Ni kilimo kipi hicho ambacho Raisi anatamba sana kukikuza? Sikioni mimi, wewe unakiona?

Ni kilimo kipi hicho ambacho Raisi anatamba sana kukikuza? Sikioni mimi, wewe unakiona?

Urea inayoitwa ya ruzuku tunauziwa 64000 wakati dukani tukinunua 67000,,,,dudu all tukiuziwa 30000 dukani ila ruzuku ni 29500,,,sulphur chapa mtende tukinunua mfuko 42000 ila hii ruzuku ni 44000
Hiyo ya dukani imetoka wapi zaidi ya kuiba ya ruzuku
 
Ila kilimo ni kama kubet.....mwezi july kilo ya vitunguu ilikua 5000tsh wakulima nadhani walichekelea, leo kilo 2000tsh na hapa tunaelekea hadi kilo tsh 600
Huku jijini kilo 1000 na watu wa dar wapendavyo hela ila hiyo ndo bei yake
 
wakulima wanapelekewa sulphur ya mo dewj ambayo haina ubora kabisa ila ndio wanalazimishwa waichukue
 
Kilimo nchi nyingi kinalipa sana na hata ukiona mtu anaendesha V8 ukaambiwa ni mkulima basi ujue ni nchi inayojielewa na kuwajali wakulima na hata wafugaji
Wanataka watu wawe matajiri kwa kulima na jembe la mkono ambalo kuna watu waliliacha miaka 200 iliyopita
 
Nchi hii inaendeshwa na vilaza ambao silaha yao kuu ni kulipa machawa wa kuwasifia.
Unakuta mabango yakisifia biashara ya nje imeongezeka Mara dufu wakati uhalisia Kuna uhaba mkubwa wa dola.
Ni aibu kwa nchi ambayo ilikuwa na viwanda vyake vyenyewe vinazalisha zana za kilimo Kama majembe, panga, fyekeo, machepe Leo hii vitu vyote vinatoka china.
Ndio maana wafanyabiashara kariakoo wakigoma serikali inatetemeka.
 
Ukienda Kanda ya Ziwa kilimo cha pamba kimekufa na ile mikoa sasa ina idadi kubwa sana ya masikini kwa sababu moja ya zao walilo kuwa wanategemea sana enzi na enzi lisha kufa.

Kahawa mikoa ya kaskazini inaendekea kufa,Kilimanjaro kule hakuna mtu anataka kulima kahawa tena, kote huko Arusha na kadhalika.

Zilizo kuwa shule za michepuo ya kilimo zisha jifia zote, sasa kilimo kipi tunakuza? nenda tembelea kwenye vyuo vya kati vya kilimo uone vilivyo choka mbaya. Huwezi zungumzia Kilimo bila kusapoti elimu ya Kilimo.

Zamani tulikuwa na kiwanda kama ZZK Mbeya suna hakika kama kipo au kisha badilishiwa matumizi,unaweza kuta watu wanafugia mbuzi kwenye majengo ya kiwanda.

Kwa sasa hadi fyekeo tuna import then tunakuja kudanganyana kwamba tumekuza kilimo. Nchi imejaaa hadaaa sana hii

Bado wakulima wa mazao mengi wanalia na changaniti zikiwemo Bei kubwa sana za pembejeo, ikiwemo madawa, Mbolea na Mbegu. Bei ya mbegu tu kama za mahindi imekuwa inapanda kila msimu mpya wa kulima na haijawahi shuka bei kabisa.

Ukiuliza wakulima wengi wana pambana wenyewe hakuna sapoti wanayo pata kutoka Serikalini.

Raisi nazani anazungumzia yale mashamba ya Bashe, yale mashamba ya mchongo ,ila kilimo kama kilimo bado sana, Wakulima wanapambana wenyewe mwanzo mwisho.

Serikali ya CCM ikisha ona Raia wamevuna sasa ndio inaibuka kujisifu bila kujua mkulima ameteseka kiasi gani haswa na gharama kubwa sana za pembejeo.
Wewe akili yako ina shida mahali
 
Back
Top Bottom