Ni kilimo kipi hicho ambacho Raisi anatamba sana kukikuza? Sikioni mimi, wewe unakiona?

Kabla hujakosoa waulize watu wa Kilimanjaro na Arusha kuhusu bei ya kahawa kwasasa...

Waulize watu wa Tabora kuhusu bei ya tumbaku...

Fructuation imebaki kwenye mazao ya chakula na bustani tu, nako sio kubaya sana...

Tusikosoe tu, tupongeze kwenye mazuri pia...
 
Kilimo cha chakula, kimekuwa ni cha kibiashara, kinalipa kuliko hayo mazao ya biashara.
 
Mazao yote ni ya biashara
Sasa ndiyo yamekuwa hivyo.

Zamani tanzania, mpaka shule walijaa watu ujinga kuwa kuna mazao ya chakula na mazao ya biashara.

Bashe na Mama Samia wamebadili ujinga huo.
 
Sasa ndiyo yamekuwa hivyo.

Zamani tanzania, mpaka shule walijaa watu ujinga kuwa kuna mazao ya chakula na mazao ya biashara.

Bashe na Mama Samia wamebadili ujinga huo.
Zamani ipi?
Tangu enzi za kabla na wakati wa Ukoloni Watanzania wamekuwa wakiuziana vyakula, Tangu enzi za Mkapa Watanzania wamekuwa wanauza vyakula nje ya nchi.
 
Mkoa wa pwani hapo zao lao kuu ni Korosho msimu uliopita mvua zimaharibu korosho at large korosho zimeoza mtini kosorosho haijauzika minada michache kabisa hakuna intervention yoyote kusidia watu wale bei wanapanga nakuamulia jukwaani BBT a failed project iliyokusanya mayuvisisiemu bajeti imeongezeka kwenye matumizi yakawaida mkulima wa kawaida ananufaikaje?
 
Kabla ya Bashe kuwa waziri wa kilimo.
Tangu enzi za kabla na wakati wa Ukoloni Watanzania wamekuwa wakiuziana vyakula, Tangu enzi za Mkapa Watanzania wamekuwa wanauza vyakula nje ya nchi.
Hata kabla wazazi wake Bashe hawajaja kutoka Somalia nchi hii watu walikuwa wakifanya biashara ya mazao.
 
Na hata hizo pembe jeo zikipatikana kuna kuwa na BANDIA ambazo zinaumiza tena mkulima.

Acha tulime mchicha mabondeni
 
Drama tupo
 
Tuulize sisi wa Vijijini tukujibu.
Kwa nini tunaagiza Ngano na mafuta yq kula kutoka Ukraine, Russia na Malaysia.
Kwa nini tunaagiza apples kutoka South Africa?
Kwa nini tunaingiza Juice kutoka South Africa, Malawi na Kenya?
Kwa nini tunaingiza maziwa kutoka Uarabuni??
Kwa nini tunaagiza sukari kutoka Brazil?
 
Ukiwa mjini huwezi kuona kinachoendelea utaendelea kulalamika tu.
Kutokana na usimamizi mzuri wa Bei mfano tu ufuta mwaka huu uzalishaji kwa mkoa kama mtwara umepanda kwa asilimia karibia 58
Mwaka Jana ilikuwa Tani 17000 ila kwa mwaka huu umefikia 28000 na Bado wanaendelea kukaa misitu
Ukweli ni kwamba sio lazima muone viwanda ila uzalishaji ukiongea viwanda vitakuja tu
 
Serikali ya CCM ikisha ona Raia wamevuna sasa ndio inaibuka kujisifu bila kujua mkulima ameteseka kiasi gani haswa na gharama kubwa sana za pembejeo.
 
Sasa kama wote mliotangulia mlikuwa busy na Sgr na maendeleo ya mjini tuu ulitegemea nini? Samia ndio ataondosha Hilo na kazi zinaendelea kukamilisha jambo Hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…