Hizi ni mila na desturi za wazungu. Waafrika hususani watanzania, hatujawahi kuwa na siku kama hizi. Siku hizi kuna ulimbukeni wa aina fulani na ukienda sehemu za uswazi unaweza kutapika kwa kichefuchefu. Mashanginfi ya huko siku hizi huyaambii kitu kwenye sherehe za birthday, au wenyewe wakiita besidei. Wanwake wa huko wako radhi kubana fedha za matumizi au kutembea na wanaume nje ya ndoa ili mradi tu wapate fedha za kununua keki ya kupiga picha kuweka kwenye mitandao. Wki moja kabla utakuta wanaanza ku post ''besidei roading'' (birth day loading), yaani kichefuchefu tupu.