Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukiwa umefulia ambayo leo ukiikumbuka unacheka tu?

Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukiwa umefulia ambayo leo ukiikumbuka unacheka tu?

1.Nilikuwa fundi vitu vya umeme wa kunjunga kwenye office ya mshkaji pale River side, sikustukiwa na wateja kwakuwa mshkaji alikuwepo muda wote, kuna siku akaniachia office akaenda kariakoo kufuata spare, akaja mteja na pasi yake ya Phillips regulator ilikuwa ngumu kidogo kwenye kuzungusha

Nikajitia bingwa nikaforce ikavunjika, nikapambana nikaifungua pasi nikaibana ile regulator na wire kisha nikairudishia. Mwenye pasi akakuta ndio namalizia.. Ile kutest kwenye umeme lilipiga bonge la shot, mimi kule pasi kule mteja mbio[emoji24][emoji23]
Nikatimuliwa nisionekane tena pale jamaa akaingia hasara ya kulipa pasi

2. Kitaa kikawa kigumu mno. Siku moja nikatembea mpaka Mugabe Sinza, nikakuta mchina anafungua duka la dawa! Nikajifanya mimi mfamasia nikapata kazi
Kuna siku nimeachwa peke yangu akaja mdada mwanae ana pumu kali sana nikamwandikia dozi dokta uchwara mimi. Kumbe sikumpa ya pumu bali ya kushusha pressure.. Mtoto wa watu aliponea tundu la sindano kurudisha number.. Na siku hiyo ndio ilikuwa ya mwisho kuitwa dokta, nilitimuliwa kazi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]...daaah! Kweli mkuu upo vizuri kwenye kujizima data.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Naomba unijuze kuhusu freelancer, mana nmejiunga juzi nmepata kazi lkn mshahara ni mkubwa kiasi nahisi jamaa anataka kunizunguka.
Ni issue pana sana.

Client ni wawapi?
Payment method iko verified?
Ana reviews ngapi?
 
Siku ingine bana nikasindikizwa kuacha kazi na walevi wenzangu[emoji28][emoji28][emoji28]
nilikua na jimama langu jitu la deal mishen town.
Deal likiitika tunachezea dollar tu , tatizo matumizi yake sasa
Ni pombe na starehe tu mpk hela iishe
Hela ikiisha mi naenda kutafuta kazi yoyote mradi tu nizugie zugie.
Kipindi fulani tuko apeche alolo nikachukua deiwaka fulani msasani mwisho kule muitaliano.
Bartender
Dah manyanyaso km yote
Nikawa namvumilia tu
Miezi miwili
E bana huku jimama deal likaitika kalamba midollar ya kutosha.
Kazi mi siitaki pia.
Aah siku hiyo tumeanza na supu na bia zikanoga weeh.
Jioni natakiwa mzigoni.[emoji23][emoji23][emoji23]
Namuaga jimama anasema weeeh uende wapi?
Kazini.
Unalipwa ngapi?
Sijui ilikua buku70000 enzi hizo.
Nikapigwa dola elfu moja.
Hakuna kufanya kazi kaa nyumbani[emoji16]unilee.
Twende ukaache kazi[emoji28][emoji28][emoji28],
Hapo kuna wapambe wanne na sisi mtu 2 tuko sita.
Vuta mashine hadi kazini.
Ile tunaingia tu bosi kaniwai we unakuja sa hii umechelewa hivi mineno kibao.
Alikula kikumbo nikazama bar anatoa macho.
Jimama na wapambe wameingia nikawapa kinywaji cha kutosha na nikatoka nikakaa nao.
Bosi anashangaa tu[emoji28][emoji28][emoji28].
Mwisho namuita namwambia naacha kazi kata hizi bia hapa kwenye mshahara nakudai[emoji28]
nigee chenchi yangu tuondoke.
E bana jamaa alichoka.
Anasema si umalize kazi kwanza alafu uje siku ingine.
Nikamwambia siji tena hapa we fanya nilichosema.
Hapo wapambe wa jimama sasa yani wanamtamani mzungu.
Wanasema unamchelewesha nenda counter chukua hela zote tuondoke.
Bahati yake aliwai kuleta hela tukatimua.

[emoji23][emoji23][emoji23]wewe kiboko
 
Nilifanya Ile kazi ya kutembeza mabeseni ya sero na viti vyao mzigo nachukua River Side napanda daladala had banana then naanza kutembea had kitunda Kuna siku nilfika karibu na chanika na sikuuza chochote
Ningekuwa mimi nachukua mzigo mwingi nauza pesa sirudishi nasepa 😃
 
Niliwahi kuona tangazo la kazi zuri kwenye nguzo ya umeme nikaona bora niwafuate nikapate hiyo kazi kwasababu vigezo ninavyo. Kufika Ngarenaro kwenye ofisi zao kumbe ni wale jamaa wa kutembeza vyombo ambapo muhimu ni kuwa na shati la mikono mirefu na tai. Yule dada niliyemkuta alijawa na roho ya huruma na kuniambia kwa kweli wanataka vijana ila kwa elimu na mwonekano wangu hata yeye haafiki mimi kufanya ile kazi ila kama nitalazimisha fresh tu kesho niende nikaanze. Ikabidi nimsikilize. Wakati narudi home nikaona wasabato kanisa la mjini kati wako kwenye shughuli yao ya Makambi hali ni mida ya lunch ikabidi nijiunge kwenye foleni kupiga msosi. Hiyo wiki nzima mida ya lunch nikawa nakula kwa wasabato. Sintakaa nisahau. WASABATO ninawashukuru na nimejipanga nitafute hata kanisa lao jipya ninunue vyombo vya muziki kama shukrani yangu.
Wewe ni kama mimi.

Yaani siku ya kwanza yule mdada akabeba vyombo tunazunguka naye mtaa kwa mtaa mimi namuangalia tu huku naapa nikirudi tena niitwe mbwa, hiyo sanawari,kijenge hadi
 
Tulienda kuiba vifaa vya ujenzi kwenye kampuni ya ujenzi..
Hakuna siku nilikuwa natetemeka km siku hiyoo..baridi kali ya usiku lakini nilikuwa nasweat balaaaa..
Tulifanikiwa tukapiga ela safii kbss.
Roho ya tamaa ya uwizi ikataka kuanza kuniandama.
Nikaikemea roho hiyo chafuu.
Wale wenzangu walinipa mchongo walipigwa shaba wawili wawili wengine walikuja kuiba kanisani wakasomewa ufunuo ni vichaa siku hizi
[emoji3516]
KUNA WATU WATASEMA "Hii ni Chai!!!",
ILA ACHA NAO, USIWAZINGATIE MKUU.
 
Nimekumbuka mbali,
Kwanza baada ya kumaliza chuo michongo ikawa inagoma. Nikamtafuta uncle wangu fundi ujenzi nikawa napiga vibarua saidia fundi *****. Yani darasa la saba ananipelekesha mtu na degree yangu roho ilikua inaniuma mbaya. Zege za magorofa nimepiga sana, aisee zile kazi inatakiwa marobot ndo yafanye sio binadamu. Kuna hiyo ilikuwa ya kupandisha tofali gorofa ya tatu duh hiyo niligoma nikalala geto. Yani mtu anapandisha tofali ikifika jioni mabega yamechubuka balaa.
Niliacha saidia fundi baada ya mwaka mmoja nikapata sehemu ya kujitolea kwenye taasisi moja ya serikali lakini tulikua hatulipwi hata mia mbovu na kazi tunafanya. Ilikua ni mwendo wa lisaa na nusu kutembea kwenda na kurudi. Hapo narudi geto hamna masosi wala nini labda nimgongee bi mkubwa ndo anifanyie muamala ndo nile.
Baada ya hapo nilifanya miezi sita nikaacha nikapata intern kwenye taasisi fulani ya serikali. Maisha hapo yakawa afadhali kidogo.
 
Ile kazi ni ngumu sana kaka hasa kwa mazingira ya dar es salaam. Kondakta anasimama siku nzma,matusi ya abiria,usumbufu wa trafki nk. Ila kwa kipindi nafanya hii kazi hela ilikuwepo nilisave sana hela nakumbuka kila wiki nilikuwa naweza kuweka benki 150,000. Kwa tuliosoma soma kidogo kufanya ile kazi inabidi ujitoe aibu kabisa coz nakumbuka kuna siku natoka mwenge stendi gari imetema balaa naenda tegeta nimebembea mlangoni chini nawaina jamaa nimesoma nao chuo wamekula moka kali na wakaniita Ommy bro ni wewe? Nikawaambia ndio ni mimi nipo town tuonane wkend mazee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu unaweza kukuta hao jamaa zako waliopiga moka Kali mfukoni wakawa na buku jero tu ya nauli mkuu , haya maisha we acha tu Kila mtu anasiri yake .
Cha msingi we fanya kitu ambacho kina manufaa kwako usimuangalie mtu , ili mradi usiibe Cha mtu

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kumaliza chuo 2018 michongo iligoma kabisa, baada ya kuzurula Sana kutafuta ajira Siku moja nilikutana na Jamaa mmoja kwenye daladala baada ya story mbili tatu akanambia amepata kazi Aghkhan anatafuta chumba cha kupanga.

Wazo likanijia nikamwambia mimi ni dalali na Kuna vyumba viko vinapangishwa maeneo ya ubungo na kimara navifahamu na ninaweza kumsaidia kupata chumba kwa malipo ya pesa mwezi mmoja, hapo sio dalali na wala hivyo vyumba sivijui vilipo tukakubaliana tukutane siku ya pili nimpeleke akavione hivyo vyumba.

Siku ya pili nikaamka asubuhi na mapema nikaenda maeneo ya ubungo Riverside nikatafuta madalali wa pale nikampata mmoja nikampanga nikamwambia mimi ni dalali na Kuna mteja anahitaji chumba cha kupanga nikachukua mwasailiano yake na tukakubaliana baadae nije nae, nikaenda kimara nikatafuta Dalali nikampanga pia.

Badae jamaa akanicheki nikampeleka Ubungo Riverside akacheki vyumba hakuvipenda, nikampeleka Kimara akacheki akapenda hapo chumba sebule na jiko 200k akalipa akanipatia 200k nikamgawia dalali 100k.

Hiyo siku ndo niligundua udalali unalipa nikaanza kuwatafuta madalali kupitia Instagram wakipost nyumba na mimi nazichukua napost nikipata mteja namcheki muhusika nampanga naenda na mteja tunapangisha tunapata pesa, hadi baadae nikaja kua dalali mkubwa Sana Dsm na nikawa nawateja wengi Sana lakini nilikuja kuacha udalali 2021 baada ya kupata mchongo wa kueleweka.
 
Back
Top Bottom