Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii nilifundishwa namna ya kubalance katika uondokaji wake.Clutch ina principles zake.. ukanyagaji hakikisha pedal inafika mwisho..
Uondokaj ktk sehem flat ni kawaida.. kimbembe ktk milima au miinuko alaf nyuma kuna gari mbele gari ndio utajua Maharage ni mboga au futari.
Ukikanyaga mafuta mengi ukarusha mguu ktk clutch unaparamia gari la mbele.. ukikanyaga Clutch bila brake chuma inarudi nyuma.. 😁 mboga moto ugali moto.
Mkuu, hii clutch less gear engagemet si dhambi, ni common sana huko america na jamaica, na truck huwa xina last almost forever.Mkuu umezunguka wee ila bado umerudi palepale!!
Hiyo modification iliyofanyika kwenye gearbox ya manual ndiyo imeifanya iwe termed as semi-automatic na siyo manual tena.
Ndio maana hata utumiaji wake umebadilika, clutch unakanyaga mda wa kuondoka na mda wa kusimama tu.
Kwa maneno hayo bado nasisitiza huu mfano sio sahihi kwenye huu mjadala maana hapa inazungumziwa manual transmission na sio semi-automatic!!!
Vilevile kwenye manual gearbox bado nakukatalia kuengage gear bila kukanyaga clutch pedal. Kwanza usipotumia clutch, utatumia nguvu zaidi maana unailazimisha. Lakini pia lazima gear zilie.
Kitendo cha kuliza gear tu ni ishara ya udereva wa hovyo unaohatarisha usalama wa gearbox.
Mkuu hii 12 speed naendeaha bila clutch ikiwa loaded with 32 tones na hutasikia gear kulia, changes down za kupanda na kushuka milima ya ruvuma, truck ni ya mwaka 2000, ilikuja bongo mwaka 2017 na hadi leo ipo kwenye original gearbox.Hii gearbox yenye gia 12, ukiamua kuendesha kwa kufuata mtiririko bado huna namna ya kukwepa clutch!! Bila clutch, splitter ni functionless..
Hata ukisema uskip matumizi ya splitter ili uzunguke 3 low na 3 high bado utaishia kuliza gear tu..
Scania huwa haidanganyi mkuu, utaforce kufloat lakini ile 'kweeeeee ' sound itakuumbua tu..
Kabisa mkuu, mie clutch ni ya kuondokea tu.Dereva mzuri hahitaji kutumia clutch unapoendesha gari manual, clutch inatumika wakati wa kuondoka tu baada ya gari kusimama au wakati wa kusimama ila ikiwa kwenye motion unacheza tu na RPM unapanga gia bila clutch
Hii ndio nasikia Leo mkuu.
Mfano kuna Cruiser flan hiv hardtop.. ktk dashboard hakuna RPM je ktk situation kama hiyo unajuaje kwamba hapa gari ipo ktk RPM kadhaa hivyo nitumie clutchless gear engagement?... au utaskiliza kwa mvumo wa engine..? Ikumbukwe kuna gari zipo silent hazivumi sana mpk high RPMS kwenye 6k
Hapo issue ni mguu wako tu kwenye mafuta, unakadiria. Na perfect timing ya kutupia gear kavu kavu ni wakat RPM inarudi chini.Nina gari ni Sport bila clutch huweki gia.. itakupigia kelele. (Siwek gia bila clutch, hii inatokea ikiwa sijakanyaga mpk mwisho)
Na RPM kutoka 1k kwend 9k ni milliseconds tu.. hasa ktk 1st gear, kwa gari kama hii unaanzaje kuweka gia bila clutch?
Kuna video jamaa anaipiga hiyo Fiat mkasi juu, mkasi chini bila kutumia clutch.Kama clutch tu inakushinda vipi ukikutana na Gari aina ya Fiat mkasi juu mkasi chini Dereva Unaendesha Gari kama unagombana nalo
Udereva wa zaman ulikuwa mgumu sana
Kwa dereva mzoefu sio big issue sanaHapo mlimani ukute na hand brake haifanyi kazi.
Njia pekee ya kuwa dereva pro kwenye gari za Manual ni kuendesha mara kwa mara mpaka upate uzoefuUnaskia harufu ya clutch tu unajua hapa kimeumana 😁.. huku na huku na gari lenyewe linazima.. MANUAL hazina uvumilivu kwa Malena.
Feeling ya kuendesha gari za manual sio ya kawaida. Madereva tunakuelewa sanaMadereva wa gari za manual mtakubali kwamba manual ni gari tamu sana...tena sana. Kuna muda nikiendesha auto sijisikii vizuri naona sifurahii kuendesha gari.
Moja ya vitu vitamu ni kuamua moto wa kutoka nao hasa unapoingia barabara kubwa.
unakuwa humalizi kuachia clutch yote pale unaporudi kwenye mafuta baada ya kumaliza kuweka gia.Ni kwa miaka zaidi ya 15 gari pekee nazoendesha ni automatic
Gari za manual nazipenda ila napata shida kubalance klachi na moto wakati wa kubadili gia.
nikiachia klachi nikianza kukanyaga moto wakati nabadili gia, gari inaruka ruka.
Tupeane ujuzi na tips