Ni jambo la kufurahisha Diamond Platnumz kuingizwa kwenye mtaala wa elimu ya Tanzania. Bado kupewa PhD ya heshima sasa

Ni jambo la kufurahisha Diamond Platnumz kuingizwa kwenye mtaala wa elimu ya Tanzania. Bado kupewa PhD ya heshima sasa

Ni jambo zuri ila tujiulize hivi vitu:
1. Unamfundishaje mtoto mambo ya maadili (moral) kwa kutumia mifano ya watu ambao mitaa na wazazi wa wanafunzi hawa wanajua kabsa kuwa ni mifano ya ovyo. Nasibu ni know womaniser wala sio suala la kificho, hata watoto wanajua kuwa amezaa na Zari, pamoja na Mobetto.

2. Kwanini tunakubali kubadilisha sehemu chache tena ambazo hazina faida, unamuweka Diamondd ili iweje, je tumeshinda kuweka kina Mbaraka Mwishehe, au kina Marijani? Tunamuweka kweli MwanaFA!? Kwanini asiwe Professor J?!
Tanganyika bhana 😃
 
Yaani kila anaekua maarufu apewe honorary phd?
Ndio maana wasomi nchi hii wanakata tamaa, uzalendo wanaweka pembeni.

Japokuwa ilibaki level moja nipate phd , naelewa msoto wake. Ni kuwatukana wasomi wanaoingia darasani

Elimu inachezewa sana tz, too much politics
Phd ya kutunukiwa kamwe haiwezi kuwa sawa na ya darasani japo linapokuja suala la mtu anayetunukiwa anaweza kuwa kafanya mambo yenye heshima kuliko mwenye phd ya darasani au kainunua tu au kapewa kisiasa.
 
Kama kweli wamezingua mtu ameenda kucheck Muvi Kwa Didy Leo anakuwa kioo Cha Jamii. Mashoga na Walawiti watakuwa wamejaa uko wizarani au hawana Habari na mambo ya ulimwengu wa Leo.

Hiyo mwingine juzi tu hapa anatunza mashoga kwenye party .

Sina shida na huyo Mh. Waziri

Bora hata wangeweka Mrisho Mpoto. Lady JD
Wizara haiwezi fanya maamuzi kwa kuogopa uzushi, lete uthibitisho hapo serikali watakuwa na makosa
 
Phd ya kutunukiwa kamwe haiwezi kuwa sawa na ya darasani japo linapokuja suala la mtu anayetunukiwa anaweza kuwa kafanya mambo yenye heshima kuliko mwenye phd ya darasani au kainunua tu au kapewa kisiasa.
“Kuinunua tu au kapewa kisiasa” hiki ndicho ninachopinga
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
View attachment 3191199

Hatimaye wizara ya elimu imeona umuhimu wa kuingizwa kwenye mitaala ya elimu wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz. Diamond na wasanii wengine wachache wa mfano kwa sasa wanasomwa na wanafunzi wetu darasani. Kwenye somo jipya la civic and moral diamond ametumika sana kama mfano mzuri wa watoto kujifunza.

Bado PhD kutoka university of dar es salaam na sanamu lake.
Elimu gani sasa apo unaona umeitoa
 
Shilole anajulikana ni pro****ute ila watu wanataka kuwafundisha kuwa ni mfano bora.
Nasibu anajulikana ni wom****er na watu wanataka kuwafundisha watu kuwa ni mfano bora.
Elimu ya Afrika ni matatizo matupu
 
Elon Musk ana PhD ya chuo gani? Angalau yeye Ana Bachelor’s na Master’s na alishaanza kusomea PhD kabla ya kuacha na kwenda kufany biashara
 
Nyie ndio mnaosababisha mpaka kina Kabendera waandike vitabu
 
Hivi unajua hata kusoma ? Au kwanza ujifunze kusoma na kuelewa ndio uje kutoa hoja... Au umeamua tu kupotosha na kuchangamsha baraza.., Nini maana ya kuingiza kwenye mtaala...

Pili hapo context ni nini ? Kama ni kutoa information basi inaonyesha uhalisia jinsi hao watu wameweza kutumia uwezo wao (talent kufanikisha maisha yao) na ndio maana huwa vitabu vina editions nina uhakika wakitoa kitabu kama hicho miaka hamsini ijayo huenda wakamuweka mtu ambaye kizazi hicho kita relate nae..., kama vile ambavyo kizazi cha nyuma kingeweza kuwaweka kina Nyambui na Philbert Bayi au hata Marijani Rajab na Mwanameka wake....
 
Nchi gani hiyo mtoto wa miaka 15 anapaisha ndege?

Kwa ufahamu wangu duniani kote chombo cha moto anaruhusiwa mtu mwenye umri kuanzia 18 yrs.
Fatilia US ndege unaanza kuendesha ukiwa na umri gani
 
Kwa hiyo watu kama Juma nature, Prof Jay, Lady Jay Dee, P Funk Majani/Masterjay hawajakidhi vigezo vya kuingia kwenye mtaala zaidi ya hao new generation artists duh! TZ Education is fvcked up!
 
Elimu ya kweli ipo kenya na uganda. Bongo kila mwenye cheo anajifanyia madudu atakayo tu kwenye system.
 
View attachment 3191199

Hatimaye wizara ya elimu imeona umuhimu wa kuingizwa kwenye mitaala ya elimu wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz. Diamond na wasanii wengine wachache wa mfano kwa sasa wanasomwa na wanafunzi wetu darasani. Kwenye somo jipya la civic and moral diamond ametumika sana kama mfano mzuri wa watoto kujifunza.

Bado PhD kutoka university of dar es salaam na sanamu lake.
Sentensi mbili zinafundisha nini sasa? Watanzabia hatuko serious asee!
 
Back
Top Bottom