Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukiwa umefulia ambayo leo ukiikumbuka unacheka tu?

Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukiwa umefulia ambayo leo ukiikumbuka unacheka tu?

Siku ingine bana nikasindikizwa kuacha kazi na walevi wenzangu😅😅😅
nilikua na jimama langu jitu la deal mishen town.
Deal likiitika tunachezea dollar tu , tatizo matumizi yake sasa
Ni pombe na starehe tu mpk hela iishe
Hela ikiisha mi naenda kutafuta kazi yoyote mradi tu nizugie zugie.
Kipindi fulani tuko apeche alolo nikachukua deiwaka fulani msasani mwisho kule muitaliano.
Bartender
Dah manyanyaso km yote
Nikawa namvumilia tu
Miezi miwili
E bana huku jimama deal likaitika kalamba midollar ya kutosha.
Kazi mi siitaki pia.
Aah siku hiyo tumeanza na supu na bia zikanoga weeh.
Jioni natakiwa mzigoni.😂😂😂
Namuaga jimama anasema weeeh uende wapi?
Kazini.
Unalipwa ngapi?
Sijui ilikua buku70000 enzi hizo.
Nikapigwa dola elfu moja.
Hakuna kufanya kazi kaa nyumbani😁unilee.
Twende ukaache kazi😅😅😅,
Hapo kuna wapambe wanne na sisi mtu 2 tuko sita.
Vuta mashine hadi kazini.
Ile tunaingia tu bosi kaniwai we unakuja sa hii umechelewa hivi mineno kibao.
Alikula kikumbo nikazama bar anatoa macho.
Jimama na wapambe wameingia nikawapa kinywaji cha kutosha na nikatoka nikakaa nao.
Bosi anashangaa tu😅😅😅.
Mwisho namuita namwambia naacha kazi kata hizi bia hapa kwenye mshahara nakudai😅
nigee chenchi yangu tuondoke.
E bana jamaa alichoka.
Anasema si umalize kazi kwanza alafu uje siku ingine.
Nikamwambia siji tena hapa we fanya nilichosema.
Hapo wapambe wa jimama sasa yani wanamtamani mzungu.
Wanasema unamchelewesha nenda counter chukua hela zote tuondoke.
Bahati yake aliwai kuleta hela tukatimua.
Aisee eti umesindikizwa na walevi wenzako kuacha kazi😂😂
 
Tulienda kuiba vifaa vya ujenzi kwenye kampuni ya ujenzi..
Hakuna siku nilikuwa natetemeka km siku hiyoo..baridi kali ya usiku lakini nilikuwa nasweat balaaaa..
Tulifanikiwa tukapiga ela safii kbss.
Roho ya tamaa ya uwizi ikataka kuanza kuniandama.
Nikaikemea roho hiyo chafuu.
Wale wenzangu walinipa mchongo walipigwa shaba wawili wawili wengine walikuja kuiba kanisani wakasomewa ufunuo ni vichaa siku hizi
Ufunuo wa Yohana au ???
 
kujifanya kilema kanisani kwa kakobe nikapewa posho nikaombewa nikapona bahati mbaya ndugu zangu wakaniona kwenye TV
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Daah kumbe huwa wanatoa posho
 
Back
Top Bottom