Ni ipi siri ya kuweza kubalance klachi kubadili gia kwenye gari za manual

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Ni kwa miaka zaidi ya 15 gari pekee nazoendesha ni automatic

Gari za manual nazipenda ila napata shida kubalance klachi na moto wakati wa kubadili gia.

nikiachia klachi nikianza kukanyaga moto wakati nabadili gia, gari inaruka ruka.

Tupeane ujuzi na tips
 
Sasa unataka vitu vya kujifunza kwa vitendo ujifunze kwa maandishi?
Haya kanyaga clutch mpaka mwisho, weka gia namba 1, anza kuachia clutch polepole na mafuta kidogo sana ukiona kama gari inakinzana kati ya breki na mwendo toa parking break gari itaanza kuserereka polepole achia clutch yote endelea kulivurumisha mpaka Gaza
 
Nilikua naogopa manual kwa vile ipo home basi ndo gari yangu pendwa kwa sasa

Kubalance klachi ni jambo la kawaida tu hakuna ugumu wowote

Ukibadili gia kwenye manual hubalance klachi ila unakanyaga klachi mpka mwisho ndo unabadili gia ila kubalance klachi una kua unakanyaga klachi na Accelerator kwa pamoja kma unaibia hivi zinakua hazifiki mwisho kabisaa na hii inatokea pale ambapo kma unataka kuingia mainroad unasubiria gari nyengine zipite ili gari isizime

Nb: Gari ya manual inamuweka dereva Active muda wote wa safari kutokana na pirika zake za kubadilisha gia
 
🀣🀣🀣🀣
 
Siri kubwa ni kuachia clutch taratibu wakati wa kuondoka. Hapo ukiwa gear 1 au 2. Gari ikishaanza kuondoka kwemye kuweka gear zinazofuata unaachia tu clutch pale ambapo gear ishaingia.
Ukizoea utaona kawaida tu, enzi zangu gari ndogo hasa hizi Toyota saloon au pick up nilikuwa naweza kuondoka hadi na gear namba 3.
 
Clutch ina principles zake.. ukanyagaji hakikisha pedal inafika mwisho..

Uondokaj ktk sehem flat ni kawaida.. kimbembe ktk milima au miinuko alaf nyuma kuna gari mbele gari ndio utajua Maharage ni mboga au futari.

Ukikanyaga mafuta mengi ukarusha mguu ktk clutch unaparamia gari la mbele.. ukikanyaga Clutch bila brake chuma inarudi nyuma.. 😁 mboga moto ugali moto.
 
Hapo mlimani ukute na hand brake haifanyi kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…