Ni kipi chanzo na tiba ya misuli ya jicho kutikisika?

Ni kipi chanzo na tiba ya misuli ya jicho kutikisika?

Ninavyofahamu na kutokana na kufuatilia kwangu sijui wengine,jicho la kulia uliposema likicheza ni kuwa kitu kizuri kinakujia,la kushoto nikiongezea ni kuwa kitu kibaya chaja,ni upande wangu mimi,sijui wengine
 
Mostly itakuwa umezidisha kiwango cha caffeine kwenye damu yako! Aidha kwa kunywa chai iliyokolea majani kwa wingi, Soda kama cokacola au pepsi au azam cola unatumia kwa wingi, pia kahawa inasababisha.

So kama unatumia sana hizo vitu fanya kama unazipunguza au kuziacha kwa muda na anza kutumia maji kwa wingi at least 3 litres per day ili uweze kuregulate kiwango cha caffeine kwenye damu na kuipunguza kabisa. Na utaona utakuwa poa kabisa na utakuwa normal
 
Mimi mara nyingi nyama ya juu ya jicho la kulia hucheza nini maana yake? Mshana naomba unijuze.
Usikubali kuamini kuna kitu kitatokea. Hizo ni imani tu. Mara nyingi jicho linapocheza inaonyesha kuna kitu hakipo sawa kwenye mwili wako. Kwa mfano mimi nanyemelewa na homa kama malaria, au flue au ninapokuwa na uchovu wa kupitiliza hii hutokea. Kuna mdau mmoja King Kong III amekujibu vizuri sana.
 
Wataalam tunaamini Kutikisika kwa jicho la kulia ni ishara ya Mtu kukaribia Kujifungua iwe wewe mkeo au ndugu yako, Kutikisika kwa jicho la Kushoto huwa ni ishara ya kupokea Mgeni, au Kuona kupata balaa fulani
 
Kuchezwa na Makalio Pia Si Alama Mbaya kama Watu wadhaniavyo, Ila Huwa ni signal ya Chakra ya Mwisho Kiunoni, maana Yake ilikiwa ni kuimarika katika Uaminifu.
Siku ukichezwa na makalio naomba uniambie.
 
Na kucheza sehemu ya mwili je labda mkono karibu Na kwapa mana imekuwa ikinitokea sana mda mwingine hata kwenye shavu
 
Nawasalimu wanaJF

Poleni na mihangaiko ya hapa na pale.

Mimi leo kuanzia asubuhi nimeamka jicho langu moja la upande wa kushoto kwenye kope kwa juu lina vibrate... (linacheza cheza)

Mwenyewe kujua tatizo hili linasababishwa na Nini?

Je, kiafya likoje?

Tafadhali wajuzi wamambo wanijuze maana linanikera sana.

Natanguliza shukrani.. 🙏🙏🙏🙏

Karibuni!!!..
 
Nawasalimu wanaJF

Poleni na mihangaiko ya hapa na pale.

Mimi leo kuanzia asubuhi nimeamka jicho langu moja la upande wa kushoto kwenye kope kwa juu lina vibrate... (linacheza cheza)

Mwenyewe kujua tatizo hili linasababishwa na Nini?

Je kiafya likoje?

Tafadhali wajuzi wamambo wanijuze maana linanikera sana.

Natanguliza shukrani.. [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Karibuni!!!..
Normal muscle twitching. Hakuna uhusiano wowote na jambo baya ni imani tu.
 
Mi huwa linacheza ila siaminig ayo ya jambo jema au baya uwa linacheza likichoka linaacha lenyew na akitokei kitu
 
Back
Top Bottom