Ni kama sielewi naombeni ufafanuzi, Kumewahi kuwa nchi au falme inayoitwa Palestina kabla ya 1948 inayoongozwa na waarabu kabla ya 1948 ?

Ni kama sielewi naombeni ufafanuzi, Kumewahi kuwa nchi au falme inayoitwa Palestina kabla ya 1948 inayoongozwa na waarabu kabla ya 1948 ?

Acha matusi huu ni uwanja huru boss. Jibu unavyoelewa boss.
Nipo tayari kukusikiliza na kukusoma.
 
Si rahisi sana kupata taarifa ya uwepo wa taifa la Palestine kabla ya 1948. Historia ya watu hawa imefutwa na kusambatatishwa vibaya. Hawana haki yoyote ya maana ulimwenguni! Wanaopigana kurejesha the so called state of Palestine wamepachikwa jina la magaidi na sio freedom seekers. Ukiinua kimdomo unauawa ! Si ajabu Kuna wazee Wana umri mkubwa kuliko taifa lililoanzishwa mwaka 1948. Wana noti na sarafu za lililokuwa taifa lao.
Too sad.
Sio kweli. Hakuna watu wanaoitwa Wapalestina. Palestina ni eneo la ardhi. Na eneo hilo ndilo liliitwa zamani Israel. Warumi walipowapiga Wayahudi mwaka 70 BK wakaamua kuibadilisha hiyo nchi na kuiuta Palestina. Hivyo tangu mwaka 70 ndipo eneo liliitwa Palestina lakini wenyeji wake walikuwa mchanganyiko wa Wayahudi na makabila mengine. Eneo hilo limekuwa uwanja wa vita tangu enzi na enzi. Eneo hilo liliwahi kuwa chini ya himaya mbalimbali hadi 1914 lilipochukuliwa na Uingereza kuwa protectorate. Kipindi hicho walikuwa wakiishi Wayahudi na Waarabu. Sasa wakati wa kutoa uhuru Waingereza wakagawa nchi mara mbili. Upande mmoja ukaitwa Jordan na upande wa pili ni Palestina . Kukatokea mgogoro baina ya Waarabu na Wayahudi. Waarabu wakidai eneo hilo ni lao na Wayahudi wakidai hilo ni eneo la Israel tangu zamani. Ndipo Uingereza ikaona igawe sehemu mbili. Eneo la Wayahudi na eneo la Waarabu. Wayahudi waliridhia lakini Waarabu wakakataa katakana. Hivyo, Waingereza wakawapa Wayahudi eneo lao na kujitangazia uhuru mwaka 1948. Lakini waarabu ambao ndio hujiita Wapalestina leo Walsingham msituni kupigana vita. Tatizo ni kuwa kila wakipigana wanapigwa na Israel inazidi kujiongezea maeneo. Hii ni kwakuwa hilo eneo ni la Mungu na aliwapa Waisraeli tangu kipindi cha Musa. Na ni Mungu mwenyewe aliyewatoa ktk nchi hiyo baada ya kumuasi. Lakini aliahidi kwenye maandiko kuwa siku za mwisho atawarejesha Israel kutoka mataifa alikowafukuzia. Hivyo tambueni tu kuwa tunaishi siku za mwisho. Yesu Kristo karibu anarudi. Na kadri siku za kurudi kwake zinapokaribia mgogoro wa mashariki utaongezeka. Mwishoni utahusisha mataifa yote!
 
Between 1517 and 1917, the Ottoman Empire—whose official religion was Islam—ruled the region. When World War I ended in 1918, the British took control of Palestine.
IMG_5723.jpeg
 
Maana nimechoka kufanya research siikuti Palestina iliyowahi kuwa nchi au Falme ikiwa chini ya waarabu

Nahitahi kuoneshwa Falme iliyoitwa Palestina na mfalme alieiongoza kama ilivyokuwa kwa Israel ya wayahudi chini ya Mfalme Sauli, Daudi, Solomon, Herodi, n.k.
Screenshot_2025-01-11-23-02-14-640_com.twitter.android.jpg
 
Maana nimechoka kufanya research siikuti Palestina iliyowahi kuwa nchi au Falme ikiwa chini ya waarabu

Nahitahi kuoneshwa Falme iliyoitwa Palestina na mfalme alieiongoza kama ilivyokuwa kwa Israel ya wayahudi chini ya Mfalme Sauli, Daudi, Solomon, Herodi, n.k.
Sauli, Daudi, solomon na Herodi hawakuwa wazungu bali wapalestina wa zamani proved by Science.

Na neno Palestina linatumika hata kabla Yesu hajaja, kuna evidence nyingi mno, Soma hii article ya Wikipedia

Maana nimechoka kufanya research siikuti Palestina iliyowahi kuwa nchi au Falme ikiwa chini ya waarabu
Sijaelewa point ya swali lako. Ila kiuchache nchi nyingi hazikuwepo kama lengo lango unamaanisha jina ndilo linalofanya nchi iwepo.

Tukianza hapa nyumbani Mwaka 1963 kurudi nyuma TANZANIA haikuwepo.

Turkey imebadilisha jina na sasa hivi inaitwa Turkiye. Je Miaka kadhaa nyuma Turkey ilikuwepo au haikuwepo?

Mwaka 1935 hakukuwa na nchi inaitwa Iran.

Mwaka 1980 hakukuwepo na nchi inaitwa Zimbabwe.

Palestine ilikuwepo tangu karne kwa kane na jina lake la asili ni Falistin.

Sasa kutokuwepo kwa jina hakufanyi ardhi ya ile nchi haijakuwepo. Kwa sababu unaamini sana wazungu nimekuweka hiyo attachment ya Bbc.
Screenshot_20250115-023826.png
 
Haikuwepo, Palestina ilikuwa sehemu ya Ottoman Empire
Umetufungia mada.

Comments zote kabla yako zina walakini kuhusu jibu toshelezi la mtoa hoja.

Umejibu swali la mada kimantiki.

Lakini ulitakiwa umwage darasa la historia ya jambo hili kabisa ili kutuliza 'mchafukoge' tuliotoka nao tangia comment #2 na kuendelea.
 
mbulula za kibongo hata hela ya kula mgogoro, lakini muda wanao kungojera historia ya kale ambayo hata mababu zao haiwahusu....
 
Sio kweli. Hakuna watu wanaoitwa Wapalestina. Palestina ni eneo la ardhi. Na eneo hilo ndilo liliitwa zamani Israel. Warumi walipowapiga Wayahudi mwaka 70 BK wakaamua kuibadilisha hiyo nchi na kuiuta Palestina. Hivyo tangu mwaka 70 ndipo eneo liliitwa Palestina lakini wenyeji wake walikuwa mchanganyiko wa Wayahudi na makabila mengine. Eneo hilo limekuwa uwanja wa vita tangu enzi na enzi. Eneo hilo liliwahi kuwa chini ya himaya mbalimbali hadi 1914 lilipochukuliwa na Uingereza kuwa protectorate. Kipindi hicho walikuwa wakiishi Wayahudi na Waarabu. Sasa wakati wa kutoa uhuru Waingereza wakagawa nchi mara mbili. Upande mmoja ukaitwa Jordan na upande wa pili ni Palestina . Kukatokea mgogoro baina ya Waarabu na Wayahudi. Waarabu wakidai eneo hilo ni lao na Wayahudi wakidai hilo ni eneo la Israel tangu zamani. Ndipo Uingereza ikaona igawe sehemu mbili. Eneo la Wayahudi na eneo la Waarabu. Wayahudi waliridhia lakini Waarabu wakakataa katakana. Hivyo, Waingereza wakawapa Wayahudi eneo lao na kujitangazia uhuru mwaka 1948. Lakini waarabu ambao ndio hujiita Wapalestina leo Walsingham msituni kupigana vita. Tatizo ni kuwa kila wakipigana wanapigwa na Israel inazidi kujiongezea maeneo. Hii ni kwakuwa hilo eneo ni la Mungu na aliwapa Waisraeli tangu kipindi cha Musa. Na ni Mungu mwenyewe aliyewatoa ktk nchi hiyo baada ya kumuasi. Lakini aliahidi kwenye maandiko kuwa siku za mwisho atawarejesha Israel kutoka mataifa alikowafukuzia. Hivyo tambueni tu kuwa tunaishi siku za mwisho. Yesu Kristo karibu anarudi. Na kadri siku za kurudi kwake zinapokaribia mgogoro wa mashariki utaongezeka. Mwishoni utahusisha mataifa yote!
Umejitahidi kunyoosha, tatizo ukiingiza tu dini, unakuwa ushaharibu.

Pia unatakiwa kuidadavua history tangia angalau mfalme Daudi, Roman empire hadi British proctorate of Palestina, ungekuwa umetufungia mada kwa kunyooka.

Ingelibakia tu watu kunyenyua mikono kutaka kujaziliza nyama nyama kidogo.
 
mbulula za kibongo hata hela ya kula mgogoro, lakini muda wanao kungojera historia ya kale ambayo hata mababu zao haiwahusu....
Somo la historia lipo kwenye mitaala ya elimu ya Tz, kwa hiyo ukiona watu wanajadili historia flani, usiwaone ni mbulula, ni wasomi wenye akili zao timamu.

Mawazo yako kama mdau, ulitakiwa uyatoe kwa Waziri wa elimu hivi karibuni walipokuwa wakirekebisha mitaala ya elimu, ili kupendekeza somo la history lifutwe mashuleni.
 
Mkuu we ni muchknow sana. Haupo tayari kusikia usichokipenda. Fungua ubongo, sikiliza tafakari.
Na Tena usisahau changia maoni yako huku ukiamini kwamba wazo lako si Bora kuliko yote. Ukubali challenge jibu ki ungwana
Acha kunipangia namna ya kujibu. Mwambie aliyeuliza awe na uhakika na anachouliza. Halafu pia hili ni jukwaa huru kama unaona majibu yangu yanakukera pita vileee usiyasome.
 
Maana kila nikifanya research sikuti sehemu yoyote Palestina iliyowahi kuwa nchi au Falme.

Nahitahi kuoneshwa Falme iliyoitwa Palestina iliyokuwa chini ya waarabu
Kwanza MOTO mmezima naona mnataka kututoa kwenye reli mwambie uyo Jehova wenu azuiwe MOTO Wafadhili wa taifa la mchongo Wamarekan wajumba yao mahospitali yao makanisa yao miundombinu muimu inateketea!!!! nyinyi vip mnaleta mada ya kitoto mkishiba kande yanawapeleka mbio mbio wewe endelea kununua udongo mtoto wajuzi wewe na vimaandiko vyako kawaulize UN watakujibu mana UN wanatambua uwepo wa Palestina na wanatambua Israel ilianzishwa kwenye kipende cha ardhi ya Palestina mwaka 1948 kwaazimio la mwakilishi kutoka uingeleza na siku wanaamia ktk ardhi ile waisrael walikwenda kupitia bahari wakiwa kwenye majahazi kama aya unayaona pale ferry wavuvi wanayatumia kusakia samaki ndio ayoayo waisrael waliyatumia kwenda ktk ardhi ya Palestina kupitia azimio la UN.
 
Kabla ya 1948, eneo la Palestina halikuwa nchi moja yenye serikali yake. Lilikuwa chini ya utawala wa mataifa mengine kwa karne nyingi, ikiwa ni pamoja na Dola la Ottoman na baadaye Uingereza. Hata hivyo, eneo hilo lilikuwa na waarabu wengi ambao wameishi huko kwa karne nyingi.
 
Back
Top Bottom