Ni ipi nafasi ya Tanzania katika Migogoro unaoendelea Mashariki ya Kati?

Ni ipi nafasi ya Tanzania katika Migogoro unaoendelea Mashariki ya Kati?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,678
Reaction score
5,166
Inajulikana kuwa nchi za Mashariki ya Kati zimejengewa misingi ya Ustaarabu wa kidini tangu enzi na tunapozungumzia dini tunajumuisha Ustawi na utulivu wa Mwanadamu.

Migogoro ya kihistoria hususani inahusisha ardhi ya israel-Palestina imeendelea kuwa nadharia kuu ya Kutoweka kwa Amani katika Mashariki ya Kati.

Lakini,nchi nyingi zimekuwa ni zenye kupata athari ya kiuchumi na kisiasa kutokana na mgogoro unaoendelea,kwa namba fulani tunaweza kusema Kuna Vita ya Biashara lakini Kuna Vita ya Itikadi ya Kisiasa vs Vita ya Teknolojia.

Bara la Ulaya limeendelea kukemea pasi kuchukua hatua stahiki katika usitishwaji wa Vita,huku bara la Asia likikemea Majibu/hatua zinazochukuliwa na Irani dhidi ya Majirani lakini Bara la Afrika limekiwa likikemea bila ya kuchukua hatua.

Tanzania kama nchi ya kimkakati katika ustawi wa Bara la Afrika kwa ujumla,imeendelea kuchukua hatua stahiki katika kuhakikisha uchumi wake hauathiriki kwa munasaba wa vita na imeendelea kushikiria msimamo wake uhusiano wa kidiplomasia pamoja na kutofungamana na upande wowote

Tumeona mwanzoni mwa mwaka tumesign mikataba na nchi ya Israel kwa ajili ya ushirikiano wa Kijeshi lakini juzi tumesign mikataba na urusi katika kuhakikisha ushirikiano wa Kiuchumi.

Hii ina maana gani?Je Tanzania anaweza kuwa Mpatanishi wa Migogoro yote inayotokea kwa sasa?Je ni ipi nafasi yetu katika kukuzaa uchumi na Amani ya Dunia?
 
Nafasi yake ni hii ya kupata upenyo wa kutupandishia bei ya mafuta karibia mara mbili ya bei ya mwanzo ili mafisadi waliojazana ndani ya serikali na chama yaweze kupata faida mara dufu kwa kuwanyonya watumiaji.

Nje ya hapo haina nafasi yoyote ile kwenye huo mgogoro.
 
Nafasi yake ni hii ya kupata upenyo wa kutupandishia bei ya mafuta karibia mara mbili ya bei ya mwanzo ili mafisadi waliojazana ndani ya serikali na chama yaweze kupata faida mara dufu kwa kuwanyonya watumiaji.

Nje ya hapo haina nafasi yoyote ile kwenye huo mgogoro.
Ukizingatia walisema tuna akiba ya mafuta ya miezi mitatu halafu siku moja baadae wakapadisha bei ya mafuta yale yale ya AKIBA ya miezi mitatu yaani wanatuchukulia powa sana hawa MAFISIEMU
 
Kama haina ubalozi wa israel mjini dodoma au dar basi haina nafasi. Lakini kuna balozi za palestina na iran zipo hata saudia upo ubalozi wao ongeza na yemen. Kutegemea ubalozi wa israel ulioko nairobi kenya kunaonesha nafasi ya tanzania kwenye migogoro ya mashariki ya kati haipo
 
Back
Top Bottom