Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Vipi kama ameamuwa kubadili biashara anata amalizie stock?

Acha uchawi haukupendezi.
 
Kwa maana hiyo mkuu una kazi ya kupita kila mkoa kukagua maduka ya vunja bei?
 
Jamaa siku hizi kaamua kuwa supplier wa madawa na vifaa vya hospital na ndio maana yupo karibu na chama tawala ,kwenye mikutano hakosekani sababu ya kujipatia tenda.So jamaa anadeal na maswala ya Pharmacy.
 
Kumbe ndio wewe uliyokuwa unapiga picha jana hapa Iringa sio?
 
Aah mi sijaona negativity bahati mbaya huwa sio mrahisi kuona chuki sijui roho mbaya huwa naenda kwenye concern ya mtu. Ila Vunjabei mwenyewe ni watu wengi wanasema ana dharau na jeuri ya hela akiwa anahonga, na wala simuoni hivyo. Mi naona maoni ya watu wabishane kwa hoja sio kuleteana uzoefu wa uchawi
 
Muda huo unachunguza maduka yake,ungekuwa unafanya kazi zako,ungejiingizia chochote. Sasa,unakalia majungu tu
 
Jamaa siku hizi kaamua kuwa supplier wa madawa na vifaa vya hospital na ndio maana yupo karibu na chama tawala ,kwenye mikutano hakosekani sababu ya kujipatia tenda.So jamaa anadeal na maswala ya Pharmacy.
Biashara ya madawa inalipa sana iwe madawa halali au madawa haram.
 
Kwa hiyo unaomba uchunguzi ufanyike, kwa nini Fred vunja bei kafirisika!!??
Kama anavo inspire watu na ku motivate watu kupata pesa Kwa media,pia tunataka kujua Kwanini maduka yake ya nguo sio kama yalivokua,hakuna traffic na maybe wafanyakazi wamepungua.

Yeye sio mfanyabiashara peke yake,ila yeye aliamua maduka yake yawe public talk and yeye mwenyewe kua public figure. Ingia YouTube andika Fred vunjabei uone Kuna videos ngapi zinazomhusu yeye akiongelea maduka yake.
 
Vunjabei kupanua biashara mikoani Kwa kudhani uchumi wa Mikoani unaweza ukafanania na Dar. Hizi bidhaa za bei rahisi kutoka China zinafanya watu waangalie ubora zaidi kuliko bei, na ukiangalia mikoa kama Mbeya, watu wengi wanapendelea mitumba kwa sababu ya bei nafuu na ubora mzuri. Kwa hiyo, ni ngumu sana kushindana na soko la mitumba kwa kuuza bidhaa za kawaida ambazo hazikidhi matarajio ya watu.

Huko Dar es Salaam alifanya vizuri kwa sababu ya wingi wa wateja na uwezo wa kununua, lakini huko mikoani hali ni tofauti kabisa. Sidhani kama kupanua biashara kote ilikuwa wazo sahihi, labda angejikita zaidi Dar es Salaam na kuboresha ubora wa bidhaa zake, hata kama bei ingeongezeka kidogo. Bora kuuza bidhaa chache lakini zenye ubora kuliko kujaribu kupanuka kwa kuuza vitu vya kawaida ambavyo vina ushindani mkubwa, hasa Kariakoo ambapo watu wanapata vitu hivyo hivyo kwa bei nafuu zaidi.
 
Iringa duka haliko mbele hapo bali liko nyuma ya hilo jengo ni kubwa tu
 
 
Tatizo Jeans za Vunjabei ukifua mara moja tu zinachujuka... Kukosa Tender ya kutengeneza Jezi za Simba pia kumempa kushuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…