Baada ya kumaliza chuo 2018 michongo iligoma kabisa, baada ya kuzurula Sana kutafuta ajira Siku moja nilikutana na Jamaa mmoja kwenye daladala baada ya story mbili tatu akanambia amepata kazi Aghkhan anatafuta chumba cha kupanga.
Wazo likanijia nikamwambia mimi ni dalali na Kuna vyumba viko vinapangishwa maeneo ya ubungo na kimara navifahamu na ninaweza kumsaidia kupata chumba kwa malipo ya pesa mwezi mmoja, hapo sio dalali na wala hivyo vyumba sivijui vilipo tukakubaliana tukutane siku ya pili nimpeleke akavione hivyo vyumba.
Siku ya pili nikaamka asubuhi na mapema nikaenda maeneo ya ubungo Riverside nikatafuta madalali wa pale nikampata mmoja nikampanga nikamwambia mimi ni dalali na Kuna mteja anahitaji chumba cha kupanga nikachukua mwasailiano yake na tukakubaliana baadae nije nae, nikaenda kimara nikatafuta Dalali nikampanga pia.
Badae jamaa akanicheki nikampeleka Ubungo Riverside akacheki vyumba hakuvipenda, nikampeleka Kimara akacheki akapenda hapo chumba sebule na jiko 200k akalipa akanipatia 200k nikamgawia dalali 100k.
Hiyo siku ndo niligundua udalali unalipa nikaanza kuwatafuta madalali kupitia Instagram wakipost nyumba na mimi nazichukua napost nikipata mteja namcheki muhusika nampanga naenda na mteja tunapangisha tunapata pesa, hadi baadae nikaja kua dalali mkubwa Sana Dsm na nikawa nawateja wengi Sana lakini nilikuja kuacha udalali 2021 baada ya kupata mchongo wa kueleweka.