Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukiwa umefulia ambayo leo ukiikumbuka unacheka tu?

Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukiwa umefulia ambayo leo ukiikumbuka unacheka tu?

Kusaidia fundi ujenzi😭😭😭 aiseee! Nilisulubika sana. Kuchanganya zege kupandisha tofali.
Malipo ni 7000/= per day ( from 7 am to 5:30pm)

Nilifanya kazi siku tatu nikaacha.
Nikarudi katika ufundi pikipiki.

Nikamwomba Mungu sana, hamadi! Nikapata kazi sehemu....!

Ujenzi ni kazi ngumu na yenye jasho kupita maelezo.
 
unakata vimeo? hii ni ipi hyo kk?
Sensor kwenye koromeo ukipanua mdomo utakiona, ndio husababisha kupaliwa
Zamani Uswazi pengine hata sasa watoto walikuwa hawazingatiwi afya na usafi hivyo kuugua minyoo sana.. Sasa minyoo ikipanda kifuani na kutaka kutoka nje inakutana na kimeo na mtoto kukohoa
Kwa ukosefu wa maarifa waganga njaa wakawa wanavikata vimeo
 
Nikiwa na degree yng.
Niliosha magari mbezi na sku zngn wakawa hawanilipi. Nashnda bila kula nikrudi home sina hela mwanamke anavuta mdomo ananisimanga, ananichukia hapo nina njaa kali nimeshnda kutwa nzma bila na nalala bila kula.
Nimechoma mahindi mbezi
SITASAHAU KBS MAISHA HAYA.
 
Sensor kwenye koromeo ukipanua mdomo utakiona, ndio husababisha kupaliwa
Zamani Uswazi pengine hata sasa watoto walikuwa hawazingatiwi afya na usafi hivyo kuugua minyoo sana.. Sasa minyoo ikipanda kifuani na kutaka kutoka nje inakutana na kimeo na mtoto kukohoa
Kwa ukosefu wa maarifa waganga njaa wakawa wanavikata vimeo
kaka mshana we ni balaa
 
Nikiwa pale udbs bana,ndipo Wakati lile jengo la pssf Tower lilikua linajengwa.kuna kipindi nilifulia nikawa sina hata mia mbovu..home nako nimeacha wife ana mimba.
Nikawa napiga vibarua vya kubeba zege pale ili walau kukidhi mahitaji.
Saivi hapa namsimulia wife ananicheka tu..
Ni kazi gani ya ajabu uliwahi kufanya kipindi umefulia?
Kuiba jeneza kaburini
 
Niliwahi kuona tangazo la kazi zuri kwenye nguzo ya umeme nikaona bora niwafuate nikapate hiyo kazi kwasababu vigezo ninavyo. Kufika Ngarenaro kwenye ofisi zao kumbe ni wale jamaa wa kutembeza vyombo ambapo muhimu ni kuwa na shati la mikono mirefu na tai. Yule dada niliyemkuta alijawa na roho ya huruma na kuniambia kwa kweli wanataka vijana ila kwa elimu na mwonekano wangu hata yeye haafiki mimi kufanya ile kazi ila kama nitalazimisha fresh tu kesho niende nikaanze. Ikabidi nimsikilize. Wakati narudi home nikaona wasabato kanisa la mjini kati wako kwenye shughuli yao ya Makambi hali ni mida ya lunch ikabidi nijiunge kwenye foleni kupiga msosi. Hiyo wiki nzima mida ya lunch nikawa nakula kwa wasabato. Sintakaa nisahau. WASABATO ninawashukuru na nimejipanga nitafute hata kanisa lao jipya ninunue vyombo vya muziki kama shukrani yangu.
 
Niliendesha daladala mpaka akili zikaa sawa [emoji2960]

Naheshimu sana nikipanda daladala hua nawatafakari sana huku nikijua wanachokifanya barabarani na nikijua wanachopitia ni maumivu makubwa sana
Nilifanyakazi ya ukondakta kwenye daladala bagamoyo to mwenge nikiwa na digrii yangu ya Marketing. Nakumbuka siku ya kwanza tumeamka saa 10 alfajiri picha linaanza vituo sivijui coz dar nilienda tu kutafuta kazi baada ya kumaliza chuo. Nikasota kama miez 8 hakuna cha maana nafanya ndio nikaamua kujiseti kwenye dala dala. Basi siku ya kwanza hiyo kuamka saa 10,piga kaz siku nzima umesimama coz ilikuwa tukienda bagamoyo na kurudi tunaanza kupiga mwenge tegeta nyuki jioni tunaiba ruti na kuvunja ruti.
Tukitoka mwenge tunaunga kawe,then kawe tunapakia kwanza tangi bovu wakienea level siti ndio tunaita tegeta. Hii ilikiwa inasaidia kupata hela nyingi,kipindi hicho kushuka na 30,000 ilikiwa kawaida. Sasa mziki ni ule uchovu wakeuniform chafu (ilibidi nishone za kwangu siku nikipumzka nashuka nazo),matusi ya abiria sasa ukiwa kanyaga kidogo (kuna siku asubuhi nmepakia watoto wa shule nursery kuna mmoja nikamkanyaga kidogo nikasikia mwenzake anasema achana na makonda hao hawana akili hata shule hawajasoma[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]),
 
M

Maumivu gani wanayopitia
Ile kazi ni ngumu sana kaka hasa kwa mazingira ya dar es salaam. Kondakta anasimama siku nzma,matusi ya abiria,usumbufu wa trafki nk. Ila kwa kipindi nafanya hii kazi hela ilikuwepo nilisave sana hela nakumbuka kila wiki nilikuwa naweza kuweka benki 150,000. Kwa tuliosoma soma kidogo kufanya ile kazi inabidi ujitoe aibu kabisa coz nakumbuka kuna siku natoka mwenge stendi gari imetema balaa naenda tegeta nimebembea mlangoni chini nawaina jamaa nimesoma nao chuo wamekula moka kali na wakaniita Ommy bro ni wewe? Nikawaambia ndio ni mimi nipo town tuonane wkend mazee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nilifanyakazi ya ukondakta kwenye daladala bagamoyo to mwenge nikiwa na digrii yangu ya Marketing. Nakumbuka siku ya kwanza tumeamka saa 10 alfajiri picha linaanza vituo sivijui coz dar nilienda tu kutafuta kazi baada ya kumaliza chuo. Nikasota kama miez 8 hakuna cha maana nafanya ndio nikaamua kujiseti kwenye dala dala. Basi siku ya kwanza hiyo kuamka saa 10,piga kaz siku nzima umesimama coz ilikuwa tukienda bagamoyo na kurudi tunaanza kupiga mwenge tegeta nyuki jioni tunaiba ruti na kuvunja ruti.
Tukitoka mwenge tunaunga kawe,then kawe tunapakia kwanza tangi bovu wakienea level siti ndio tunaita tegeta. Hii ilikiwa inasaidia kupata hela nyingi,kipindi hicho kushuka na 30,000 ilikiwa kawaida. Sasa mziki ni ule uchovu wakeuniform chafu (ilibidi nishone za kwangu siku nikipumzka nashuka nazo),matusi ya abiria sasa ukiwa kanyaga kidogo (kuna siku asubuhi nmepakia watoto wa shule nursery kuna mmoja nikamkanyaga kidogo nikasikia mwenzake anasema achana na makonda hao hawana akili hata shule hawajasoma[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]),
Kazi ya daladala sitaki hata kuikumbuka kwakeli, na kushuka na 30 au 40 sio jambo la kushangaa ila ishu niza msimu, mara nyingi ni yale majira ya mwisho wa mwezi, ila kuanzia hapo niaumivu, na bahati mbaya nyingine sikua kondakta pengine ndio maana nilipata maumivu makubwa
 
Hakuna kazi mbaya mkuu ,kazi ni kazi ,watu wanaendesha maisha kwa kazi hizo hizo unazozidharau.

Kuna mwanamuziki Kenya Mustafa miaka ya 2009-2012 ali hit sana na alikuwa na chapaa na demu mkali ,juzi juzi niliona alikuwa anachangiwa pesa na kina jaguar ,alifulia ikabidi aanze kazi za saidia fundi za ujenzi.

Mimi kazi yeyote kwangu ipo poa ili mradi napata chapaa....Mimi nimekaa na hawa wachuuzi ,asikwambie mtu jamaa wanapata mpunga sana,kuna jamaa anauza matikiti ya kukata haya yanauza buku kipande ,jamaa ana mjengo mzuri hata mtu mwenye degree anayelipwa laki 7 kwa mwezi hana....Kuna jamaa ni chinga k/kko ana mjengo wa maana kpiga hadi fensi na kaweka aluminium window.

Kazi ni kazi...Hakuna kazi mbaya ,kuna watu wanashinda kwenye computer na wanapigwa kipupwe lakini mshahara haikutani ,anadaiwa kwa mangi balaa,kuna hawa chinga jua lake mvua yake lakini maisha yake safi mjengo wa maana.

Mimi nimepiga kazi zote ,ujenzi ,kuuza mkaa,machungwa ,udalali ,kulima maeneo ya watu kwa kuyasafisha,sales,viwandani etc
 
Kusaidia fundi ujenzi😭😭😭 aiseee! Nilisulubika sana. Kuchanganya zege kupandisha tofali.
Malipo ni 7000/= per day ( from 7 am to 5:30pm)

Nilifanya kazi siku tatu nikaacha.
Nikarudi katika ufundi pikipiki.

Nikamwomba Mungu sana, hamadi! Nikapata kazi sehemu....!

Ujenzi ni kazi ngumu na yenye jasho kupita maelezo.
  • Nilifanyaga mwaka. Duh! Siku moja tunamwaga zege la juu floor ya kwanza (kama ujuavyo zege hailali), kufika saa 8 jamaa mmoja akashindwa - akaondoka - hela yake ikalipia maji (hakuambulia kitu).
  • Imepita miongo kadhaa ila bado nina alama za kuunguzwa na cement.
  • Ahsante Mungu kwa hali yangu ya sasa.
 
Back
Top Bottom