Ni kauli gani unaweza kumwambia mgeni wako kuwa ni muda wa yeye kuondoka bila kumkwaza?

Ni kauli gani unaweza kumwambia mgeni wako kuwa ni muda wa yeye kuondoka bila kumkwaza?

Vuta pumzi ndefu kisha anza kujinyoosha kwa kunyanyua mikono juu huku ukipiga na mwayo.

Hiyo ni ishara ya kuonesha umechoka, kama mgeni ni mtu rational atajiongeza.

Au wakati wa mazungumzo kila muda we angalia saa. Atajiongeza
 
Ni kauli gani unaweza kumwambia mgeni wako kuwa ni muda wa yeye kuondoka bila kumkwaza?
 
Mgeni aliyekuja kuishi kwa siku kadhaa halafu hana dalili ya kuondoka? Au mgeni aliyekuja kwako na anaondoka siku hiyo hiyo ila wewe unataka umharakishe aondoke mapema?

Fafanua

Hili ndio swali maana wengi wanafafanua njia ya kumuondoa mgeni aliyekuja kukaa kwa masaa-hawa hawanaga tatizo ila,

Tatizo lipo kwa wageni wanaokaa week(s) [emoji3]
 
Mbona simpo sana kwa anayekuja na kuondoka lakini anayelala hapo Kuna kachangamoto kidogo, lakini twende mbele turudi nyuma mgeni amekutembelea kwanini umharakishe kuondoka?? Tuwe wakarimu jamani haya maisha tutayaacha, Mali tutaziacha tujali utu kuliko kuwaza mambo yetu binafsi
 
Hili ndio swali maana wengi wanafafanua njia ya kumuondoa mgeni aliyekuja kukaa kwa masaa-hawa hawanaga tatizo ila,

Tatizo lipo kwa wageni wanaokaa week(s) [emoji3]
Haya manbo..kuna mahali niliwahi enda ndani ya siku 2 wakaniambia wanasafiri [emoji3]
Toka hapo niliapa kutoenda tena kwenye milango ya watu.
 
'Ee bwana eh'
unasubiri aitikie na akijikausha unarudi 'Eee bwana eh' huku umekunja sura kana umebanwa....chagua mwenyewe....kama mjusi, umebanwa na nnya , umebanwa kidole na kibanio cha nguo.....yani vyovyote vile, alimradi unaonyesha hisia za kukunja uso. Na akijibu unatema.....

'samahani itabidi uanze'

Akiuliza nini tena kulikoni? itabidi uanze upya....'eeeee bwana eeehhhh' unakaza sauti kana kwamba wameongeza sauti redioni huku ukikaza sura 'we anza' 'nitakutafuta baadae.!'

Rahisi sana.
 
Back
Top Bottom