Ni ipi siri ya mafanikio ya kudumu kwenye ndoa za Wazee wetu?

Ni ipi siri ya mafanikio ya kudumu kwenye ndoa za Wazee wetu?

kilamba lamba

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2020
Posts
427
Reaction score
738
Habarini wana MMU,

Natumai ni wazima wa afya kabisa na wenye shida kidogo mungu awabariki warudi kwenye hali yao ya kawaida ya kiafya.

Hili jambo limekuwa likinitatiza sana. Na leo nimeamua niwashirikishe ndugu zangu labda tutapata wasaa zaidi wa kulifafanua hili jambo.

JE NI IPI SIRI YA MAFANIKIO YA KUDUMU KWA NDOA ZA WAZEE WETU?
Ipo hivi, mimi ni miongoni mwa watu wa mwisho kabisa kuamin kwamba mambo yanayotokea kipindi hchi kwenye ndoa yalikuwa hayatokei kwa wazee wetu huko nyuma.

Kama Uzinzi, uongo, kufumuniana, kudharauliana, kugombana hivyo vitu vyote vilitokea kwa wazee wetu. Sasa wao waliwezaje kufanikiwa kudumu kwenye ndoa zao tofauti na zama hizi.

Siri kubwa ni ipi.?
Kama ni Uvumilivu ndo tuseme zama hizi uvumilivu baina ya wanandoa hakuna kabisa. Kama ni upendo ndo tueseme umepotea kabisa zama hizi.

Tulijadili hili wana MMU
Ni ipi Siri ya kudumu kwa ndoa za wazee wetu kuliko zama hizi.?
 
BINAFSI NAZIONA SABABU ZIFUATAZO

[emoji117]Kushindwa kutimiza majukumu kwa kila mwanandoa
[emoji117]Wanaume kuoa kutokana na msukumu wa nje
[emoji117]Wanawake kupenda harusi na sio ndoa
[emoji117]Baadhi ya mwanandoa kuamini kuwa ndoa ikivunjika watapata mwingine ambaye hana mapungufu kabisa au bora kuliko aliye nayel

Ni hayo tu
[emoji146][emoji1241][emoji111]
 
Wanawake wa Enzi hzo walikuwa ni kondoo na walijitambua hvyo , na mwanaume alichukua mamlaka kamili , sa hv wadada waliopita na chuo hawa full reasoning , wewe mwanaume usipocheza Kwa hekima dk mbili nyingi mshaachana ...
Nimekuelewa sana mfano

Mfano siku hizi mwanamke ni mtoa taarifa hawaombi ruhusa tena
 
Mbona zama ni tofauti sema kuna kitu hakipo sawa haswa maadili ...yaani enzi hizo ukisikia mke wa mtu hata kumpa mkono unaona kesi ila sasa mke wa mtu anakumbatiwa hata kutongozwa bila ya wasiwasi..

Wanawake walikuwa na maadili mema kuanzia muonekano kama kuvaa mpaka lugha safi mbele ya wanaume ila sasa ni kisanga yaani unakuta denti kaolewa ila vinguo mpaka mapaja yapo nje kama bado yupo sokoni vile🤔
 
Maadili Maadili Maadili

mmomonyoko wa maadili unateketeza ndoa, wanaume kua na michepuko kibao, wanawake chupi mkononi
.. siku hizi kuoa demu limetembezewa dudu 30 na zingine mitungo kitu cha kawaida gaddemit! Unaacha kitambaa unaoa chujio 😂😂 atleast wazee wetu walipata wanawake wana maadili. Jitu lina mikucha mireeefu hata kujichamba sijui inakuaje apo achilia mbali kusonga ugali.

Upande wa wanaume yan mwanamke anatoka kwenda kutafuta iwe viwandani,mama ntilie,kazi yoyote wee unakuna mbupu tu kijiweni wengine wanazalisha hovyo na kukimbia majukumu hopeless kabisa wanawake wamekua wasaka tonge kwa kias kikubwa kuliko sisi acha watupande vichwani!
 
Back
Top Bottom