Ni kipi cha thamani kwa mwanamke kati ya kitanda na mwili wa mwanaume?

Ni kipi cha thamani kwa mwanamke kati ya kitanda na mwili wa mwanaume?

Kuzini ni dhambi, lkn mnzizi alieenda lodge na aliezini madhabahuni unadhani ni sawa? Tunakubaliana kwamba kuchepuka sio kuzuri lakini bora ukafanyie mbali kuliko nyumbani .

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app

Unamaanisha ukiiba Biblia utaenda Peponi?
 
Sasa huwezi chepuka ukasema uende kwenye kitanda ambacho mke wako analala akitoka mihangaiko. Hizo ni dharay na dharau ni matokeo ya kuvunja heshima. Elewa ndugu. Or else utupe kwanza maana ya heshima unayoijua ili tukocoment accordingly.

Nimeuleta msemo kama unavyotumika na watetezi wakitaka kuchepuka nanukuu, " siwezi kulala na mwanamke asiyekua Mke wangu kwenye Kitanda chetu na Mke wangu, itakua kumvunjia heshima". Kutoka kwenye hiyo nukuu, nikaona kumbe suala la kuchepuka tayari linaisuta nafsi Sina shida hapo, utata unaanza kama mtu anaona sio sawa kunajisi Kitanda na mchepuko, mwili wake si ungekua wa kwanza kutunzwa asipelekewe mchepuko?

Hapo Sasa nikahitimisha ukishaona umefika maamuzi ya kuchepuka, usijifariji Kwa kuheshimu Kitanda au kuvua Pete, wewe endelea tu ukiwa tayari kuyapokea matokeo ya maamuzi Yako.
 
Tambua tu kwamba mwanamke akigundua umechepuka na kufanÿa zinaa tena kwenye kitanda mnacholala wote usitarajie heshima/upendo uliyokuwa ukiipata awali, na hii itakuwa pia ni chanzo cha Migogoro kwenu maana tayari mshaleta nuksi ndani maana ile image itakuwa inamrudia mkeo kila wakati na kumjaza hasira upya kila akikumbuka ulimsaliti katika mazingira manyoishi wote.

Lakini pia ni dharau ya kiwango cha juu mno kumleta mchepuko na kufanyia mapenzi katika kitanda chenu.atumie mataulo kanga za mkeo mashuka na vipodozi vya mkeo..
Kiimani kitanda ni madhabahu ile..ndipo mnapopumzika baada ya mizunguko yenu,kujadili mipango maono na malengo ya familia pia ndio mnapoongezea familia pale imagine unaleta mchepuko hapo hapo (akili mbovu kabisa hii).

Wanaume wa aina hii mara nyingi hawana hofu ya Mungu nafsini mwao ukijawa na Mungu ndani yako utajitenga na zinaa..imagine nyumba inavyumba zaidi ya kimoja lakini atamleta chumba cha mkewe sia ajabu wakatumia mataulo na kanga za mkewe (Mungu huwa anawaumbua).

Wanaume wengi wa aina hii ukichunguza zaidi wanafanya uchafuu huu wake zao wakiwa wajawazito au wakiwa wamekwenda likizo ya kawaida au kujifungua..tena wanawasindikiza kwa bashasha ili wapate space ya kufanya umalaya.huku ni kukosa utu kabisa
 
Tunapoelekea mwisho wa mwaka, nikaona nijaribu kuleta kwenu hii hoja ambayo imekua ikiibuka Mara nyingi hasa Kwa wanandoa wanaume.

Hapa naongelea Mme ameoa, anaamua kuchepuka anasema hawezifanya hicho kitendo na mwanamke mwingine kwenye Kitanda anacholalia na Mke wake.

Sasa kama unamheshimu mkeo kiasi Cha kuthamini Kitanda unacholalia nae, mwili wako si ndio unatamani zaidi ya Kitanda? Kwanini umpe mwili wako mchepuko na kuhangaika kufanyia eneo lingine kisa heshima Kwa Mke wako?

Ukishaamua kusaliti, hua hapo hakuna Tena suala la heshima haijalishi utafanyia kwenye mti, vichakani, hoteli ya nyota 5 au ufukweni. Tuache kujifariji.

Niwatakie heri, afya njema na mafanikio wanajukwaa wote wa JF tunapoingia mwaka 2023.
Duuh
 
Back
Top Bottom