Ni kipi cha thamani kwa mwanamke kati ya kitanda na mwili wa mwanaume?

Ni kipi cha thamani kwa mwanamke kati ya kitanda na mwili wa mwanaume?

Kuna mahali haupo sawa..au sija kuelewa.kwaio tusichepuke au?

Hapa mjadala sio kuchepuka au kutokuchepuka mkuu, tuanza kujadili Hilo tutajaza servers za JF bila kufikia makubaliano. Tupo Kwa mchepukaji anapopunguza maumivu ya usaliti Kwa kuonyesha heshima ya mwenza anapokataa kutumia Kitanda akiwa na mchepuko au kuvua Pete wakati mwili ambao ndio kitendea kazi anaukabidhi Kwa mchepuko.

Hapo ndio swali linakuja, kati ya mwili na Kitanda, kipi ni Cha Thamani Kwa mwenza?
 
Hapa mjadala sio kuchepuka au kutokuchepuka mkuu, tuanza kujadili Hilo tutajaza servers za JF bila kufikia makubaliano. Tupo Kwa mchepukaji anapopunguza maumivu ya usaliti Kwa kuonyesha heshima ya mwenza anapokataa kutumia Kitanda akiwa na mchepuko au kuvua Pete wakati mwili ambao ndio kitendea kazi anaukabidhi Kwa mchepuko.

Hapo ndio swali linakuja, kati ya mwili na Kitanda, kipi ni Cha Thamani Kwa mwenza?
Mimi nazani nikitanda.
 
Tunapoelekea mwisho wa mwaka, nikaona nijaribu kuleta kwenu hii hoja ambayo imekua ikiibuka Mara nyingi hasa Kwa wanandoa wanaume.

Hapa naongelea Mme ameoa, anaamua kuchepuka anasema hawezifanya hicho kitendo na mwanamke mwingine kwenye Kitanda anacholalia na Mke wake.

Sasa kama unamheshimu mkeo kiasi Cha kuthamini Kitanda unacholalia nae, mwili wako si ndio unatamani zaidi ya Kitanda? Kwanini umpe mwili wako mchepuko na kuhangaika kufanyia eneo lingine kisa heshima Kwa Mke wako?

Ukishaamua kusaliti, hua hapo hakuna Tena suala la heshima haijalishi utafanyia kwenye mti, vichakani, hoteli ya nyota 5 au ufukweni. Tuache kujifariji.

Niwatakie heri, afya njema na mafanikio wanajukwaa wote wa JF tunapoingia mwaka 2023.
Nadhani logic ni anaweza kurudi ghafla akakukuta
 
Nadhani logic ni anaweza kurudi ghafla akakukuta

Kuna Rafiki yangu yeye alikua anaishi mbali na familia yake, ni msomi mwenye nafasi ya juu kabisa tukiwa nae kazini, hii ilikua ni kanuni yake kwamba hata akipeleka mtu kwake, wanamalizana chumba Cha wageni.
Alikua mtu wa kujali sana Mila na tamaduni zao, ndio Mtu wa kwanza kumuuliza hili swali kwamba kama nafsi inamsuta kuhusu Kitanda, mwili wake sio Bora na Thamani Kwa Mke wake? Alibaki anacheka tu.

Huyu unaona kabisa suala la kurudi ghafla akafumaniwa halipo, Mke wake alikua akiishi nchi nyingine kabisa.
 
Naona umechoka🤣🤣

Hapana, ni busara kuheshimu mitazamo na maoni ya watu. Unajua licha ya kuandika chochote, amechukua muda kuusoma Uzi wako, akaamua kuandika kitu, ni busara kuthamini muda na mchango wake.

Nasubiria lipa namba usijekuwekwa rumande Kwa mangi
 
Okay, hii kwa mtazamo wangu ipo na pande mbili. Wewe unaandika zaidi kwa msaliti yaani mtenda usaliti.

Ila kwa mtendewa ni tofauti. Kinachoumiza zaidi kwenye usaliti ni hisia na kumbukumbu. Unapomsaliti mtu na asijue mazingira ambayo usaliti umetendeka inakuwa tofauti na umemsaliti na anajua ni katika mazingira gani hilo jambo limetokea.

Fikiria nyumba mnayoishi pamoja, au kitanda mnacholala pamoja na mpenzi wako leo unapata kumbukumbu mpya za mpenzi wako kuwa hapo kimapenzi na mtu mwingine.

Sijui nielezee kwa namna gani ila ni namna gani unaweza kulalia hicho kitanda au kutazama mazingira ya hiyo nyumba bila kupata picha ya mpenzi wako akiwa uchi na mtu mwingine? Inakuchelewesha ku heal ama ku move on hata kama umemsamehe au hata kama haujamsamehe ila unaendelea kuishi kwenye hiyo nyumba.

Namfahamu mtu ilibidi auze gari yake baada yamke wake kukataa kulitumia baada ya kujua alifanya mapenzi na mwanamke mwingine kwenye hilo gari. Unaweza ukashangaa kwamba, mbona anaendelea kutumia dick ambayo ilitumika kwa mwanamke mwingine na sio gari lililotumiwa tu?

Hisia na kuvuta picha namna tendo lilivyotendeka ndiyo inaumiza zaidi na unachelewa kusahaulika kuliko hata huo usaliti wenyewe.

Sasa kwa watenda jambo, ili kuepusha haya ndiyo maana wanaona ni bora kwenda kufanyia mbali kwamba hata mwenza wake akijua matokeo yake yanakuwa tofauti. Japo yeah, cheating is cheating .

Unajua nimeandika na kufuta mara ngapi? Hadi ninatamani kulia.
Pole sana, Umepona au Bado Moyo unajeraha?
 
🤣🤣🤣Mkuki kwa nguruwe
Amna, unajua inabidi NATURE ifanye kazi yake ndio maana waswahili wakasema MAFAHARI wawili hawawezi kaa ZIZI moja. Means wanaume wawili hawawez ishi nyumba moja na Mke mmoja, ila kwa Wanawake hata wawe kumi Mwanaume Mmoja wanaweza ishi.
 
Hapo mimi ninaona inategemeana na dhamiri. Sasa ili dhamiri isikutese unakuta unajisemea aaaah lakini sijatumia kitanda kile kile😂😂
 
Back
Top Bottom