Nilifika pale mlimani nikakuta Harrier tako la nyani nyeusi ya mwaka 2005 nikaipenda, wakaniwashia chuma kucheki odometer nikaona inasoma imetembea kilometa 25000. Yani gari ina miaka 17 halafu iwe imetembea km 25k, kweli? Daaah halafu bei imechangamka kweli kweli wanataka mil35!
Madalali wawili wamevaa kaunda suti wanaongea saaana mda wote wanaipamba tu gari, mara engine haijaguswa, sijui haijarudiwa rangi, kule japan owner alikua ni mdada, alikua anaifuga tu nyumbani akiwa na mishe mishe hua anapanda matreni yao ya umeme! Duh nikaona hawa jamaa wanataka kuniingiza mkenge nikabwaga sikuinunua...
Wakaniambia siwezi pata gari makini kama ile popote pale duniani [emoji23]