Ni kheri ufiwe na mzazi kuliko kufiwa na mume/mke

Mkuu pole sana. Ila inaonekana we huna huruma na ni mbinafsi sana. Yan unahisi kufiwa na mke kunauma kuliko kufiwa na mzazi just imagine watoto wanajisikiaje kumpoteza mama yao. Ubinafsi ni pale unahisi wewe ndio mwenye maumivu wao hawana maumivu that is not fair. Kuwa na fikra pengine ndio inapelekea haya maumivu kuchukua muda sana kupona.

Hebu kuwa strong kwa ajili ya familia yao kwa sababu hata wao wamepoteza mama.
 
Amka mkuu kumekucha.

Yaani ktk ulimwengu huu huu unadiriki kusema ni kheri ufiwe na....kuliko kufiwa....?
Huu mlinganyo wako kwa upande wangu siyo sahili.
Kifo kisikie mbaaaali na siyo kufiwa na yeyote wa karibu nawe iwe ni ukaribu wa damu ama uhusiano wa kirafiki (mahusiano).
Pengo linalo achwa na mwanadamu kutokana na umauti halizibiki.
 
Umenea vyema mkuu.
 
Pole sana! Ujaliwe ujasiri wa kukabiliana na hali halisi.
 
Mimi yote yaliishanitokea. Nilifiwa na baba; nikafiwa na mama; nikafiwa na mtoto; na mwisho nikafiwa na mke. Hapo katikati nilifiwa na kaka watano na dada watatu. Kila kimoja wa vifo hivyo kina uzito wake. Huwezi kulinganisha kwamba afadhali hiki kuliko kile.
 
Yaani mimi nina hisi huyu ndugu yetu ana msongo wa mawazo (matatizo ya kiakili).
 
Pole sana kwa misiba mizito!
 
Sema basi lkn nilitaka nikwambie hivi;
Hivi km mkeo angekuwepo ukamwambia afanye uchaguzi wa kumuua mtu mmoja kati ya mzazi wake ama wewe mmewe unadhani angelimchagua nani?
 
umekufuru ile mbaya
unafananisha mzazi na mambo ya kijinga aisee
Ukiwa umepata ugonjwa mkubwa wewe ni wa kitandani muda wote, umefulia huwezi kuhudumia mke na watoto

Mke anaweza kukukimbia ila kuna mtu anaitwa mama huyo atashikamana na wewe na kukuhudumia, kukutunza na kukutia moyo mpaka ufe au upone na kurudia hali yako
 

Pole sana mkuu
Mshukuru Mungu kwa uhai wake, mshukuru kwa watoto
Pambana kusimama kwenye nafasi yake kwa watoto wenu3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…