Ni kama Bahati vile ila unaweza sema Mungu kampendelea Rais Samia

Inaonekana u azungumza kwa ushabiki.
Alie kuambia vifaa vya ujenxi vya mwekezaji vinachajiwa kodi ni nani?
 
Hiyo Gas ya Mtwara tunafaidika nayo nini kama Nchi?,inavunwa yote na mapato yote wanafaudi wawekezaji

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Mbona niliwahi kusikia kuwa mikataba mibovu sana iliyoingiwa ya Natural Gas itatufanya tusifaidike nayo kwa miaka chungu mzima ijayo,yaani watakaokuja kufaidika ni ni vijukuu vyetu...?
 
Ana nyota njema kweli kikubwa aitumie vizuri vizazi na vizazi tuje Kim kumbuka. Hii ni fursa adhimu kweli kwake
Niliwahi sema humu na narudia ni nadra kwa sasa kupita siku 3 eti hujasikia habari njema za uwekezaji wapya au Mataifa na wakuu wa Taasisi za Dunia hawajafika Tzn kuchungulia fursa au kusaidia nchi.

Kikubwa tujifunze kuchangamkia fursa za kushilikiana nao tupige hela,sio kama wale wa madini ya dhahabu walipata washirika baada ya kuchukua pesa za wenzao wakaanza kujificha na kusingizia wanaumwa covid mara wamekufa.

Hii kaongea Biteko,kama kawaida ya WaTzn uhuni na kulalamika ndio tunaweza..

Hapa Waziri wa mambo ya Nje wa Jamhuri ya Schec yuko Bongo na wafanyabiashara 👇





 
Usisahau10% lazima ipo, wanaofunga mikataba itawanufaisha

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Uhuni unawaharibia sana watanzania. Hapa vyombo vya dola inabidi vikaze Kweli! Wanapenda sana utapeli na wanakuwa Kama Wanigeria
 
Mbona niliwahi kusikia kuwa mikataba mibovu sana iliyoingiwa ya Natural Gas itatufanya tusifaidike nayo kwa miaka chungu mzima ijayo,yaani watakaokuja kufaidika ni ni vijukuu vyetu...?
Ulisikia kutoka kwa Nani? Usilete Habari za vijiwe vya kahawa hapa
 

..nazungumzia faida au hasara kwa WAWEKEZAJI ktk mradi wa LNG.

..Wawekezaji ktk huo mradi ni serikali kwa niaba ya Watz, na makampuni ya uchimbaji ya kigeni.

..Na faida au matumaini ya faida kwa wawekezaji ktk mradi ndio kichocheo cha faida za watu wa pembezoni kama mahoteli, real estate, etc etc.
 
Hoja yako ni ipi sasa?
 
..Hoja yangu ni kwamba tujikite kwenye faida au hasara kwa WAWEKEZAJI wa mradi wa LNG ambao ni serikali ya Tz na makampuni ya uchimbaji toka nje.
Naamini timu ya majadiliano itakuwa imezingatia hayo yote ili kuhakikisha Faida inachukua nafasi hata kwenye hatari ya kupata hasara
 
Umesema kweli kabisa gesi inalipa haswa na ndio maana hata Qatar wamepatia hela ndefu hapo na kuwatunishia misuli wengine

Alipokatiwa mahitaji na Saudia akaamua kwenda solo na sasa watu binafsi wana hela nyingi kiasi wameamua kuilisha nchi kwa maziwa na nyama

Tukifanikiwa kuuza gesi tumeula
 

..Ni kweli Qatar wanapiga pesa kubwa kutokana na natural gas.

..lakini tusisahau kwamba Qatar ni nchi ndogo na ina watu wachache sana.

..Hali hiyo ni moja ya factors zinazopelekea Qatar kuweza kufanya matumizi makubwa-makubwa, na raia wake kuishi kwa anasa.

..Nchi kama Tanzania inatakiwa iwe makini sana ktk matumizi ya rasilimali kama madini na gesi kwasababu ya ukubwa wa nchi na idadi ya watu ilionao.

..Naunga mkono hoja yako lakini nilitaka niweke angalizo dogo.
 
Ni mipango tu! Haijalishi kama nchi yako ni kubwa au ndogo au ina idadi wengi au kidogo ya watu!

Tukijipanga vizuri Gesi ndo inaweza kuwa breakthrough kwenye uchumi wetu Tanzania.

Hii nishati inahitajika sana duniani na demand inazidi kuwa kubwa siku hadi siku! Pesa tutakayopiga hapa tunaweza itumia vizuri sana na ikalifaidisha sana Taifa letu
 

Ni kweli Mkuu
Inabidi tutumie akili kubwa kwa manufaa ya nchi
Hii itasaidia mambo mengi sana ya maendeleo

Ila tunaweza kama vijana watawezeshwa kwenda kusoma sana nje na kuja na akili mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…