Ni jambo gani ambalo kama ungelijua mapema maisha yako yangebadilika

Ni jambo gani ambalo kama ungelijua mapema maisha yako yangebadilika

Naona kila kitu kama kimepangwa ,nilipo sasa hata sielewi nimefikaje na miaka inaenda tu ..Kikubwa kutokujilaumu na kusimama mwenyewe...Miaka 6 nyuma nilikuwa mzee wa kuzunguka Dar bila ya kusettle.

Kama ningejua ningenunua viwanja vyangu huku kange uzunguni -Tanga.
 
Kwenda chuo cha driving na kupata leseni nikiwa na miaka 20 na kitu matokeo yake nimefika mpaka 30 na Sasa ndio nimegundua kama ningefanya hivyo ningekuwa mbali sana muda huu,badala yake mda huo nikawa nasoma kozi ambazon Sina future nazo mpaka sasa
 
Pesa sio bodhaa halisi, ni kitu Cha kufikirika.
 
NINGEACHA DHAMBI MAPEMA (Ningeokoka mapema),Ningemtumikia Mungu wakati wa ujana wangu...
Huwa nikiona vijana wadogo wanamtumikia Mungu kwa kuimba kwaya,kupiga vyombo vya mziki kanisani,viongozi wa jumuiya,wazee wa kanisa,wanashiriki kazi mbalimbali za kanisa,uinjililist pamoja na elimu yao ya kubwa na kazi zao nzuri,bado wanamtumikia Mungu kwa bidii wakiwa vijana wabichi na wenye nguvu..
HUWA NAJUTIA UJANA WANGU sikumtumikia Mungu kama wao,ila WATOTO wangu ninawafundisha kumjua Mungu mapema..wasiwe kama mimi ujana wangu niliuchezea kwa anasa sizizokuwa na faida yotote usela nondo ujanja pori ambao hauna faida.
 
1995 kama ningejua hayati MREMA na NCCR MAGEUZI ni CCM B na alikuwa shushushu TISS nisingepoteza muda wangu na nguvu zangu na pesa zangu ,katika kazi za chama cha NCCR MAGEUZI.(nisingepoteza muda na siasa za NCCR MAGEUZI)

kama vijana wa leo walivyopoteza vingi mpaka UHAI ,WAMEUWAWA NA WATU WASIOJULIKANA,NA KUTEKWA kwa siasa ya chadema ya mbowe huku wakidhani ni MWAMBA WAO.
 
NINGEACHA DHAMBI MAPEMA (Ningeokoka mapema),Ningemtumikia Mungu wakati wa ujana wangu...
Huwa nikiona vijana wadogo wanamtumikia Mungu kwa kuimba kwaya,kupiga vyombo vya mziki kanisani,viongozi wa jumuiya,wazee wa kanisa,wanashiriki kazi mbalimbali za kanisa,uinjililist pamoja na elimu yao ya kubwa na kazi zao nzuri,bado wanamtumikia Mungu kwa bidii wakiwa vijana wabichi na wenye nguvu..
HUWA NAJUTIA UJANA WANGU sikumtumikia Mungu kama wao,ila WATOTO wangu ninawafundisha kumjua Mungu mapema..wasiwe kama mimi ujana wangu niliuchezea kwa anasa sizizokuwa na faida yotote usela nondo ujanja pori ambao hauna faida.
Amina. Hatujachelewa, Mungu ni mwema wakati wote
 
Back
Top Bottom