Nyumba hizi ni moja ama zinahesabika kijiji kizima, kwengine ni nyumba za nyasi ama mabati kuukuu
maji ya kisimani
umeme hadi jenereta / sola
hospitali hadi mjini
maduka hadi mjini
barabara za vumbi
shule nzuri hadi mjini
Network inasumbua
ndio shida ya kujenga hivyo vijiji
Sorry bila Shaka huzungumzii Vijiji nilivyopost hapa....
Hebu tuongelee wilaya ya Muleba...( Moja ya wilaya za wahaya maana wengi mmekalili Bukoba Tu)..
Wilaya ina jumla ya hospital tano...Tatu za binafsi na mbili za serikali...
Wilaya ya Muleba ni wilaya ya pili kwa shule nyingi Tz hii...ni kawaida kijiji kuwa na shule Tatu sehemu moja...
Wilaya ya Muleba kama ilivyo Bukoba ni wilaya inayoongoza kupata mvua nyingi Tz hii...inazalisha sana ndizi, maharagwe, kahawa, chai na siku hiz vanilla...
Maji inatumia ya bomba kutoka Victoria kupitia mradi wa maji kemondo...
Barabara za lami zipo Hadi vijijini mfano Muhutwe to kamachumu, Muleba to Rubya, Muleba to nshamba... Barabara zote hizo zina lami
Bila kusahau Barabara kuu ya Muleba to Bukoba...
Wilaya ina visiwa na bandari kubwa ya magarini japo inahudumiwa na bandari ya kemondo...
Kutoka Muleba kwenda Bukoba panafikika maana kuna daladala kibao Hadi saa Tatu usiku...
Wilaya hii ukubwa wake ni Sawa na mkoa mzima wa Kilimanjaro...