja mbele, kwani nyuma haikuwepo?

Nakumbuka Lowassa alikuja na yale "mafuriko", hapa kwa mtazamo wako najua unaamini ile ilikuwa nguvu ya Chadema kujitangaza kabla ya uchaguzi.

Sasa kama unaamini hivyo, kwanini basi wale watu waliojitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya Lowassa wakafanya vile kama walikuwa hawampendi Lowassa kama mgombea urais? au huiamini nguvu ya mgombea Urais kwenye kampeni?

Kama unaiamini, huoni Lowassa nae kama mgombea alikuwa na ushawishi wake tena mkubwa tu kwenye zile kampeni?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Lowassa alikuwa na nguvu na ushawishi mkubwa hasa kanda ya ziwa kipindi hicho na kama asingefanyiwa fitna na JK Lowassa ndie angelikuwa Raisi wa Tanzania. Kauli ya kumwambia JK kuwa hana maamuzi magumu ilimgharimu na kumleta JPM
 
- Part ya 1 ya mada yako, kosa la Dr. Slaa.

Kosa la Dr. Slaa alikuwa msaliti, alinunuliwa na CCM akaenda kufichwa hotelini, kisha akapewa ulinzi na TISS.

Alikuwa msaliti pia kwasababu, wakati wa kumpokea Lowassa alikuwepo, akajua yote yatakayotokea, lakini ghafla akabadilika na kuifuata njia ya CCM.

Nafahamu alinunuliwa na CCM ili apunguze nguvu ya Chadema kwa wakati ule, bahati nzuri licha ya kuhama kwake, bado Chadema ilishinda uchaguzi mkuu 2015 lakini wakaibiwa kura na wakina Nape na Makamba.

- Part 2 kumsimamisha Lowassa.

Alikuwa mgombea mwenye ushawishi kwa wakati ule, hili linathibitishwa na idadi ya kura za urais ilizopata Chadema zaidi ya milioni sita, licha ya kuibiwa kura nyingine na wakina Makamba.

Suala la ruzuku nalo ni sahihi, kwasababu chama kinapopata kura nyingi kwenye uchaguzi, matokeo yake huwa ni kupata ruzuku nyingi pia inayokiwezesha kuendesha chama.

Lowassa aliletwa kwa maslahi ya wananchi, na wananchi hao walikuja kuthibitisha kumuunga mkono kupitia idadi ya kura alizopata kama mgombea urais, alipata kura nyingi ambazo hazijawahi kupatikana kwa mgombea yeyote wa upinzani mpaka sasa.

Suala la kuhalalisha tuhuma za ufisadi zilizowahi kutolewa dhidi ya Lowassa, hapa ndipo kuna "collective responsibility", kwasababu rule inasema; he who alledges must prove.

Bahati mbaya wale waliomtuhumu hawakuwahi kuja na ushahidi, na bahati mbaya zaidi yule aliyemtuhumu kwa kulitaja jina lake kwenye list of shame pale Temeke, Mwembeyanga, akawa wa kwanza kukimbilia kwa wale waliomlea Lowassa.

Above all, usidanganyike na kile kinachoitwa "nguvu ya Dr. Slaa", huo ulikuwa ni msemo tu, kumbuka Dr. Slaa huyo mwenye nguvu aliwahi kushindwa uchaguzi dhidi ya Kikwete aliyeonekana dhaifu 2010, sasa utamuitaje mwenye nguvu mtu wa aina hiyo?!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kwani kipindi hicho si ndio kipindi ambacho vyama vilishirikiana na kuamua kumpigia kura za urais mtu mmoja ambaye ni Lowassa?
 
Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kumsimamisha Edward Lowassa kama mgombea wa Urais CHADEMA 2015? Lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa?
Mimi si Chadema lakini nafikiri kosa lako kubwa hapa, Nehemia Kilave, ni utoto. Tatizo la nyie watoto wa jana ni kwamba hamuijui historia.

Kihistoria hakuna tofauti yoyote kati ya Slaa na Lowassa. Kwa namna ile ile Slaa alivyotoka CCM na kukimbilia Chadema na kukaribishwa ndivyo Lowassa alivyotoka CCM na kukimbilia Chadema.

Sababu kubwa ya wana siasa malaya kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa ni kwamba ni walafi wa madaraka...huku wataka na kule wataka!
Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kusimamishwa EL? Je kama ni maslahi ya wachache kulikuwa na haja ya Viongozi wa CHADEMA walioshiriki kuachia ngazi/
Slaa aliisaliti chama chake cha kifisadi, CCM, baada ya jina lake kukatwa kugombea ubunge mwaka 1995. Chadema ilimpa hifadhi na hivyo akagombea ubunge kwa tiketi ya Chadema.

Lowassa aliisaliti chama chake cha kifisadi cha CCM na kutafuta hifadhi Chadema baada ya jina lake kukatwa alipotaka kugombea Urais mwaka 2000!

Hata marehemu mzee wa Kiraracha naye mwaka 1995 pamoja na kupiga vita mageuzi alidandia NCCR baada ya jina lake kukatwa kugombea Urais kupitia chama cha kifisadi cha CCM.

Kwa kifupi ni kwamba awali wote walikuwa mamluki wa Chama cha Kifisadi, CCM. Slaa alimtaka Lowassa kama mtaji wa kuukwaa Urais. Kwa bahati mbaya UKAWA wakamteua Lowassa kugombea, hivyo akazira!
 
Tunajifunza kutokana na makosa.
Chama makini kinaangalia makosa ya nyuma ili kujiimarisha.
Hii ndiyo mijadala inayopaswa kujadailiwa ili kujisahihisha katika kujiimarisha.
Mkuu tuanzie hapa kwa kujiuliza role ya Dr. Slaa kwenye umoja wa ukawa ilikuwa ipi?

Dr. Slaa ali husika vipi kama kama kiongozi mwandamizi wa ukawa kumshawishi Lowasa ahamie ukawa?
 
Mimi si Chadema lakini nafikiri kosa lako kubwa hapa, Nehemia Kilave, ni utoto. Tatizo la nyie watoto wa jana ni kwamba hamuijui historia.

Kihistoria hakuna tofauti yoyote kati ya Slaa na Lowassa. Kwa namna ile ile Slaa alivyotoka CCM na kukimbilia Chadema na kukaribishwa ndivyo Lowassa alivyotoka CCM na kukimbilia Chadema.

Sababu kubwa ya wana siasa malaya kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa ni kwamba ni walafi wa madaraka...huku wataka na kule wataka!

Slaa aliisaliti chama chake cha kifisadi, CCM, baada ya jina lake kukatwa kugombea ubunge mwaka 1995. Chadema ilimpa hifadhi na hivyo akagombea ubunge kwa tiketi ya Chadema.

Lowassa aliisaliti chama chake cha kifisadi cha CCM na kutafuta hifadhi Chadema baada ya jina lake kukatwa alipotaka kugombea Urais mwaka 2000!

Hata marehemu mzee wa Kiraracha naye mwaka 1995 pamoja na kupiga vita mageuzi alidandia NCCR baada ya jina lake kukatwa kugombea Urais kupitia chama cha kifisadi cha CCM.

Kwa kifupi ni kwamba awali wote walikuwa mamluki wa Chama cha Kifisadi, CCM. Slaa alimtaka Lowassa kama mtaji wa kuukwaa Urais. Kwa bahati mbaya UKAWA wakamteua Lowassa kugombea, hivyo akazira!
Umeeleza vizuri tatizo hujawa clear sababu ya CHADEMA kumsimamisha EL
 
Slaa ndiye aliyekijenga Chadema kwa kiasi kikubwa, wangechukua idadi ya kula alizopata Dr. Slaa mwaka 2010 na idadi ya wapiga kura ni wazi angepata kura maradufu katika uchaguzi wa 2015. Lowassa kama alikuwa na nguvu kwanini hakuchagua vyama vingine kama Cuf au NCCR Mageuzi, ni wazi alitafuta chama chenye mtaji wa wapiga kura kazi iliyofanywa na Dr. Slaa.
Kama Chadema walikuwa wanaheshimu mawazo ya wanachama wao basi wangefata taratibu za vikao na kumteua mgombea urais badala ya watu wachache kukaa na kuja na jina lao hii ilionyesha wazi Chadema sio chama cha kidemokrasia kama kinavyojiita ila ni kikundi cha watu wachache wenye malengo maalumu.
Chadema hawakutaka kukubaliana na ukweli badala yake wakaamua kumchafua Dr. Slaa kuwa amenunuliwa wakati ukweli viongozi wa Chadema ndio walinunuliwa na pesa za Lowassa.
 
EL ni mtaji, Dr ni hakuna kitu pale!.
Karibu Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM!
Dr. Slaa hakuwa na uwezo wa kupata hata nusu ya kura za Eddo!. Elections 2015 - Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa... mtaji huu ndio Chadema wameutumia. Na kilichowakosesha Chadema ikulu ile 2015 ni kufanya makosa ya kijinga tuu Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...

P
Jibu maswali kiongozi
 
Back
Top Bottom