Kuna jambo ambalo tangu utoto nimekuwa nikilisikia na wengi kuliamini, kuna kitu kinacheza juu au chini ya kope za jicho.
Huko bara wana amini jicho likicheza upande wa juu huwa ni bahati hivyo tarajia kupata taarifa njema, lkn kuna Imani kwamba jicho likicheza upande wa chini ni dariri ya kutoa machozi, hivyo tarajia taarifa mbaya kama misiba, magonjwa au kupoteza pesa na kadhalika.
UZOEFU WANGU:
Nimekuwa nikitokewa na vitu hivyo: 80% baada ya kufuatilia nimejikuta ikitokea hivyo. Mfano upande wa juu wa kope za jicho langu ziliwahi kuwa zinacheza, (yaani kinakuja kitu kama mtetemo), kwa muda wa wiki mbili, baadae nilipigiwa simu kuitwa kwenye interview na nikapata kazi, kuna matukio mengi mengine siyakumbuki lkn nakumbua pia ilinitokea wakati nasubiri matokeo ya mtihiani ambao nilifauru vizuri sana, kwa kifupi ikitokea mara nyingi huwa napata good news ambayo sikutarajia. Lakini pia niliwahi kutokewa upande wa chini wa jicho, niliogopa sana. Nilikaa kimya na baade nilipata taarifa za msiba, kuna wakati nilipata taarifa za magonjwa. Hali hii huwa haitokei mara kwa mara.
Kuna Imani kwamba ikiwa unatokewa na jicho kucheza upande wa juu yaa ni juu ya kope usimwambie mtu kwaani unaweza kufukuza bahati.
Anaefahamu ukweli wa hili jambo atujuze, MSHANA JR tunaomba elimu yako ya kiroho hapa.
Aksante.