Ni ipi hasa sababu ya Freeman Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa kipindi kirefu hivi?

Ni ipi hasa sababu ya Freeman Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa kipindi kirefu hivi?

CCM fomu moja ya Urais,
CHADEMA fomu moja ya mwenyekiti.
 
Kwan wewe inakuhusu nn. Anyway ngoja wawaletee mwamba lissu msaidiz lema, katibu heche maji mtaita bhaji.
 
Hiyo nchi ya kupewa chadema ni nchi gani kweli?
Hawa mkiwapa nchi wanabadili katiba ya nchi mara moja ili rais toka kwao awe madarakani kama mwenyekiti wao.
Uenyekiti wa chama wameugeuza kuwa ufalme!
Kama watatupatia umeme wa uhakika wapewe nchi, maana Hawa waliopo ni outdated, wamebaki kucheza na maneno tu na wizi wa kura.
 
Je CHADEMA watu wenye hakuna uwezo wa kuwa wenyeviti? Mbona kina Mtei na Bob Makani walimuamini inamaana baada ya yeye hakuna mwingine mwenye uwezo?

Ni kipi kinafanyika kwenye chama chetu CHADEMA kinachoonesha uwepo wa Demokrasia ? Ni miaka zaidi ya 20 mwenyekiti yule yule.

Binafsi kama mwanachama huwa najiuza hili swali nikiuliza najibiwa akiondoka chama kinakufa, je kweli?

Je, hakuna namna ikawekwa misingi Imara kama ilivyo kwa Republican na Democratic US?

Au kuna elements za dictatorship kama

Kuamini hakuna mtu mwenye uwezo zaidi yako

Tamaa ya kuendelea kuwepo madarakani?

Kuna muda naona kama anafanya vitu ambavyo vinaipa faida sana CCM kuliko CDM naona akipumzika akawa Mlezi wa chama kinaweza songa mbele zaidi .
Kama wewe ni mwanachama wakati ukifika chukua form ugombee kama kura zikitosha utakuwa mwenyekiti.
 
Kama watatupatia umeme wa uhakika wapewe nchi, maana Hawa waliopo ni outdated, wamebaki kucheza na maneno tu na wizi wa kura.
Wameshindwa kununua hata kiwanja cha kujenga ofisi ya makao makuu, huo umeme watauiba toka wapi?
 
Wameshindwa kununua hata kiwanja cha kujenga ofisi ya makao makuu, huo umeme watauiba toka wapi?
Kama ukinunua kiwanja Cha kujenga ofisi ya makao makuu ndio unaweza kuleta umeme, ccm kimewashinda Nini?
 
Kama ukinunua kiwanja Cha kujenga ofisi ya makao makuu ndio unaweza kuleta umeme, ccm kimewashinda Nini?
Bwawa la yule jamaa litaanza kutema mzigo wakati chadema bado hawana hata kiwanja. We subiri uone!
Mwenyekiti amekigeuza chama kuwa shamba la bibi.
 
Bwawa la yule jamaa litaanza kutema mzigo wakati chadema bado hawana hata kiwanja. We subiri uone!
Mwenyekiti amekigeuza chama kuwa shamba la bibi.
Hata bomba la gas mlilosema likifika hapa Dar mgao utakuwa ni historia, bomba liko hapa Dar na porojo ni zile zile. Kipi kinakufanya ujiamini kuhusu hilo bwawa kufanya unachotamani? Isitoshe hilo bwawa sio la ccm, japo unafanya Miradi ya umma ndio kipimo Cha ccm dhidi ya cdm.

Kwa taarifa yako kwa miaka ya zamani ofisi zilikuwa zina maana sana, lakini kwa sasa Kuna mitandao, unaweza kupata taarifa zote online kiasi kwamba haiwi lazima sana kwenda ofisini. Kwahiyo ofisi kuwepo ni kwa ajili ya mazoea tu, lakini mbadala wake upo. Una lingine kwa msaada zaidi? Ccm ina ofisi nchi nzima, lakini hizo ofisi zimekuwa vijiwe vya majobless, kufanyia majungu, fitina, ushirikina, wizi na uchafu wa aina hiyo. So ofisi sio za sifa kwa hivyo, hasa ukizingatia 80% ya ofisi za ccm ni za urithi. Pale mwenye nyumba ya urithi anapomtambia asiye na nyumba!
 
Back
Top Bottom