Ni ipi siri ya mafanikio ya kudumu kwenye ndoa za Wazee wetu?

Ni ipi siri ya mafanikio ya kudumu kwenye ndoa za Wazee wetu?

Tulipo waruhusu kuvaa suruale tu kila kitu kiliishia hapo.
 
Siri ilikuwa ni kumcontrol mwanamke na kumbania fursa za kiuchumi, kupitia hili wanawake walichukulia ndoa Kama ajira, mwanamke hakuruhusiwa kurithi ardhi (chanzo kikuu cha uzalishaji) angetumia ardhi ya mumewe kuzalisha/kumzalishia mume.
Kama ujuavyo bosi hanuniwi, bosi ananyenyekewa.....mke ukizingatia Hana PA kwenda, ndoa zilidumu bila hata upendo, Ile sogeza siku.

Siku hizi wanawake Wana Uhuru wa kiuchumi, Wana uwezo wa kujihudumia bila kutegemea mume.....wanachohitaji Kwa mume ni upendo Tu...bahati mbaya wanaume wengi bado Wana Ile mentality ya kale ya 'boss husband'.....wakitegemea ule uvumilivu wa wanawake WA zamani upo.

Mambo yamebadilika siku hizi, ukitaka mwanamke akunyenyekee we mpende, muogeshe upendo....uwezo wa kumcontrol Kama kale huna.....hawadhibitiki.
 
Habarini wana MMU,

Natumai ni wazima wa afya kabisa na wenye shida kidogo mungu awabariki warudi kwenye hali yao ya kawaida ya kiafya.

Hili jambo limekuwa likinitatiza sana. Na leo nimeamua niwashirikishe ndugu zangu labda tutapata wasaa zaidi wa kulifafanua hili jambo.

JE NI IPI SIRI YA MAFANIKIO YA KUDUMU KWA NDOA ZA WAZEE WETU?
Ipo hivi, mimi ni miongoni mwa watu wa mwisho kabisa kuamin kwamba mambo yanayotokea kipindi hchi kwenye ndoa yalikuwa hayatokei kwa wazee wetu huko nyuma.

Kama Uzinzi, uongo, kufumuniana, kudharauliana, kugombana hivyo vitu vyote vilitokea kwa wazee wetu. Sasa wao waliwezaje kufanikiwa kudumu kwenye ndoa zao tofauti na zama hizi.

Siri kubwa ni ipi.?
Kama ni Uvumilivu ndo tuseme zama hizi uvumilivu baina ya wanandoa hakuna kabisa. Kama ni upendo ndo tueseme umepotea kabisa zama hizi.

Tulijadili hili wana MMU
Ni ipi Siri ya kudumu kwa ndoa za wazee wetu kuliko zama hizi.?
Ni kama tu, zamani hata ukiwa na elimu ya darasa la saba unapata ajira nzuri.
lakini sasa zama zimebadilika, inabidi uwe na uwezo zaidi.
Na ndo hivyo kwenye mahusiano, zamani huhitaji uwezo mwingi lakini sasa uwe na uwezo na akili ya kuchagua mwanamke wa kuishi naye na akili ya kuishi naye.
 
Back
Top Bottom