Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukiwa umefulia ambayo leo ukiikumbuka unacheka tu?

Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukiwa umefulia ambayo leo ukiikumbuka unacheka tu?

Japo sijatoka kwenye msoto bado, ila mpaka sasa kazi za ajabu nilizofanya ni pamoja na kufyeka majani na kupalilia majani mbele ya nyumba za watu (kazi tembo mshahara sisimizi),kupakia tofali na kushusha kwenye site za wateja kutoka zinakotengenezwa (tofali moja kupakia na kushusha sh 40/= fu*kin job),kuchimba makaburi ,(kaburi moja 20000/= tupo wanne means tunagawana 5000/=)-hii nimefanya mara mbili mara ya mwisho nikadhulumiwa na wenzangu.
 
Niliendesha daladala mpaka akili zikakaa sawa [emoji2960]

Naheshimu sana nikipanda daladala hua nawatafakari sana huku nikijua wanachokifanya barabarani na nikijua wanachopitia ni maumivu makubwa sana
 
Nikiwahi kuwa saidia fundi kwenye kampuni ya wahindi. Asubuhi mpaka jioni malipo ni 2,000/-. Wahindi wanatukana balsa, hata shule hawana, na tunagimbania kazi asubuhi, na kumyenyekea msimamizi - m'mbogo. Baadhi ya kina dada walikuwa mpaka wanauza 'utu' wao.
We Mungu wajalie nguvu wanafanya kazi kama zile; na ibariki juhudi zangu nisirejee kule
 
Kipindi flani na rafiki yangu mmoja tulipigwa chini kazini,😁
Tukakaa sana kijiweni
Sasa hela 'ishaisha ikabidi tushauriane ebana tukatafute mzigo masaki huko
Gonga moka
Suruali cerebration shati nyeupe.
Twende kazi.
Safari ni kupiga border tu mguu nauli hamna.
Hapo kila mtu ana bonge la bahasha mi certificate.
Border Victoria.
Khanakhazana tukaacha copy .
Kula border kairuki hadi shoppers acha copy
Border tukafika lile boti namanga yule muitaliano fala sana🤣🤣🤣.
Bahati nzuri tukamkuta.
Ikawa enhee tena nilikua natafuta watu km nyinyi njooni ofisini.
Zama kule interview ya fasta tu
Tukapewa kazi.
Yule mnduku kaoa malaya changudoa.
Sie tunatafta riziki.
Pale wateja wenyewe kuhesabu.
Jamaa kajaza camera km zote mle kwenye boti.
Na alituambia kabisa nawaona mda wote.
Ofisini anamonitor km na screen tano.
Kimbembe si na njaa zetu mshahara mdogo tukakubali.
Tukitegemea tip😂😂😂😂
Kwa hiyo kupiga deal pale hamna.
Ukicheck camera unaona yule vuzi labda ananiona
O bay police jirani tu.
Haya tip kasema zote zikusanywe😁
Kuna chupa kwa cashier zote wekeni humo mtagawana mwisho wa mwezi
ebana yaani hapa na njaa yote hii hata nauli hatuna tip unachukua.
Tukafata masharti ,
Mwezi ukapita mshahara nada
Mwezi unaenda wa pili
Hamna kipato.
Lile jimalaya mkewe
bana siku moja si likazama likakomba na zile tip😅
Alikua anacheza kamari casino kaliwa
Anachukua tip zetu kufidia.
Aisee lile timbwili pale
Ilibidi jamaa atulipe atuage
Tukafanye kazi zingine kudadeki zake
 
......niliishia kupewa buku nikaambiwa kanywe chai, hapo ni baada ya kuangaliwa kwa macho nikagundulika niko hoi[emoji3][emoji3][emoji3].

Kazi sikupewa...
1.Nilikuwa fundi vitu vya umeme wa kunjunga kwenye office ya mshkaji pale River side, sikustukiwa na wateja kwakuwa mshkaji alikuwepo muda wote, kuna siku akaniachia office akaenda kariakoo kufuata spare, akaja mteja na pasi yake ya Phillips regulator ilikuwa ngumu kidogo kwenye kuzungusha

Nikajitia bingwa nikaforce ikavunjika, nikapambana nikaifungua pasi nikaibana ile regulator na wire kisha nikairudishia. Mwenye pasi akakuta ndio namalizia.. Ile kutest kwenye umeme lilipiga bonge la shot, mimi kule pasi kule mteja mbio[emoji24][emoji23]
Nikatimuliwa nisionekane tena pale jamaa akaingia hasara ya kulipa pasi

2. Kitaa kikawa kigumu mno. Siku moja nikatembea mpaka Mugabe Sinza, nikakuta mchina anafungua duka la dawa! Nikajifanya mimi mfamasia nikapata kazi
Kuna siku nimeachwa peke yangu akaja mdada mwanae ana pumu kali sana nikamwandikia dozi dokta uchwara mimi. Kumbe sikumpa ya pumu bali ya kushusha pressure.. Mtoto wa watu aliponea tundu la sindano kurudisha number.. Na siku hiyo ndio ilikuwa ya mwisho kuitwa dokta, nilitimuliwa kazi
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Wee Mzee wa Matunguli.....

Umenikumbusha story ya Analyse aliyejifanya ni Plumber akapewa kazi ya kuziba Bomba[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tulienda kuiba vifaa vya ujenzi kwenye kampuni ya ujenzi..
Hakuna siku nilikuwa natetemeka km siku hiyoo..baridi kali ya usiku lakini nilikuwa nasweat balaaaa..
Tulifanikiwa tukapiga ela safii kbss.
Roho ya tamaa ya uwizi ikataka kuanza kuniandama.
Nikaikemea roho hiyo chafuu.
Wale wenzangu walinipa mchongo walipigwa shaba wawili wawili wengine walikuja kuiba kanisani wakasomewa ufunuo ni vichaa siku hizi
Umetubu mkuu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mkuu yaani ulienda kuomba KAZI halafu alivyokuangalia tu akakupa buku akakwambia ukanywe chai? Au ni sijaelewa mimi[emoji23][emoji23][emoji23]
Yeah, aliona nitaharibu kazi yake kutokana na udhaifu niliokuwa nimepigika nao[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kazi(kibarua) ilikuwa ni ya kutumia nguvu
 
Back
Top Bottom