Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Hii nchi kumbe ndio maana ina machawa tu, tunaweza kuwa tunalaumu viongozi ila wanaowazunguka ndio sampuli hizi zenu humu. Jamaa kauliza swali kama Vunjabei anaelekea kufirisika, kwa wenye akili ambao hawajazaliwa na wachawi na waganga wa kienyeji hilo ni swali la kawaida halina wivu au roho mbaya.

Ni suala la kujadili kibiashara, kwamba Vubjabei kawekeza kwenye madawa ya binadamu nguo anaona zimevamiwa, kapata sekta nyingine inayomlipa zaidi, au kapata ushindani, au ameuza brand, au aliingia kwenye nguo akiwa na exit plan na mpango wake umetimia. Sasa badala mjadili kibiashara sababu yeye mwenyewe aliileta public biashara yake hivyo ni lazima ijadiliwe. Nyinyi mnaijibu kama waganga wa jadi, wachawi, wenye wivu, wanafiki.

Kwani biashara inatakiwa izungumziwe kwa sifa tu, hakuna kuhoji au kuuliza?

"Jana nimepita Iringa napo naona lile duka alilolifungua kwa
mbwembwe nalo lishajifia na kufungwa muda tu.
Hapo Dar duka lake la Sinza nalo linapumulia mashine."


Ukisoma namna alivyowasilisha utabaini dhamira. Inaoneka hilo duka lililofunguliwa kwa "mbwembwe" lilimuumiza sana na aliisubiri hii siku kwa hamu sana.
 
Unapata wapi huo mda wa kufutilia biashara ya mtu kiasi hicho?huo mda ungeuza hata barafu ungesogea kidogo kwenye maisha yako
Timu DAI, imeona Mwijaku amemdharau sana Dangote kuwa, utajiri wake haufikii hata 40% wa VB. Sasa wanafanya uchunguzi, jee, ni kweli Dai hafikii hata % 40 kwa hali hiiii?
 
Wakipata kidogo kelele vuvuzela.Lakini wenye nazo Huwa hawana maisha ya mitandaoni na udaku.

DC wa zamani Sasa ana Cheo kipya afanye jambo huyu asije jitundika 😆😆
Vunjabei akiwa anasema kuhonga wanawake wetu na kuwapa hela huwa silalamiki kwa sababu ni mtazamo wake, mimi wanawake siwapi hela burebure.

Sasa kama yeye ana uhuru wa kujadili wanawake wetu, ana uhuru wa kutangaza biashara zake na kuzipa promo kwa media. Kwanini walengwa wasiwe na uhuru kujadili biashara zilezile alizowatangazia na wasiwe na maoni juu ya maisha yake eti waogope kuitwa wachawi
FB_IMG_1725624732802.jpg
 
The guy is a head of the time
Smart
Humble

Anaweza kushuka kimpato Ila hawezi kufirisika kuwa financially broke.

Maana fred hajawekeza ktk nguo tu Ila amewekeza ktk biashara tofauti tofauti.
 
Nilikuwa Mbeya huko nikapita mitaa ile ya SIDO ni kama vile duka la Vunjabei linapumulia mashine, halina mzunguko wa biashara kivile.

Jana nimepita Iringa napo naona lile duka alilolifungua kwa mbwembwe nalo lishajifia na kufungwa muda tu.
Hapo Dar duka lake la Sinza nalo linapumulia mashine.

Ni kama vile jamaa kaanza kufilisika mdogo mdogo.

Nimeambatanisha picha za duka lake la Iringa lililofungwa.

View attachment 3088613
Kwa hiyo unafurahia anguko la mwenzio? Je kama kabadirisha aina ya biashara?
 
Back
Top Bottom