Maana nimechoka kufanya research siikuti Palestina iliyowahi kuwa nchi au Falme ikiwa chini ya waarabu
Nahitaji kuoneshwa Falme iliyoitwa Palestina na mfalme alieiongoza kama ilivyokuwa kwa Israel ya wayahudi chini ya Mfalme Sauli, Daudi, Solomon, Herodi, n.k.
Mkuu ni KWELI hapakuwahi kuwa na DOLA inayoitwa Palestine...... ila palikuwepo na eneo lililobadilishwa jina na kuitwa PALESTINE na wakaazi wa eneo hilo wakawa Wapalestina
Kama nimekuelewa vizuri unamaanisha ni kwanini Wapalestina wanadai nchi ambayo HAIKUWEPO?
kwanza kabisa unapaswa kujua HISTORIA ya binadamu na uanzishwaji wa mataifa YANAYOTAMBULIKA sasa
Binadamu ni kiumbe anayehama hama kila wakati kwasababu mbali mbali
Ndio maana leo hii watu wa jamii ya kiarabu utawakuta kwa wingi Afrika Kaskazini ambapo ni asili ya watu weusi
Na ndio maana leo hii jamii ya wahindi wekundu wa Amerika wamemezwa na jamii ya wazungu kutoka Ulaya waliokuja kufanya taifa la USA
Nadhani umesoma kuhusu Ngoni immigration nk nk
Hawa wambulu na wa Iraki nk wamehamia kutoka Afrika ya juu na kusambaa hadi Tanganyika na sasa Tz
Hali hiyo ya kuhama hama pia ilihusu pia eneo la mashariki yakati ikiwemo Israel/Palestine
Kama waarabu waliweza kusambaa na kufika Misri, Moroko, Aljeria, Tunisia nk
Waliweza pia kufika “Israel” na wakaanzisha makazi
Ikumbukwe kwamba Waisrael wengi walilikimbia eneo lile kwasababu ya tawala mbali mbali za mkono wa chuma dhidi yao zilizokua zinatawala pale kwa kupokezana baada ya vita
Inakadiriwa kwamba ilifikia wakati zaidi ya 90% ya wakaazi wa eneo lile walikua ni waarabu na jamii zingine
Kwasababu ya waarabu ku dominate eneo hilo hata majina yakaanza kutumika zaidi yenye asili ya kiarabu...... na hapo ndipo watawala wakatumia jina Palestine
Toka waarabu waanze kuishi pale inakadiriwa ni miaka isiyopungua 600..... miongo kama 6 hivi
Tunapaswa kujua ni namna gani mataifa yalianzishwa enzi hizo baada ya kuwa na vita nyingi sana za kugombania utawala na aridhi
Mfano Tannganyika
Wakati tunadai uhuru hapakua na taifa linaitwa Tanganyika wala hapakua na watanganyika
Palikua na eneo ambalo watawala walikua wanalitawala
Muingereza alipotupa uhuru raia wote waliokua ndani ya nchi hii walikuwa watanganyika automatically...... hii ndio ilikua KANUNI
Tukija kwa Israel/Palestine eneo lile lilikua chini ya Uingereza pia na lilikua linaitwa Palestine
Na uingereza ilikua na jukumu la kuwapa uhuru wao wajitawale
Sasa ukitaka kujua shida iko wapi kwa waarabu na waisrael tafuta sababu ya kwanini uingreza haikutoa uhuru kwa taifa moja kama ni Palestine au Israel na raia wote wa eneo lile wawe raia automatically?