Ni kipi kifanyike ili kuondoa wizi maofisini na katika mashirika ya Kiserikali?

Pslmp

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2021
Posts
1,622
Reaction score
2,458
Toa maoni yako hapa,

Jambo gani lifanyike ili kudhibiti wizi wa Mali na fedha za serikali?

Je, mishahara ni kidogo?
Marupurupu yaongezwe?

Unadhani ni kipi kiboreshwe ili kukomesha hali hiyo?
 
Bila kuwafanya wafanyakazi wathamini kazi zao kwamba zinawapa uhakika wao wa maisha ya sasa na baada ya kustaafu hakuna jinsi ya kubadilika.

Ikiwa mafisadi na mijizi ndio yanayo enziwa na kuheshimika katika jamii sababu ya mali zao nani hatataka kuiba ili kuvuna heshima katika jamii?
 
Tatizo wafanyakazi wameshagundua wanasiasa wanafaidi zaidi keki ya Taifa. Hivyo wanapo pata nafasi na wenyewe wanajimegea.

Haiwezekani Mbunge anayejua tu kusoma na kuandika, anakaa miaka mitano tu Bungeni! lakini mafao yako ni zaidi milioni 200! Halafu mfanyakazi anayefanya kazi miaka 30-40, analipwa mafao ya milioni 60!
 
Mkuu, asante Kwa maoni yako, tunachotaka ni kutaka kukomesha kabisa uwizi, haijarishi fisadi ama mkwapuaji, ila tunataka tutoke hapa tulipo
 
Pointi kubwa Sana hii
 
Mkuu, asante Kwa maoni yako, tunachotaka ni kutaka kukomesha kabisa uwizi, haijarishi fisadi ama mkwapuaji, ila tunataka tutoke hapa tulipo

Alipe vizuri na marupurupu yawe ya kueleweka wakati wote mfanyakazi akiwa kazini na akistaafu. Hii itafanya kazi iwe ni secirity ya maisha ya mtu na ni ya umuhimu wa pili baada ya Mungu. Mwizi achukuliwe hatua stahiki kisheria na kuwekewa mazingira ya kumfanya asiwe na heshima kuanzia kwenye familia yake na jamii.
 
Toa maoni yako hapa,

Jambo gani lifanyike ili kudhibiti wizi wa Mali na fedha za serikali?

Je mishahara ni kidogo?
Marupurupu yaongezwe?

Unadhani ni kipi kiboreshwe ili kukomesha Hali hiyo
Kama zingetungwa sharia kali za kuwafilisi wahusika ingesaidia sana watu kuogopa wizi, ila shida ni kwamba watunga sharia ni wanamtandao hawawezi kutunga sharia zitakazo backfire
 
Bro uwizi upo na utaendelea kuwepo ishu ni sheria kali mzew kama china unanyngwa kweupe ila hapa kujuana kwingi mkuu akiwaita ofisi when no media to expose the conversation wanachekeana tu maana wanajuana sheria kali maana ukisema mshahata uongeze mshahara unazoeleka kaka hata upeww million 10 kwa wiki itakuwa kubwa at the begin ila ukiuzoea miaka kadhaa utademand upya

Sheria kali kaka ndo kila kitu nchi kama china ,korea huko ukifanya ufisadi huna maelezo ni kifo
 
Toa maoni yako hapa,

Jambo gani lifanyike ili kudhibiti wizi wa Mali na fedha za serikali?

Je mishahara ni kidogo?
Marupurupu yaongezwe?

Unadhani ni kipi kiboreshwe ili kukomesha Hali hiyo
Majibu yapo wazi kutokana na maswali YAKO,ila lazima sehem nyeti kua na uchambunzi yakinifu kabla ya kuteua mtu, mshahara huwa hautoshi siku zote that's utakuta mbunge Bado anakuja rushwa pitisha hoja ya serikali haliali anapata mshahara makubwa,tra hivyohivyo
So inaweza tungwa sheria kali kwamba nafasi flani tokana na unyeti wake ulipwe vizuri ila ikidhibitika umekula rushwa basi pigwa risasi adhalani ,hapo mtu agusi
 
Kama zingetungwa sharia kali za kuwafilisi wahusika ingesaidia sana watu kuogopa wizi, ila shida ni kwamba watunga sharia ni wanamtandao hawawezi kutunga sharia zitakazo backfire
Nakuelewa vema mkuu, unamaanisha kwamba, hata kukiongezwa mishahara haiwezi kuwa tiba ya uwizi siyo?
 
Majibu yapo wazi kutokana na maswali YAKO,ila lazima sehem nyeti kua na uchambunzi yakinifu kabla ya kuteua mtu, mshahara huwa hautoshi siku zote that's utakuta mbunge Bado anakuja rushwa pitisha hoja ya serikali haliali anapata mshahara makubwa,tra hivyohivyo
So inaweza tungwa sheria kali kwamba nafasi flani tokana na unyeti wake ulipwe vizuri ila ikidhibitika umekula rushwa basi pigwa risasi adhalani ,hapo mtu agusi
Rudia tena mkuu Kwa sauti kubwa, unamaanisha wapigwe....??
 
Nafasi za wakurugenzi wa mashirika zipatikane kupitia mchujo wa kamati za bunge kupitia michakato ya wazi wa mchujo na uajiri.
Unamashaka na mchakato wa kuwapata wakurugenzi siyo??

Inawezekana kuna rushwa inatumik kuwapata siyo?
 
Inawezekana hakuna rushwa ila inawezekana watu wanaoteuliwa wana uwezo mdogo sana au hawakidhi vigezo wa kuongoza hayo mashirika kwa sababu wanapatikana kwa kujuana zaidi badala ya merits

Mkuu,kumbuka hapa kinachowakumba karibu Kila ofisa wa serikali ni ufujaji wa fedha za Umma, na uwizi hauna mtu mwenye uwezo wa elimu n.k

Maana tumewaona wengi tu ambao wanauwezo mkubwa ki elimu lakini ndio yamekuwa majangili na mafisadi makubwa zaidi kama jamaa la nyoka wa makengeza

Au unamaanisha Uwizi uliopo unawahusu wasio na uwezo ki elimu pekee
 
Siongeli uwezo mkubwa wa elimu, nazungumzia azma na uwezo mkubwa wa uongozi ambao huenda tungeweza kuuona kama kamati za bunge zingekuwa zinawafanyia interview live inayoonekana nchi nzima wakati wa kuwaajiri.
Mkuu,kumbuka hapa kinachowakumba karibu Kila ofisa wa serikali ni ufujaji wa fedha za Umma, na uwizi hauna mtu mwenye uwezo wa elimu n.k

Maana tumewaona wengi tu ambao wanauwezo mkubwa ki elimu lakini ndio yamekuwa majangili na mafisadi makubwa zaidi kama jamaa la nyoka wa makengeza

Au unamaanisha Uwizi uliopo unawahusu wasio na uwezo ki elimu pekee
 
Inatia faraja sana kuona Mataga nao wameacha kuabudu na wanaungana na Wapinzani katika kutafuta solution, Nchi hii itajengwa kwa kuambiana ukweli.

Wapinzani sio maadui, wala sio Vibaraka wa Mabeberu Wapinzani ni watu Wema sana kwa Taifa hili.
 
Mkuu, hujatoa maoni yako juu ya hili!!
 
Back
Top Bottom