Ni kilimo kipi hicho ambacho Raisi anatamba sana kukikuza? Sikioni mimi, wewe unakiona?

Urea inayoitwa ya ruzuku tunauziwa 64000 wakati dukani tukinunua 67000,,,,dudu all tukiuziwa 30000 dukani ila ruzuku ni 29500,,,sulphur chapa mtende tukinunua mfuko 42000 ila hii ruzuku ni 44000
Hiyo ya dukani imetoka wapi zaidi ya kuiba ya ruzuku
 
Ila kilimo ni kama kubet.....mwezi july kilo ya vitunguu ilikua 5000tsh wakulima nadhani walichekelea, leo kilo 2000tsh na hapa tunaelekea hadi kilo tsh 600
Huku jijini kilo 1000 na watu wa dar wapendavyo hela ila hiyo ndo bei yake
 
wakulima wanapelekewa sulphur ya mo dewj ambayo haina ubora kabisa ila ndio wanalazimishwa waichukue
 
Kilimo nchi nyingi kinalipa sana na hata ukiona mtu anaendesha V8 ukaambiwa ni mkulima basi ujue ni nchi inayojielewa na kuwajali wakulima na hata wafugaji
Wanataka watu wawe matajiri kwa kulima na jembe la mkono ambalo kuna watu waliliacha miaka 200 iliyopita
 
Nchi hii inaendeshwa na vilaza ambao silaha yao kuu ni kulipa machawa wa kuwasifia.
Unakuta mabango yakisifia biashara ya nje imeongezeka Mara dufu wakati uhalisia Kuna uhaba mkubwa wa dola.
Ni aibu kwa nchi ambayo ilikuwa na viwanda vyake vyenyewe vinazalisha zana za kilimo Kama majembe, panga, fyekeo, machepe Leo hii vitu vyote vinatoka china.
Ndio maana wafanyabiashara kariakoo wakigoma serikali inatetemeka.
 
Wewe akili yako ina shida mahali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…