Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Nilikuwa Mbeya huko nikapita mitaa ile ya SIDO ni kama vile duka la Vunjabei linapumulia mashine, halina mzunguko wa biashara kivile.

Jana nimepita Iringa napo naona lile duka alilolifungua kwa mbwembwe nalo lishajifia na kufungwa muda tu.
Hapo Dar duka lake la Sinza nalo linapumulia mashine.

Ni kama vile jamaa kaanza kufilisika mdogo mdogo.

Nimeambatanisha picha za duka lake la Iringa lililofungwa.

View attachment 3088613
Alipofika kileleni akaingia kwenye ushirikiano na CCM akidhani utajiri wake umetokana na hilo zimwi.

Wateja tumeamua kuachana naye ili atumikie ndoa yake na CCM....
 
Alipofika kileleni akaingia kwenye ushirikiano na CCM akidhani utajiri wake umetokana na hilo zimwi.

Wateja tumeamua kuachana naye ili atumikie ndoa yake na CCM....
Wateja wangapi mmekubaliana hivyo?
 
Hizi ni dalili za juu kabisa za UCHAWI. Afu mbaya sana wakati unafuatilia hayo maduka ulipanda gari za umma.
 
Bora waganga kuliko hawa wachungaji na manabii. Kuna wakati nilipoteza mwelekeo mzima wa maisha nikaona bora niende kuombeawa. Mchungaji wa kwanza alinipokea vizuri siku ya kwanza na kuniombea ila wakati naaga akaniambia nirudi wiki inayofuata na bahasha ya sadaka angalau 20k. Nikaona fresh tu. Mara ya pili alizingua alivyoniambia nitoe mchango wa vifaa vya muziki vya kwaya. Kimoyomoyo nikajiuliza huyu K mbona anaanza ishu za kiwaki? Yaani mimi hata kula ya tabu nitoe mchango wa vyombo vya kwaya? Sikurudi tena. Nikaona niende kwa GeorDavie mwenyewe. Nafika Kisongo kumbe kuna utaratibu wa kishenzi kuliko nilivyodhani. Ilikuwa ni kulipa Tsh 500 kuombewa na wasaidizi wake. Mimi nililipa Tsh 500 nikaombewa na kina mama fulani ambao walionekana kama wamepigika kuliko hata mimi. Geordavie mwenyewe ilikuwa lazima ulipe noti ndefu sana kuweza kuombewa nae. Uamuzi wa mwisho ilikuwa kwenda kwa mganga. Kuna mganga mitaa ya kambi ya fisi akaniambia nisijali nitamlipa baada ya kazi ila nimletee vifaa vya kazi. Vifaa vingi vilikuwa complicated nikaona bora tupige hesabu nimpe mganga hela akanunue. Kwa hesabu ya haraka ilikuwa zaidi ya laki na sikuwa hata na 10k. Nilikaa chini na kuamua sitaki mambo ya wachungaji wala waganga. Baada kama miaka mitatu nilirudi tena kwenye mstari hadi leo. Wachungaji ninawaheshimu ila najua hawana msaada wowote kwa maskini zaidi ya kuwavuna kidogo walicho nacho.
Vizuri sana mkuu ulipambana.
 
Back
Top Bottom