Pole ndugu. Kwakweli mtoto mtundu nadhani ni changamoto inayotukuta wengi ila wakati mwingine inakuwa ni kipindi tu kifupi cha mpito, sijui wanasaikolojia wanakiitaje. Kinachotakiwa ni kuwa makini naye na kuweka control measures ili asipitilize. Mimi nina mtoto sasa hivi ana miaka 10 yuko grade 5, kuna kipindi nililazimika kumtengea chumba chake na kuondoa kila kitu kisha nikawa namfungia humo wakati wa week end asipoenda shule maana alikuwa anawasumbua sana wadogo zake kwa michezo ya ajabu na hatarishi hadi nikahisi kama ana majini maana alikuwa hasikii kabisa. Baadae nikaja kugundua tabia mbovu anajifunza kutoka shule zetu hizi binafsi za english media. Wengi wao hawafuatilii makuzi/maadili ya watoto, wao kazi ni kuwakaririsha masomo basi. Nilimwamisha nikampeleka shule moja hivi ya kikatoliki, kila akikosea wakawa wanamchapa hadi anatusimulia nyumbani - uwezi amini mwaka mmoja tangu ahamie shule hii mpya alibadilika kabisa, akawa anawapenda na hana ugomvi wala vituko na wadogo zake tena. Alikuwa anapata maksi ndogo darasani, sasa hivi wala anaonyesha hali ya ushindani kwa wenzake na anafaulu vizuri masomo yote hadi amenishawishi nikarudisha mapenzi kwake maana nilishaanza kumchukia na kutaka kumpeleka kijijini akalelewe na bibi yake hadi ukazuka ugomvi na mama yake akipinga uamuzi wa kumpeleka mtoto kwa bibi yake!.