Ni ipi siri ya mafanikio ya kudumu kwenye ndoa za Wazee wetu?

Tulipo waruhusu kuvaa suruale tu kila kitu kiliishia hapo.
 
Siri ilikuwa ni kumcontrol mwanamke na kumbania fursa za kiuchumi, kupitia hili wanawake walichukulia ndoa Kama ajira, mwanamke hakuruhusiwa kurithi ardhi (chanzo kikuu cha uzalishaji) angetumia ardhi ya mumewe kuzalisha/kumzalishia mume.
Kama ujuavyo bosi hanuniwi, bosi ananyenyekewa.....mke ukizingatia Hana PA kwenda, ndoa zilidumu bila hata upendo, Ile sogeza siku.

Siku hizi wanawake Wana Uhuru wa kiuchumi, Wana uwezo wa kujihudumia bila kutegemea mume.....wanachohitaji Kwa mume ni upendo Tu...bahati mbaya wanaume wengi bado Wana Ile mentality ya kale ya 'boss husband'.....wakitegemea ule uvumilivu wa wanawake WA zamani upo.

Mambo yamebadilika siku hizi, ukitaka mwanamke akunyenyekee we mpende, muogeshe upendo....uwezo wa kumcontrol Kama kale huna.....hawadhibitiki.
 
Ni kama tu, zamani hata ukiwa na elimu ya darasa la saba unapata ajira nzuri.
lakini sasa zama zimebadilika, inabidi uwe na uwezo zaidi.
Na ndo hivyo kwenye mahusiano, zamani huhitaji uwezo mwingi lakini sasa uwe na uwezo na akili ya kuchagua mwanamke wa kuishi naye na akili ya kuishi naye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…