binafsi naweza kusema kwa kiasi kikubwa utandawazi umebadili mtindo wetu wa maisha ambao ulikuwepo hapo awali. ndoa za kipindi hiki cha utandawazi zimekua na changamoto nyingi ukilinganisha na zamani kulingana na uwepo wa mambo kadhaa.
mitandao ya kijamii. kwamfano shemeji yako kaweka status whatsapp kuhusu hisia zake either akiwa mwenye huzuni, au furaha au akiwa kwenye tukio fulani ni rahisi kuanzisha mazungumzo juu ya status yake na kuongeza ukaribu mpaka kujikuta katika hali ya kutamaniana. zamani kumuona tu mtu au kufahamu hisia zake ilikua ngumu sababu hatukua na hizi simu za kisasa tulizonazo sasahivi.
Tamaa.hasa kwa wakinadada unakuta hali ya maisha nyumbani kwake ni ya kipato cha kawaida au cha chini ila akiwatizama marafiki zake wanamiliki vitu vya gharama hivyo inapelekea kujiona mpweke na kutamani vitu visivyoendana na kipato chake hivyo inakua rahisi kushawishika na watu wenye kipato cha juu na kuamua kuisaliti ndoa yake.
changamoto za kiafya. hapa ipo mifano hai kabisa. mpo kwenye ndoa wote mkiwa na afya nzuri ila ikatokea mmoja wapo akatetereka kiafya mwenza anakosa uvumilivu na kuamua kumsaliti mwenzake.
malezi. aina ya malezi pia kwa namna fulani inachangia ndoa nyingi kutodumu ukilinganisha na miaka ya nyuma. kwa hivi karibuni tumekua na changamoto za kima adili pamoja na malezi. watu hawazingatii tena miiko na maadili pindi unapokua kwenye ndoa ndo kama tulivyosikia baadhi ya semina za wanawake kwamba sio lazima kumuaga mume pindi unapotaka kutoka.
usawa wa kininsia. ukweli hili suala la usawa wa kinjinsia limekua ni changamoto kubwa sana katika ndoa zetu. unakuta mwanamke hatimizi mambo ya kifamilia kwasababu ya ubize wa kazi za kazini. hali ya kujiona mko sawa wote na kupelekea ubishani na hata kuwa tayari kutengana pindi mnaposhindwa kuelewana.
miaka ya nyuma sana aina fulani ya mtindo wa maisha ulisaidia sana kudumisha ndoa pamoja na maadili kwa wanandoa pamoja na jamii kwa ujumla. ila hatuwezi kupingana na utandawazi ila tusiache asili na tamaduni zetu kwani zilituongoza katika njia sahihi na bora.
Sent from my TECNO KB7j using
JamiiForums mobile app