Hivi hawa wagombea huwa wanaonaje wananchi? Kwamba ni mazuzu? Wanaendaje INEC kuchukua fomu za kugombea urais wakati vyama vyao havijulikani kwa wapiga kura? Vyama vinajulikana kwa msajili wa vyama vya siasa tu kwa wananchi havijulikani! vingine havina ofisi mikoani na wilayani hadi mashinani, vitapataje ushindi kama si vituko vya uchaguzi? kuna vyama vinaokoteza wagombea ubunge na udiwani mradi tu vionekane vimeshiriki, fomu bure kampeni utajigharamikia, elimu yoyote ruksa kugombea. Uchaguzi wa mwaka huu ni vituko vitupu!